Thursday, January 14, 2010

Haiti Yaangamizwa na Tetemeko la Ardhi

Wadau, sijui ni mavoodoo ya Haiti, yaani kila nikitaka kuposti habari ya Haiti nashindwa. Mara posti inapotea, mara inashindwa kwenda!

Ni hivi, juzi huko Haiti kulitokea tetemeko la ardhi. Shauri ya ujenzi holela huko, nyumba nyingi zimeanguka. Wataalamu wanasema kuwa huenda watu 500,000 wamekufa. Maiti zimelundikana kaika mitaa. Hii janga haikuchagua tajiri wala maskini, wote wamekufa. Hata Askofu Mkuu wa Roman Katoliki alifariki ofisini kwake. Wazungu pia wamekufa. Mungu alaze roho zao mahala pema mbinguni. AMEN.

Ukitaka kutoa msaada dola $10 text Haiti to 90999. Pia FBI wametoa onyo kuwa katika mtandao tayari matapeli wameanza mchezo wao wa kuiba pesa za watu kwa kudai wana charities feki.

Kwa habari zaidi someni:

http://www.cnn.com/2010/WORLD/americas/01/14/haiti.earthquake/index.html?hpt=T1

id=9556519aitiEarthquake/haiti-earthquake-overwhelms-medical-aid-workers/story?id=9556519

Hata Ikulu ya Haiti Imebomoka!

9 comments:

Anonymous said...

Sitaki kuwasema vibaya lakini wametaka wenyewe. Hiyo Voodooo imeita hiyo ethikwaki!

Anonymous said...

Natoa pole sana kwa Haiti. Lakini wamekuwa na Uhuru zaid ya miaka 200. Nchi maskini kuliko zote Western hemisphere, watu wao wanaringa. kazi kufanya voodoo. Lakini nasema pole. Wajiulize sana, kama siyo adhabu kutoka kwa Mungu.

Anonymous said...

Si wakati wake,jamani ni kuwapa pole na kuwasupport km una uwezo

Anonymous said...

Yote hio ni mitihani ya mwenyezi mungu fuska na kufuru zimezidi duniani.

Anonymous said...

Kama ni ujenzi holela mbona mpaka Ikulu yao imebomoka? Nadhani hamna haja ya kuweka sababu yoyote ya maafa hayo ajali ni ajali tu. Wazungu pia wamekufa! kwani wazungu hawafi? Jamani tuwape pole watu wa Haiti tuache majungu mara vodoo mara nini...Hayo yote hayana maana katika kipindi hiki kigumu kwao.Ujumbe umefika.

Anonymous said...

Na Dar ikipigwa hali inaweza kuwa mbaya, hasa City Centre!

Mzee wa Changamoto said...

Nakubaliana na Anon January 15, 2010 7:21PM
Watu wanasema na kulaumu lakini kilichowakuta hao kikitokea Dar hatutakuwa na tofauti. Tutaumbuka tuu maana tunaudanganya ulimwengu kuwa tuna maendeleo lakini hatuna barabara, mifumo ya majitaka, majengo yaliyo katika viwango na vifaa vya uonkozi.
Nimeandika http://changamotoyetu.blogspot.com/2010/01/niangaliapo-haiti-naiona-tanzania.html

Anonymous said...

Nawashangaa sana mnaosema voodoo, hao watu wanaamini voodoo miaka mingi kama nyie mnavyoamini christianity. Usikashifu imani ya mwenzako maana wewe mwenyewe huna uhakika na imani yako. Imani zote tumezikuta na zilikuwepo tangu miaka zaidi ya 2000 na tutaziacha. Heshimu imani ya mwenzako maana hujui hata kama ya kwako ni ya kweli. Ukiwa na ubinadamu, utaakubali kuwa hili jambo la Haiti linatisha sana na kamwe hatuwezi kulielezea kwa maneno.

Anonymous said...

Jamani nchi za kiarabu mbona hazitoi misaada?au kwa kuwa nchi iliyokutwa na hili balaa c ya kiislamu,hata brazili dunia ya tatu wamepeleka misaada,warabu na miela yao haitoi misaada hata siku1,loh hawa watu hawana hata chembe ya upendo kwenye mioyo yao.