Thursday, January 24, 2008

Nani Bosi?


Sijui nani kashinda hapo?

5 comments:

Anonymous said...

Wewe toto huyo buzi atakumiza!

KKMie said...

Sahamani dada'ngu. Hii habari imenisikitisha sana. Kilichonisikitisha sio kifo cha mtoto bali ufuatiliaji wa kesi nzima ili kupata ukweli.

Hivi Pilisi wetu hawafunzwi mbinu za kutumia midomo na maneno yao au deals kwa mujibu wa sheria ili kupata ukweli badala ya kupiga watuhumiwa?

Ni wazi kuwa huyu binti hakukusudia kuua mtoto bali alikuwa ajijaribu kumnyamazisha tu ili amalize kazi zake nyingi alizo achiwa.

Binti wa miaka 16 wa kibongo halingani kabisa na shughuli hizo, mtoto tu alimtosha na sio kila kitu ndani ya nyumba.

Wapigania haki za binaadamu na wanaharakati wa ajila kwa watoto wanafanya nini ndani ya Tz?

Watanzania tunahitaji kuzijua haki zetu ili tusinyanyaswe na Polisi.

Katika hali halisi Polisi wanapaswa kufunguliwa mashitaka ya unyanyasaji.....ni mtoto (16yrs) alafu mwanamke. Binti ameua bila kukusudia kw amajibu wa maelezo ya habari hii.

"Nilimsokomeza khanga mdomoni asinipigie kelele"

2008-01-25 08:34:43
Na Devota Kabuta


Msichana anayefanya kazi za ndani, Tabu Isaya (16) ambaye anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumnyonga hadi kumuua mtoto wa mwajiri wake, alifikishwa Mahakama ya Mwanzo Manzese/Sinza Dar es Salaam kwa ajili ya kuchukuliwa maelezo ya awali.

Msichana huyo ambaye alifikishwa mbele ya hakimu, Hilda Lyatuu wa mahakama hiyo katika maelezo yake alidai kuwa, aliamua kumweka mtoto huyo kipande cha khanga mdomoni kwa lengo la kumnyamazisha asiendelee kulia ili aweze kufanya kazi zake haraka.

Alidai kuwa, siku hiyo, Jumatatu Jan 21, saa 4:00 asubuhi, mama wa mtoto aliondoka nyumbani kwenda kazini na kumwachia vyombo vingi sana pamoja na kazi za kufagia uwanja na kufua nguo za mtoto na za kwake.

Alidai kabla hajaanza kazi hizo mtoto huyo alianza kulia na ndipo akaamua amwekee mdomoni kipande cha khanga kisha akamziba mkono mmoja mdomo na mwingine puani kama kwa dakika mbili hivi kwa lengo la kumnyamazisha.

Alidai alipomziba mtoto huyo alianza kutupatupa mikono na miguu kisha akanyamaza.

Alidai kuwa, alipoona amenyamaza alimtoa kipande kile cha khanga mdomoni, lakini alishangaa kumwona hapumui na ndipo alipogundua kuwa amekufa.

Alidai alichukua gauni lake na kuuviringisha mwili wa mtoto huyo kisha akachukua mfuko na kumweka ndani ya mfuko na kumbeba mgongoni.

Alidai alitoka na kwenda mpaka makaburi ya Manzese na alipofika alimtupa mtoto huyo sehemu yenye takataka jirani na makaburi hayo.

Alidai kuwa, alipomtupa aliondoka na kwenda kwa bibi wa mtoto huyo ambaye walikuwa wakiishi naye jirani na kumwambia kuwa mtoto ameibiwa na vijana wawili waliokuwa na mwanamke mmoja.

Alidai bibi huyo alimwambia amsubiri hapo nyumbani ili akamwite mama yake kazini.

Alidai mama yake alipofika huku akilia kwa hasira alimrukia na kuchanachana nguo alizokuwa amevaa na baadaye walimpeleka polisi.

Alidai huko polisi alisema anamtambua kijana mmoja ambaye alimtaja kwa jina la Rajabu wanayeishi naye jirani akidai pamoja na mwenzake ndiye aliyeshiriki kumwiba mtoto huyo.

Msichana huyo alidai polisi walimfuata Rajabu lakini licha ya kupigwa sana alikataa kuwa hakumwiba mpaka polisi wakaamua kumwachia.

Alidai polisi walimgeukia na kumpiga sana pamoja na kumbamiza ukutani na chini na ndipo alipoamua kuwaambia ukweli ili wasije wakamuua.

Alidai aliwaeleza kuwa mtoto huyo amemuua na kwenda kumtupa makaburini Manzese kutokana na hasira kwani alikuwa akilia na alikuwa na kazi nyingi, akaamua afanye hivyo amalize kazi kabla ya sasa nane ili mama yake atakaporudi asigombezwe.

Alidai aliwapeleka polisi na gari mpaka kwenye makaburi hayo na kuwaonyesha maiti ya mtoto huyo ambayo ilikuwa imebadilika na kuwa nyeusi.

Msichana huyo alidai kuwa, hakumuua mtoto huyo kwa kunyimwa mshahara kwani alikuwa akipewa mshahara wake kama kawaida isipokuwa aliamua kusema hivyo kwa kuwa walikuwa wakimhoji hoji sana.

Alidai mwajiri wake alimtorosha kutoka kwa wazazi wake mkoani Dodoma ili aje kufanya kazi kwake jijini Dar es Salaam kwa mshahara wa Sh. 20,000 kwa mwezi.

Alidai alimtorosha kwa kuwa baba yake alikuwa akitaka kumuoza kwa Mmasai wakati umri wake ulikuwa mdogo.

Alidai hapo nyumbani walikuwa wakiishi na mama huyo pamoja na mtoto aliyemuua lakini baba wa mtoto huyo alikuwa akija kulala mara moja moja.

Alidai mwajiri wake ana watoto wengine wawili ambao wanaishi Dodoma wilaya ya Kondoa.

Wakati huo huo, Joseph Mwendapole anaripoti kwamba Mama wa mtoto aliyeuawa kwa kunyongwa hadi kufa na msichana wa kazi za ndani, Asia Ali (28), amekiri kuwa hakuwahi kumlipa mshahara mfanyakazi wake tangu amchukue kutoka nyumbani kwao Dodoma.

Mtoto aliyeuawa ni Renaida Sebo aliyekuwa na umri wa miezi minane.

Akizungumza na Nipashe nyumbani kwake Manzese Penisula, Bi. Asia alisema alimchukua msichana huyo mwaka jana kutoka kwa mama yake mzazi lakini hakukuwa na makubaliano ya kumlipa mshahara.

``Mama yake aliniruhusu kuja naye Dar es Salaam lakini hatukuzungumza kuwa nitakuwa namlipa mshahara, sasa nashangaa kama anasema sikumlipa mshahara kwa kuwa hatukukubaliana hivyo,`` alisema.

Alisema tangu waanze kuishi pamoja wamekuwa wakiishi maisha ya furaha na mtuhumiwa huyo hakuwahi kuonyesha chuki kwake wala kwa mtoto.

Alieleza kuwa siku ya tukio hilo juzi yeye alikuwa katika biashara zake Ubungo na ndipo alipojulishwa na ndugu zake kuwa mtoto wake ameibiwa.

``Baada ya kufanya unyama wake akaja kusema kuwa kaibiwa mtoto na majirani na ndugu wakaenda hiyo sehemu aliyoporwa lakini baadae iligundulika kuwa ni uongo,`` alisema.

Anonymous said...

Hii ndo tatizo ya dume. Yaani si mnyama si binadamu mradi nyama ile inainginia kati kati ya miguu ni taabu.

Anonymous said...

Dinah, sasa hapo unaonesha wewe mtu waajabu sana, au sababu halijakufika wewe?! Huongei kama "analyst" au hata kibinaadamu tu, bali unaongea kufurahisha barza sio?! nanukuu "..Alidai kabla hajaanza kazi hizo mtoto huyo alianza kulia na ndipo akaamua amwekee mdomoni kipande cha khanga kisha akamziba mkono mmoja mdomo na mwingine puani kama kwa dakika mbili hivi kwa lengo la kumnyamazisha.." Loh ukatili waina gani huu, Dináh hapo hiyo haki sijui unaizungumzia ya kiumbe yupi mtoto wa miaka 16 anaejuwa zuri na baya (tena kwa watoto wa siku hizi at that age ni mkubwa mwenzio dada)au alidhulumiwa roho yake akiwa hata hata hajui jema wala baya, hajui mama kenda wapi wala baba yuwapi, hajui mbele wala nyuma, maskini kichanaga hichi kisicho na hatia kikaondoewa duniani kwa ujinga ukatili na unyama na ujinga wa huyu msichana. Ah anastahili msamaha gani huyu,Dina plz hem kuwa "sirias sometimes" Hivi kweli, mwari wa miaka 16 hajui kwamba ukimziba mtu pumzi anakufa? Haaa eti kauwa bila kukusudia! Yaani akusudie vipi tena?!! ikiwa mtoto kapiga piga miguu yeye bado kamminya tu mpaka alipoona kazi yake imefana, kama haitoshi anajuwa mpaka sehemu wanzowekwa wafu (makaburini)Dinah yaonesha hujazaa na pengine hata hujazaliwa (samahani)au pia hujui thamani ya roho! jee wewe uuliwe kwa upuuzi wa mwengine? Think critically" kabla hujabwabwaja, na jee unajuwa maadili ya kazi za kiaskri, kama hujui hiyo ni moja ya mbinu, incase umekataa kutoa ushirikiano kwa njia ya ustaarabu! Hiyo si tz tu ndio duniani kote hata kwa Bush (dada chemi atasaidia). Mwisho naomba kuchukuwa nafasi hii kumpa pole mfiwa (mama aliyenyongewa mtoto wake). Pia kwa wale wanaofanya kazi za ndani, msifanye kama huyu punguwani, kama hupati maslahi au kazi nyingi kupita uwezo wako plz plz heri kutoroka, nenda polisi kajieleze utarudishwa kwenu! Miaka 16 ni mama mtu mzima anabeba majibaba ya haja hasa, na "for sure" anajuwa zuri na baya!
Mungu ampe subra mama aliefiwa, kichanga daima kipeponi, na mungu ampe moyo wakutubia muuaji.

"Ni mtazamo tu usijenge bifu"

KKMie said...

Asante kwa maelezo yako ambayo yanaonyesha wazi hujanielewa na unamachungu na kifo cha mtoto.


Huitaji kuni-attack mimi bali kutoa melezo ili kujenga hoja yako ya kupinga maelezo yangu ili ieleweke.


Ktk hali halisi au niseme kibinaadamu, mtu akifa au akiuwawa huwa tunajenga chuki na hasira dhidi ya mtuhumiwa bila kujua ukweli wa mambo na nini kilipelekea hilo kutokea.


Nilichoegemea hapa na kilichonisikitisha ni "ufuatiliaji wa tukio" kabla ya kufungua kesi.


Sidhani kama KIPIGO kinafanyw ana Polisi wote Duniani labda US lakini mimi nimeishi Spain na UK na nina kuhakikishia ufuatiliaji wao wa tukio sio wa kupiga, wana mbinu nyingi tu za kumshawishi mtuhumiwa kukili kama kweli kakosa, na mtuhumiwa nalindwa dhidi ya watu wenye hasira, mtuhumiwa hapigwi hili likotokea au yeye akilalamika kuwa kapigwa na pilisi basi polisi anaachishwa kazi na kufunguli wa mashitaka.

Mtuhumiwa anahaki ya kutosema chochote kama hataki kufanya hivyo mpaka awe na wakili (kwa case ya huyo dogo Serikali ilipaswa kumpa).

Ikiwa Polisi wanauhakika na mtuhumiwa wanapaswa kumshawishi ili akili kosa na Mbinu kubwa hutumiwa kwa kuhusisha sheria kwamba kama Hukumu ni kifo basi ataambiwa akisema ukweli atafungwa maisha na kama hukumu ya kosa ni maisha basi ataambiwa akisema ukweli au kukili atafungwa miaka 20 na aki-save nusu anaweza kuachiwa n.k.


SIO KUMPIGA MTUHUMIWA......NI KINYUME NA HAKI ZA BINAADAMU NO MATTER what u've done!

Sio mtazamo ni hali hali halisi.