Monday, July 16, 2007

Bagamoyo Road

Leo nimekwenda mjini Bagamoyo, mkoa wa Pwani. Barabara safi kabisa. Ila magari yanaenda kwa kasi na wana overtake hata kwenye maeneo ya solid lines. Mji wa Bagamoyo unapanuka kweli, na hapajalala kama zamani.

Anayecheza kama Juma, Peter Omari amefiwa na alienda kuzika, hivyo nilikuwa na mapumziko kidogo.

14 comments:

Simon Kitururu said...

Tuletee picha za huko basi Dada Chemi!

Chemi Che-Mponda said...

Nitawaletea wiki ijayo.

Egidio Ndabagoye said...

Tutashukuru sana.

Anonymous said...

Bongo sio mchezo, kuna muda wa ku-post picha!!! Ni kubanjuka tuu!

Anonymous said...

DADA CHEMI MBONA UNANIDHARAU, HUTAKI KUNIJIBU SWALI LANGU NILO KUULIZA KAMA UNA MUME AU BOY FRIEND.

Anonymous said...

Chemi ninajiskia vibaya ninapoingia humu nakukuta kuko kutupu... aaaaaaah nimilipa vi mia 500 naishia kwenda kwa MICHUZI na MJENGWA vp u-busy sana??? Naomba usisingizie Internet za Bongo...

Anonymous said...

Tunazisubiri kwa hamu

Anonymous said...

Peter alifiwa nani tena!, Dada Chemi?

MICHUZI BLOG said...

usisahau kwenda badeco

Anonymous said...

vijana wanaomba mcheck blog yao
http://kamerayamwanafunzi.blogspot.com/

Anonymous said...

Nimeona Michuzi kakupa konyagi moja. Kwa hiyo ukirudi mjini tu, "nitakutembelea kukusalimia na kukupa pole ya safari," si unajua zetu waswahili? Najua sitakosa angalau kizibo cha konyagi, kwani wafanya mchezo eti.

Mie nipo hapa Amherst nakusubiri kwa hamu sana; bahati nzuri nimeshajua nyumbani kwako ingawa sijui simu yako. Kwa uswahili wangu sitaweka appointment yoyote ili nidhihirishe utamaduni wetu; nitajimwaga bila taarifa.

Anonymous said...

Tanzania sasa kumeendelea.
Wachina wameleta wireless internet technology ya bei ndogo ambayo hata ukiwa bagamoyo waweza pata internet ukiwa na simu na laptop yako tu.Uwe kwenye daladala,basi au unasafiri njiani kwa gari yako au baiskeli kwa kupitia TTCL mobile phone unapata intenet bila shida.

Internet cafe siku hizi wanaenda maskini wa kutupwa wasiokuwa na komputa nyumbani na watu wa kuja wabahili kama akina Chemi Chemponda ambao hawataki kununu TTCL Mobile ambayo inauzwa chini ya dola 100 za marekani.

Kuna mzungu mmarekani toka Texas alishangaa kukuta TTCL mobile Internet akiwa nayo mtu MASKINI mchovu kabisa MBAGALA,Temeke.

Ni aibu kutoka USA na kuja kufikia internet cafe CHemponda! Acha ubahili! Hata kama una save dola 100 Haziwezi kukuondolea ulofa!

Nilikushangaa kwenye blogu yako uliposema eti ulienda Internet Cafe! Nikakuona kama mtu unayeishi enzi za karne ya mawe(Stone age)!!

Wasomi na wenye hadhi Tanzania wana TTCL mobile .Pole wewe mchovu wa USA ambaye ukitoka huko unafikia kwenye ka-intenet cafe usome na kupokea mails.

Chemi Che-Mponda said...

anonymous wa 8:57am, Simu nyingi sana Bongo, mpaka housegirls, shamba boys wanazo, ila wanatumia sana kwa SMS. Kupiga ni ghali. Budgt yangu kubwa ilikuwa kununua hizo Tigo za 5000/- kila mara.

Kuhusu swali ya Boyfriend, ninaye na ni mpenzi mume wangu. Nangojea kumwona kwa hamu baada ya masaa kadhaa.

Anonymous said...

Da Chemi wekaga basi picha ya huyo shemeji hapa basi tumuonage hata siku moja ili tukikutana naye sehemu sehemu tujue huyuuu ndio shemeji letu.