Tuesday, July 24, 2007

Niko Dubai Tena




Haya ndugu wasomaji wapendwa, niko njiani kurudi USA. Niko Dubai Airport ni midnight (Saa sita za usiku) nangojea flight ya kwenda New York.

Samahani nilibanwa sana kwenye shghuli za sinema, lakini nadhani mtapenda sinema enyewe. Itatoka hivi karibuni. Hiyo Emirates ni ndege safi sana. Wanachukua soko ya British Airways / KLM etc. naona na Qatar Airways wameingia na bei nafuu za tiketi.

Mengine Kesho kutwa.

Na kwa yule aliyekuwa na wasiwasi....mbona nilikuwa na simu Bongo.

7 comments:

Anonymous said...

nimekubali emirates wako juu mnoo,,mi wananifuraisha hadi mao MAEAOSTEEEEZII wanaongea kiswahili,,na hawabanii unywaji ,,teh teh teh..

na hakuna *viubaguzi* vya kizushi vya waswazi na weupe,,nawafagilii kinomiiii

ila wapi picha za shootings ya filamu au *hairuhusiwi* kutoa kiduchu duchu,,kama unaibia vile,,?? ningependa scene za manzese,,am waiting,,,

KakaTrio said...

Da chemi ubaya wa izo ndege za arabuni ni pale zinapokuwa na stop nyingi kama dala dala na mizigo kupotea mara kwa maara na muda mrefu wa kusubiri connection.

Chemi Che-Mponda said...

Hizo nilizopanda zilikuwa non-stop Dubai/New York, Dubai/Dar na zilikuwa zimejaa!

Kwa kweli Emirates wana huduma nzuri sana. Ila ubaya kwa sasa wanafika New York tu hapa USA.

Na ni kweli crew zao ni COSMOPOLITAN, mchanganyiko wa makibila. Unakuta weusi, wachina, wazungu etc. kweenye kila crew na wanaongea lugha kama saba kwenye flight.

Anonymous said...

Waarabu macrews wanawake nao wapo??

Anonymous said...

Hongera kwa yote uliyofanya Bongo kuhusu hiyo filamu. Ombi ni lile lile nililoandika kwa Michuzi please fanya ufanyalo rekebisha hawa provider wa bongo wasiendeleze kero zao... kwenye internet

Anonymous said...

TARAAAAAA....DUBAI ON TRANSIT.NIPO DUBAI, NIPO DUBAI. CHEMI HAPO KAMA UNA GAMBA LAKO KAMILI UNASHUKA TUU BILA MATATIZO.
LAKINI KAMA UNA KARATASI AU GAMBA LAKO LISILO KAMILI (TRAVEL DOC) UTAISHIA HAPO HAPO NA KUNUNUA DUTY FREE MBILI TATU, HUYOOO KWENYE NDEGE.
RAHA YA DUABI, SHUKA NENDA MITAANI UKUONE MADUKA YA GOLD, DIRA NA MZAGAZAGA MENGINE. LAKINI SIYO KUPIGA PICHA ZA DUTY FREE SHOPS, MCDONALD YAO YA HALAL, NA NJIA YA KWENDA KWENYE MAGETI YA KUPANDA NDEGE...NIPO DUBAI NIPO DUBAI. UNGEOMBA KUTOKA NJE KIDOGO NDIYO UKADENGUA NA DUBAI. MAMBO SIKU HIZI DOHA KWA TAARIFA YAKO.

Anonymous said...

kweli mimi namuunga mkono mdau aliyempa changamoto da Chemi. Kwa nini usingeomba kutuama angalau siku mbili tatu ukajionea mambo nje ya Dubai kwenyewe?
Hoteli bei rahisi tu kuanzia Dirham 200 mpaka kuendelea. Ungeshuka tu hapo da Chemi ukawakata vilimilimi waosha vinywa.