Wednesday, December 23, 2009

Ajali ya American Airlines JamaicaWadau, ndege ya American Airlines imepata ajali mara baada ya kutua huko Norman Manley International airport, Kingston, Jamaica. Kwa waliowahi kufika huko wanaelewa kuwa huo uwanja uko mwambao mwa bahari ya Caribbean. Habari zinasema kuwa ndege hiyo iliyokuwa na abiria 154 karibu iingie kwenye bahari! Ilisimama futi 10 (mita 3) kabla ya ufukwe! Ni miujiza hakuna aliyekufa ingawa watu 90 waliumia. Ajali hiyo ilitokea usiku wa kuamkia leo.
Habari zinasema kuwa ndege ilielekea kutua salama, abiria walikuwa wanapiga makofi, lakini wakati wa 'taxi' ndege haikusimama na badala yake ikaanza kuteleza, na kugonga vitu na zile oxygen masks zilishuka na zile overhead compartment za carryon baggage zilifunguka. Watu walikuwa wanapiga mayowe na kumwomba Mungu! Walisikia ndege inakatika vipande vipande.
Ndege hiyo aina ya 737, ilikuwa imetoka Washington, D.C.

1 comment:

Anonymous said...

acheni Mungu aitwe Mungu.