Tuesday, September 07, 2010

Dr. Slaa Afunguliwa Mashitaka Mahakama Kuu!

(Pichani Dr. Wilbrod Slaa - CHADEMA)

Jamani, sasa badala ya kuwa kampeni ya siasa, ugombea rais wa Dr. Wilbrod Slaa wa chama cha CHADEMA, unageuka kuwa Soap Opera (Tamthiliya)! Majuzi huko Babati walimwuliza Dr. Slaa ana wake wangapi(BOFYA HAPA kupata maelezo zaidi), leo eti mume halali wa mke wa Dr. Slaa, kaenda mahakamani na kusema kuwa Dk. Slaa kamwibia mke wake! Kusoma habari zaidi za kesi BOFYA HAPA.
Huo mchezo wa kukuchunguza mpaka umevaa chupi gani kama ni mwanasiasa ni mchezo mkuu hapa Marekani. Ukiwa mwanasiasa lazima uwe msafi. Kwa maana hiyo usitembee nje ya ndoa, usiwe na kimada, usizae nje, usifanye ngono na malaya... listi ni ndefu. Bado wanafanya na wakigundulika wengi wanalazimishwa kujiuzulu.

Enzi za Mwalimu ulikuwa husikii kwenye vyombo vya habari kiongozi fulani anatembea na fulani! Sasa ni jambo la kawaida, sijui ndo uhuru wa vyombo vya habari au nchi kukua kisiasa. Wangekuwa wanasema mambo ya watu enzi za Mwalimu mbona yangesemwa mengi. Ungesikia fulani kazaa katika kila mkoa wa Tanzania, fulani ana familia nyingine sehemu fulani, binti fulani katoa mimba ya kiongozi fulani n.k. Sidhani kama kuna kiongozi 'msafi', hata kwa upande wa wanawake! Kiongozi fulani kazaa sehemu fulani, kiongozi huo kapata ugonjwa fulani mahala fulani.....Doh! Tunaelekea wapi?

Mwisho nauliza kwa nini wanamsakama Dk. Slaa sasa? Naona kampeni yake imepamba moto kweli halafu ndo jamaa anataka alipe eti mabilioni!

12 comments:

Anonymous said...

Slaa anaandamwa kwa sababu kadiriki kumfungulia mashitaka Kikwete na kuendelea kukisakama CCM kama chama kilichooza kimaadili, na kwa kuifanya hivo kujichora yeye binafsi kama Champion wa ukamilifu uadilifu. Yawezekana kabisa hili kuwa jibu la CCM kwa mapigo ambayo wameyapokea toka kwa Slaa tangu aanze Campain. Kama ulivosema Chemi, mwana siasa hawezi kamwe kuwa na strictly private life, hasa kwa ngazi kama hiyo ya urais. Kama hayo madai ni ya kweli, basi Slaa kapoteza moral credibility ya kuweza kuongoza nchi. Ataongozaje raia anaowanyang'anya wake zao na kuchangia kusambaratisha famili zenye watoto wachanga kama hao wa huyo Josephine, pasi na kujali athari za divorce kwa hao viumbe innocent kama huyo Precious na dadake.Huwezi kudai na kunadi kwamba un upendo na uchungu wa kwa taifa lako hukukatika faragha unafanya vitendo vinavyo bomoa msingi na nguzo ya taifa lilo hilo, yaani familia. No coherence! Isitoshe, kama padri anapaswa kujua barabara yasemavyo maandiko matakatifu kuhusu swala la talaka na ndoa ya pili.Biblia inaweka bayana kwamba mtu akimwacha mkewe kwa sababu ziwazo zote kando ya uzinzi,hanaruhusa ya kuoa au kuolewa tena mpaka huyo ex-wake aage dunia. Ninavoelewa ni kwamba ex-wa Slaa na ex-wa Josephine wate wa hai bado, jambo ambalo linawafanya, S & J, kuwa WAZINZI, kulingana na Romans chapter 7.Sasa tafauti gani iliyopo kati ya Slaa na list of shame yake aloipigia sana kelele kiasi cha kututeka sote mioyo? Si wote wametumia influence yao kubomoa - wengine uchumi na yeye familia. HATA KAMA MUME HALALI WA JOSEPHINE HAKUWA RESPONSIBLE KAMA WANAVODAI BAADHI, still Bw. Slaa hajawa matrimonial mesiah kufariji wanawake walio na matatizo katika ndoa zao. Kwa sababu kama Future possible President akianza hivo, future ministers wataishia wapi!

Anonymous said...

Mfa maji haishi kutapa

Anonymous said...

Naona kama umeamua kuwa Dr Slaa kashtakiwa kwa kuwa anagombea urais na kampeni zimepamba moto, una uhakika gani kuwa mwenye mke asingeshtaki kama hakuna campaign?Au amekosea kudai haki yake?Au alitakiwa kudai haki yake wakati gani?

Anonymous said...

Dr. Slaa alikuwa padri wa RC. Kashindwa. Kazi kuiba wake za watu. Atawez akuongoza nchi kweliw akati anashindwa hata kumudu sheria za RC? Ni kweli yeye ni selebriti hivyo maisha yake ni sawa kuanika hadhrani. Watu wanataka kujua wanaongozwa na nani. siyo enzi za Mwalimu mambo ya giza!

Anonymous said...

Njama za CCM hizo kuangusha kampeni ya SLAA. CHADEMA Watashinda sfari hii. Sisi si wadanganyika kama enzi za Nyerere!

Ms. Msemakweli said...

Josephine Mushumbusi, amezungumza kupitia Mwanasheria Mkuu wa Chadema,ambaye pia ni wakili wa Dk Willibrod Slaa, Tundu Lissu, akaviambia vyombo vya habari kuhusu tuhuma zinazowakabili yeye na Dk. Slaa kuwa kwa mara nyingine, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimerejesha mfumo wa uchaguzi
unaobadilishwa kuwa mfumo ya kijinga. Akasema kwamba CCM wamekuwa akikishambulia Chadema kuwa ni chama Wachagga; kwamba baadhi ya viongozi wake ndio walimuua Chacha Wangwe; na kwamba Dk Slaa ametumwa na kanisa Katoliki kugombea urais; lakini baada ya kuona hadithi hizo zimepuuzwa, sasa wameibuka na suala jipya na “ndoa za Dk. Slaa” wakidhani zitawasaidia kugeuza macho ya umma kutoka kwenye masuala muhimu ya wakati huu.

Akasema CCM hawataki Dk. Slaa na Chadema wajadili wizi, ubadhirifu wa fedha na mali za umma; hawataki wajadili wizi wa Sh. bilioni 772 zilizoibwa katika mwaka 2008/9 tu, kwa mujibu wa ripoti ya Mkaguzi na mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali; hawataki Chadema itaje majina ya wezi wa Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT); hataki Chadema wajadili jinsi JK na rafiki zake, akina Edward Lowasaa, Nazir Karamagi, Andrew Chenge na Rostam Azizi walivyofilisi taifa hili; hawataki Chadema ijadili madai halali ya wafanyakazi wa Tanzania na ahadi za ‘maisha bora kwa kila Mtanzania.’ CCM hawataki Chadema kijadili sera mbadala ambazo zinalenga kuwakomboa Watanzania kutoka Lindi la umaskini.

Wanataka kulielekeza taifa zima katika kujadili masuala ya ‘chumbani’ kwa Dk. Slaa; analala na nani, ana wake wangapi, kawapata wapi na kadhalika;

Tundu Lissu amesisitiza kuwa kila wanapoona wamebanwa, CCM huwa wanabuni njama za kukomoa washindani wao, kama walivyofanya huko nyuma. Alitoa mifano ya kilichotokea miaka ya 1995 na 2005.

Mwaka 1995: Kwa kumwogopa Mrema aliyekuwa tishio kwa CCM, walimtumia mwanamke mmoja, aitwaye Angelina, wakidai ni kimada aliyezaa na Mrema; akawa
analala getini kwa Mrema, Masaki, Dar es Salaam. Wakamdhalilisha. Baada ya uchaguzi, Mrema akashindwa, na suala la Angelina halikujadiliwa tena.

Mwaka 2005 tishio la CCM ilikuwa Chama cha Wananchi (CUF), hasa Zanzibar. CCM wakamtumia Inspekta Jenerali wa Polisi, Omar Mahita, siku chache kabla ya uchaguzi, kudai kuwa amekamata lori lenye mapanga, majambia, visu na silaha nyingine zenye nembo ya CUF. Wakakipaka chama matope. Baada ya uchaguzi, hatukuelezwa lolote kuhusu visu hivyo.

Mwaka 2010: Tishio la CCM ni Chadema na Dk. Slaa. Baada ya kuona upepo unawaendea vibaya, CCM wameamua kufanya siasa za mtaro wa maji taka; hizi wanazotumia watu kumwandama Dk Slaa.

Tundu Lissu alisema kuwa Chadema hawako tayari kufanya siasa za majitaka; na kwamba Watanzania hawako katika kujadili mambo hayo, kama hali ya afya za wagombea, ambao baadhi wanadaiwa kuwa na virusi vya ukimwi kiasi cha kubadili damu kila baada ya miezi, na kwamba kwa sababu ya unyonge huo,baadhi yao waanguka mara kadhaa jukwaani.

Akasema wao hawatazungumzia baadhi ya wagombea urais wana wake wangapi,mahawara wangapi, na wamewaweka katika ofisi gani za umma, wapi wamepewa mikataba minono ya fedha kwa upendeleo, na kadhalika. Akasisitiza kwamba
Chadema haitajibu uchafu unaosambazwa na vyombo vya habari, lakini akasema, “sauti yetu itasikika iwapo wataenda mahakamani.”

Akasema Chadema itazungumzia umaskini wa Watanzania na namna ya kuupunguza au kuuondoa; jinsi Tanzania ilivyo nchi ya tatu katika Afrika lakini wanakijiji wanalazimishwa kujenga shule za kata huku serikali ikifuja
mabilioni ya pesa (kama hizo bilioni 772/- zilizotafunwa ndani ya mwaka mmoja.

Akasema Chadema itajadili jinsi ya kuboresha afya za wananchi.
Akasema, “hatutaki siasa za chumbani, bali za hadharani.”

Amekuwa sauti kuu ya wananchi Bungeni, inayotetea masilahi ya umma Kuliko kiongozi yeyote aliyewahi kuwapo Tanzania ndani ya miaka 50, ni Dk Slaa pekee aliyetaja hadharani mafisadi 11 bla woga wowote.

Walioathirika kwa ujasiri wake ndio hao wanaomsakama sasa kwa mambo ya chumbani badala ya mambo ya hadharani.

Anonymous said...

Katika masuala ya chumbani JK mwenyewe si msafi kabisaaa tena bora Slaa kamtangaza wa kwake hadharani ndio anaonyesha uwazi na ukweli. Tena si JK tu wengi sana na kungekuwa na ile sheria inayosema ambaye ni msafi na ampige mawe Slaa ungeona kama kuna hata mmoja ambaye angejitokeza. Fanyeni kampeni hayo mambo ya kumshtaki mtu na vimada Afrika hayalipi ingekuwa Ulaya na Marekani labda.

Anonymous said...

Dr. Slaa naye fisadi! Ikiwa kweli huyo mashumbusi alikuwa hajapewa talaka, kisheria, basi, Dr. Slaa ni fisadi. Ni sawa na kuhodhi bidhaa zilizoibiwa!

Anonymous said...

Huyo bodyguard nyuma ya Slaa anaeleka hana mchezo!

Anonymous said...

Huko ndiko kudhalilisha utu wa mwanamke; utasemaje unamshitaki mwanamue aliyechukua huyo mwanamke ilihali mwanamke mwenyewe alikuwa na haki ya kukataa? Kufanya hivyo ni kumfanya mwanamke kama vile ni mali inayoweza kuibiwa bila hiari yake kama vile baiskeli au gari.

Anonymous said...

Ishu hapa si kuwa yeye Dr. Slaa alikuwa anajifanya msafi na mtakatifu kumbe??? Anakula huku anapuliza, siwezi kumuamini mtu anayechukua mke wa mwenzie inawezekana hajui uchungu wa mke maana nasikia hata huyo Rose Kamili waliishi tu kama bibi na bwana hakufunga naye ndoa!

Kweli JIDE ni mkali maana aliimba wimbo wake ule nasonga mbele sijui kisha akasema HAKUNA ALIYE MSAFI maana image aliyokuwa anaipotray sio image yake je na yeye kuhusu watoto wake alozaa na huyo Rose Kamili? Jamani mbona kizungumkuti?

Anonymous said...

Nyie watoa maoni wawili wa mwisho ni vipofu! Tanzania itabakia kuwa masikini kwasababu ya upofu wenu! Badilikeni, acheni tabia ya jazba, umbea, ushabiki, porojo, majungu na kuongelea mambo msiyoyafahamu.