Tuesday, September 14, 2010

Wazee Wauwawa Kenya eti Wachawi!

Jamani, utalia ukitazama jinsi hao wazee wanawake wanne na mwanaume moja walivyouwawa kwa kuchomwa moto na wananchi wenye hasira. Yaani watu wanashangilia kabisa! Mtu akitoka kwenye moto wanamrudisha kwenye moto! Hata mtu anapiga video! Hao waliotenda wachukuliwe hatua kali na serikali ya Kenya!

Mnaweza kuona video kwa kubofya HAPA:

http://www.wisdia.com/articles/shocking_video_five_suspected_witches_burnt_to_death_in_kenya.aspx

Lakini Tanzania kuna tabia mabya ya kuua wazee hasa huko Shinyanga! Wakiwa na macho mekundu shauri yua kupika kuni, eti mchawi, unaua! Jamani! Hebu waafrika acheni kuwa na imani potofu!

5 comments:

Anonymous said...

Da Chemi usishangae sana Maafrika ndivyo yalivyo.(Yote hii inatokana na UBINAFSI wa WACHACHE-20% kupora mali za UMMA kwa manufaa yao na faimilia zao na kuwasahau walio WENGI-80% matokeo yake watu kukata TAMAA kwa kila jambo)

Anonymous said...

Mimi ni mzaliwa wa shinyanga , huwa inaniuma sana hii kauli ya kusema ati mtu akiwa na macho mekundu hasa wazee ni mchawi na anauawa!!, sielewi ni nani alifanya research potofu kama hii
jamani ajitokeze mtu akafanye utafiti sio kauli ya mlevi mmoja alishawahi tamka hivyo ndo likawa jibu si kweli hata kidogo ni uzushi mauji ya vikongwe siri yake ni kubwa na si uzushi kama huo. mimi nafahamu vizuri sana ila kwakuwa nchi hii in ya kipungufu haina viongozi makini ndo maana mtu anazusha jambo linakuwa msamiati miaka nenda rudi
Inasikitisha sana sana . inatia hasira na nyie waandishi mnajiita kafanyeni tafiti sio kuibuka tu na habari

Anonymous said...

Watu wakatili! Wanaua hivi hivi? Polisi Kenya wamechukua hatua gani? Ushahidi ni huo! Wauaji wakamatwe mara moja! Nimeumia sana!

Anonymous said...

Wewe Anonymous 2:44AM hebu acha zako! Shinyanga ndo penyewe kwa kuua wazee! Eti wachawi. Usizeeke Shinyanga utauawa! Umesahau ilibidi rais Kikwete aende huko kuwabembeleza watu wasiwaue! Kweli mna imani potofu!

Anonymous said...

Hard to believe that this kind of stuff still goes on, this day and age! When are people going to wake up?