Friday, July 06, 2012

Chuo Kipya cha Zanzibar School of Health


Chuo cha Zanzibar School of Health kinamilikiwa na Zanzibar School of Health Company Limited.

Tuna wingi wa Shukrani kwa vile Chuo cha Zanzibar School of Health kinatowa mafunzo ya Afya kutokana na ruhusa kutoka Wizara ya Afya Zanzibar.Wanafunzi wanaosoma hapo ni 45 kwa Fani ya Psychology na 88 kwa Fani ya Uuguzi.

Chuo kimeajiri Walimu wenye Sifa kusomesha Fani husika na pia kimeajiri Wafanyakazi wa ngazi mbali mbali ili kuleta ufanisi wa Chuo. Tunayo azma ya kuanzisha na kuendeleza mtandao wa Elimu ya Masafa
ikiwemo ushauri wa Afya wa Masafa yaani Tele Medicine kupitia mitandao ya kimataifa na ya kitaifa. Chuo kinafanya taratibu ya kuwawezesha wanafunzi kupata mazoezi ya vitendo nje na ndani ya Zanzibar. Kuna
azma pia ya kuanzisha Continuing Medical Education kupitia mtandao,semina ,na kongamano za kiwengo cha kimataifa.

Chuo kimepeleka Ombi Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (Nacte), na kupata Form maalum kwa ajili ya usajili kwa ngazi ya NACTE baada ya kupata Usajili Rasmi kwa Ngazi ya Baraza la Wauguzi la Zanzibar kwa Fani ya Uuguzi na baada ya kupata barua ya kutokuwa na pingamizi kutoka Wizara ya Afya za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuundesha Masomo ya Psychologia Nasaha yaani Counseling Psychology ya Tumaini University College Iringa. Chuo kimejisali na Taasisi ya kodi TRA ,ZRB Taassisi ya Usajili wa Kampuni ya Zanzibar na kupata Zanzibar Government Certificate of Incorporation.

Chuo kimepitisha Mtaala wake wa Diploma ya Nursing chini ya ukaguzi na masahihisho ya Zanzibar Council of Nurse Midwives na kupata School Registration Certificate number PNS/01 ya tarehe 29.09.2011 .

Chuo kitashukuru ikiwa Wawakilishi wetu watapata Nafasi kutembelea Chuo hich ili waweze kutupatia Ushauri wao wa Busara.

Baada ya kukamilisha hesabu za Budget ,Chuo kimewaslisha Form za Maombi kwa Usajili wa NACTE. Pia Chuo kina azma ya kuanzisha Fani zifuatatazo:

1. Diploma in Speech and Language Therapy

2. Diploma in Clinical Pharmacy

3. Diploma in Physiotherapy

4. Diploma in Clinical Medicine

5. Diploma in Medical Laboratory Technology

6. Doctor of Medicine Degree

Chuo kimeunda Board ya Taaluma na kimewaalika wajumbe kutoka Wizara ya Afya kueomo kwenye Board hio. Chuo kinachangia maendeleo ya Taifa kwa kutowa ajira kwa wataalam 10 wa Tanzania kufanya kazi Chuoni hapo . Aidha Chuo kimewasilisha Maombi Wizara ya Ardhi kwa kupatiwa Eneo la Kujenga Teaching Hospital yenye Vitanda 200 ,Maabara ya kisasa, na Taasisi ya Elimu ya Afya ambazo itakuwa na kiwango cha Kimataifa.

Vile vile Cho kimewasiliana na na Baraza la Mitihani yaani NECTA kwa madhumuni ya kuanzisha Shule ya Sekondari maalum na kituo cha kufanya Mitihani ya Kitaifa na Kimataifa.Sasa Chuo kinaandikisha Wanafunzi hao ili waweze kufanya Mitihani ya Kimataifa .

Uongozi wa Chuo unashukuru Wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kwa kuwaunga mkono kwa kuleta vijana wao kusoma Chuoni hapo na unaahidi Umma wa Nchi hii Elimu bora yenye Ufanisi wa Hali ya Juu.

Chuo kingependa pia kuendelea kupata Ushirikiano ili kiweze kutimiza ahadi zake za kuendeleza Nchi yetu na kutumikia Umma.

Ahsante

AMUR

No comments: