Friday, December 11, 2009

UKIMWI Bagamoyo


Pamoja na kuwa watu 880 wameptikana na virusi vya HIV ni bora wajuwe ili wapate dawa za VVU/ARV kurefusha maisha yao. Na hao 880 waliopatika na virusi ni kati ya 7,985 waliojitokeza. Je, ni asimilia gani katika wasiojitokeza? UKIMWI bado ni tishio tusizembee.

**********************************************
Kutoka ippmedia.com

Watu 880 Bagamoyo wakutwa na Virusi
Na Futuna Seleman
11th December 2009

Jumla ya watu 880 wamegundulika kuwa na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kati ya watu 7,985 waliojitokeza kupima virusi hivyo kuanzia Januari hadi Oktoba mwaka huu.

Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Bagamoyo, Erasto Mfugale, ametoa taarifa ya utekelezaji ya mapambano ya ugonjwa huo kwa mkoa wa Pwani hivi karibuni.

Akasema idadi hiyo ni sawa na asilimia 11 ambayo chanzo cha taarifa zake kinatoka kwenye Hospitali za Wilaya, Vituo vya Afya na pia taarifa za asasi.

Akasema kwa kipindi hicho, jumla ya watu 10,653, wanaume wakiwa 4,127 na wanawake 6,516, walishauriwa kupima kwa hiari na kati yao, watu 7,985 walipimwa VVU, huku miongoni mwao, watu 880 wakikutwa na maambukizi hayo.

5 comments:

Anonymous said...

DUH!

Anonymous said...

imenibidi nicheke, hii katuni kiboko yao. Jibaba sharti ute wamchuruzika..... antaka aone kilichofichwa

Anonymous said...

Watu wangefungwa makufuli sehemu za siri kweli magonjwa ya zinaa na UKIMWI ungepungua!

Simon Kitururu said...

Hivi ni kila mtu anataka kuwa na maisha marefu?

Anonymous said...

Huyo jibaba! Bora wamefungwa kufuli! Mimate inamtoka na msichana anadunda tu. Mambo si ndo hayo!