Sunday, September 12, 2010

Vibaka Ubungo Dar es Salaam

Kuna Mdau H. S. ameleta taarifa hii:

Leo nimeibiwa pale ubungo mataa, gari langu limengolewa side mirror katika hali ya ajabu na wepesi hata nilipojaribu kujihami lau kwa kumpiga kibaka mmoja na Lungu niliyokuwa nayo bado sikumpata uzuri ameenda na side Mirror zangu!!!

Imeniuma sana lakini napanga kufanya operation kwenye hilo eneo lau nipate kibaka mmoja wa kutolea mfano...hili ni eneo ambalo kwa makusudi linageuka taratibu kuwa jehenamu kwa kila kitu ulichonacho, anzia sim,begi, saa, laptop, pochi na hata heleni za akina mama.

AJABU unapoibiwakama hivo walikua wa 4 na magari yalikua yapo sikupata msaada hata kwa mtu mmoja nilihangaika peke yangu huku watanzania wenzangu wanaangalia hilo LIMENISHANGAZA SANA,,,

Nchi hii sasa ina poteza usalama kiasi kile na kwa kweli watu wa mji huu wa Dar sijui ni uoga ama vipi!!! naamininingekua sehem nyingine kama mbeya wale vibaka wangekiona leo....natoa wito kwa wote kuweni makini na Ubungo mataa,keko,Fire,jangwani,buguruni haya maeneo yanatakiwa kusafishwa!

1 comment:

Anonymous said...

Yaani enzi za kupiga wezi zimeisha! Hao wanatakiwa kupigwa karibu kufa! Nikiwaona mi naua! Sorry!