Tuesday, January 12, 2010

Kampeni ya Kitaifa ya Kuchangia Wahanga wa Mafuriko

Wazalendo Wanataaluma Wenzangu; Mtandao Wa Wanataaluma Tanzania (TPN) Kwa kushirikiana na Push Mobile na wadau wengine inaendesha kampeni ya kusaidia wahanga wa mafuriko yaliyoikumba Tanzania tangu wakati wa Siku Kuu ya Krismasi 2009 ambapo maelefu ya watu (hadi sasa zaidi ya 40,000), Familia zaidi ya 8,000 wameathirika kwa kukosa makazi, vyakula, na huduma za afya na kupoteza mali nyingi.

Hadi sasa idadi ya waliokufa inakadiriwa kuwa zaidi ya 14huku kukiwa na hofu ya mlipuko wa magonjwa yatokanayo na maji machafu kama Kipindupindu na Typhoid. Harambee hii inahusu kuwasaidia wananchi wenzetu ambao wako katika hali ngumu kutokana na athari za mvua kubwa na mafuriko. Mafuriko haya hadi hivi sasa yamegusa mikoa ya Morogoro, Dodoma, Shinyanga, Mwanza, Ruvuma, Arusha (Karatu); Rukwa; Tanga; Kilimanjaro n.k.. Na kwa vile mvua zinaendelea kunyesha kuna uwezekano wa maeneo mengi zaidi kuathirika. Uwezo wa Tanzania Red Cross kusaidia ni mdogo sana ukilinganisha na mahitaji.

TPN na wadau wake inaratibu harambee ya kuchangia wahanga wa mafuriko haya kwa kukusanya misaada ya vitu mbalimbali na pesa kwenda kwenye ofisi za Chama cha Msalaba na Mwezi Mwekundu cha Tanzania. Chama cha Msalaba Mwekundu ndio chombo ambacho kiko mstari wa mbele kuongoza juhudi za kusaidia walioathirika ikishirikiana na taasisi mbalimbali binafsi na vyombo vya serikali.

TPN inatoa wito kwa Wanachama wake, wapenzi na Watanzania kwa ujumla kuchangia kupitia makato ya kila siku ya muda wa maongezi wa simu za mkononi (Zantel; Tigo; Zain na Vodacom): “Changia Shs 150 kwa siku kwa waathirika wa mafuriko. Tuma SMS yenye neno TPN kwenda 15522. Utakatwa Shs 250 kujisajili. Kwa maelezo zaidi wasiliana na 0715 740 047”

Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Maafa cha Chama cha Msalaba Mwekundu Bw. Joseph Kimaryo ambaye TPN na wadau wake ilifanya naye mkutano mahitaji makubwa hivi sasa ni pamoja na Magodoro, Mahema, Vyandarua, Vyakula (visivyoharibika), Maji safi (masanduku ya chupa za maji), Madawa ya kuzuia maambukizi (ambayo hayajaharibika au kufunguliwa), Vifaa kwa ajili ya matumizi ya kina mama na watoto, Makaratasi ya kujipangusia (clean wipes), Fedha kwa ajili ya mahitaji Muhimu na kugharimia usafirishaji na ufikishaji misaaa kwa walengwa, n.k.

Misaada itakapokelewa katika makao makuu ya Msalaba Mwekundu Jijini Dar-es-Salaam Masaki; Mrokao Street/Coral Lane (Karibu na Kora Beach Hotel, barabara ya kwenda Chole) na katika matawi ya Red Cross mikoani pote. Hakuna msaada mdogo au usio na maana na Chama kitapokea misaada ya aina zote. Misaada ya fedha na vitu yaweza kupokelewa kwenye ofisi YOYOTE ya Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania. Au ofisi za Tanzania Professionals Network. Kwa wale watakopenda kutoa michango yao kupitia TPN. Misaada itolewe kwa njia zifuatazo:

1. Crossed Cheque written to: Tanzania Professionals Network

2. Bank Deposits or Transfers to: Account Name: Tanzania Professionals Network, Bank Name: CRDB Bank, Bank Branch: Lumumba Branch, City: Dar Es Salaam, Country: Tanzania, Swift Code: CORUTZ TZ, US $ A/C No: 02J1 007 608 900; TZS A/C No: 01J1 007 608 901

3. M-Pesa (Vodacom): 0768 777 888

4. Z-Pesa (Zantel): 0773 88 18 88

5. Zap (Zain) 0784 00 88 99

6. Western Union — Tuma kwa: Mr. Emmanuel Mmari; TPN Finance and Administrative Manager; Dar Es Salaam. Tuma nakala ya MTCN kwa president@tpn.co.tz

7. Fedha Taslimu: Ofisi za TPN — Barabara ya Nyerere; Jengo la TOHS (Dar Group); Ghorofa ya 1, karibu na Radio Tanzania.

8. Kuchangia kupitia makato ya kila siku ya muda wa maongezi: “Changia Shs 150 kwa siku kwa waathirika wa mafuriko. Tuma SMS yenye neno TPN kwenda 15522. Utakatwa Shs 250 kujisajili. Kwa maelezo zaidi wasiliana na 0715 740 047”

9. Kuchangia vitu mbalimbali: Leta ofisi za TPN — Barabara ya Nyerere; Jengo la TOHS (Dar Group); ghorofa ya 1 karibu na Radio Tanzania au piga simu namba: 0715 740 047 ili ofisa wa TPN avifuate (utalipia usafiri)

10. Kwa kutumia kadi za Kibenki kwa walio USA na sehemu nyingine ambazo kadi hizi hutumika (Visa, MasterCard, Discovery na America Express) kupitia mtandao wa www.mwanakijiji.com , upande wa kulia chini kuna mahali pana nembo yenye maneno “donate”.

Kwa kuanzia TPN imechangia TZS Million 1.0. na tunawaomba wote kila moja kwa nafasi yake kuchangia.

Pamoja Tunaweza! Amua sasa kuwasaidia Wahanga Wa Mafuriko. Kwa maelezo zaidi, tuandikie: president@tpn.co.tz

Tafadhali tuma ujumbe huu kwa wengine wengi.

Imetolewa na:

Sanctus Mtsimbe;

Rais; Mtandao Wa Wanataaluma Tanzania

Tel: 255 754 833 985

No comments: