Tuesday, July 24, 2012

Ugeni wa Malaika


Nimepata kwa Email:

Malaika wawili watembeaji walisimama usiku mmoja katika nyumba ya Familia ya Kitajiri. Familia ile ilikuwa JEURI na walikataa kuwaruhusu wale malaika kulala kwenye chumba chao cha wageni.

Badala yake wale Malaika walipewa kasehemu kadogo kauchochoroni chenye baridi chini ya Nyumba ya wale Matajiri.  Wakati wanajiandaa kutandika kwenye sakafu ngumu kujiandaa kulala,Malaika Mkubwa aliona kuna tundu ukutani wa sehemu ile na akaliziba.

Malaika mdogo akauliza kwa nini umeliziba tundu hilo wakati familia hiyo ni ya watu jeuri? Malaika mkubwa akajibu:

"Mambo siku zote hayawi kama tunavyo dhania"

Usiku ya Pili wale Malaika walikwenda kupumzika kwenye Nyumba ya Mtu masikini sana,lakini ni Mkulima mwenye huruma sana yeye na Mkewe.

Baada ya kushirikiana chakula kidogo walichonacho,wale masikini waliwakaribisha chumbani kwao wale Malaika ili wapate kupumzika vizuri usiku ule.

Wakati Jua lilipochomoza asubuhi ya pili yake,wale Malaika walimuona yule Mkulima masikini na Mkewe wanatokwa machozi. Walipowauliza kulikoni? Wakajibu:

“Ng’ombe wetu mmoja tu tulienae ambae maziwa yake ndio kipato pekee tunachokitegemea tumemkuta amekufa Shambani.”

Yule Malaika mdogo alikasirika na akamuuliza Malaika mkubwa:

“inakuwaje umeacha jambo hili litokee” ?

Yule jamaa wa kwanza tulielala kwake alikuwa na kila kitu,hata

hivyo ulimsaidia kuziba tundu kwenye nyumba yake,alilaumu

Malaika mdogo.

Huyu jamaa wa Pili alikuwa anakitu kidogo sana lakini alikubali kushirikiana na sisi kila kitu lakini umemuachia Ng’ombe wake afe,inakuwaje ?

Malaika Mkubwa akajibu:

"Mambo siku zote hayawi kama tunavyo dhania”.

"Tulipokaa chini kwenye Nyumba ya yule Tajiri,niliona kupitia kwenye lile tundu kuna DHAHABU nyingi sana chini ya Jumba lile”.

Lakini kwa kuwa yule Tajiri alikuwa Jeuri na Kiburi sana na alikuwa hataki kushirikiana na wenzake na kutoa missada,NILILIZIBA LILE

TUNDU ili asije kuiona ile Dhahabu."

"Usiku uliopita tulilala kwenye Nyumba ya Masikini tena kwenye Kitanda chake.Usiku ule Malaika wa MAUTI alikuja kutaka kuchukua ROHO ya Mke wa yule Masikini.Nikaamua kutoa msaada kwa kumtoa yule Ng’ombe badala ya Mke wa masikini”.

“Mambo siku zote hayawi kama tunavyo dhania.”

Wakati mwingine haya ndio mambo haswa yanvyotokea kinyume na vile tulivyo tarajia.Kama UNAIMANI YA MUNGU basi unahitajiwa kuamini kuwa matokeo yoyote yale ni faida kwako.Huwezi kujua hayo mpaka hapo baadae....

Kuna Watu wanakuja katika maisha yetu baadae huondoka

Kuna Watu wanakuwa  marafiki zetu kwa muda tu baadae hutoweka huku wakiacha makovu kwenye nyoyo zetu  na wote hatupo  sawasawa katika  kufaulu kupata marafiki wazuri !!!


Ya Jana ni Historia.
Ya Kesho ni Miujiza.
Ya Leo ni Zawadi kutoka kwa Mungu.
Tunapaswa kushukuru kwa zawadi hii pekee.

HUYU NI MALAIKA AMEKUTEMBELEA,TUMA UJUMBE HUU KWA WATU 5 NA UOMBE MUNGU AKUSAIDIE KATIKA SHIDA ZAKO

Usifute Message hii kwa sababu inatoka kwa Malaika maalum kwa ajili yako.

HUWEZI JUA HIVI SASA: -

-kuna mtu anakufikiria wewe,
-kuna mtu anakujali wewe,
-kuna mtu anakukosa wewe,
-kuna mtu anahitaji kuongea na wewe,
-kuna mtu anataka kuwa na wewe,
-kuna mtu anatarajia haupo kwenye matatizo,
-kuna mtu anataka kuushika mkono wako,
-kuna mtu anakuombea mambo yako yote yawe mazuri,
-kuna mtu anataka uwe kwenye furaha wakati wote,
-kuna mtu anahitaji umtafute,
-kuna mtu anashangilia mafanikio yako,
-kuna mtu anataka kukupa zawadi,
-kuna mtu anakufikiria wewe ni zawadi kwake kutoka kwa MOLA,

-KUNA MTU ANAKUPENDA,
-kuna mtu anavutiwa na haiba na Nguvu zako,
-kuna mtu anafikiria TABASAMU lako,
-kuna mtu anatamani muwe bega kwa bega katika kila kitu.

No comments: