Saturday, April 06, 2013

Vurugu Tunduma Baada ya DC Kukataza Kuchinja - Maoni

 Received via Email:

 Na Mdau Hildegarde Kiwasila

Watu Tanzania hula vibudu anyway wawe wakristu au waislamu. Tunaonaga kwenye TV na magazeti kuwa baadhi ya kuku wa kizungu au hata wa kienyeji hufa wanapokuwa wanasafirishwa nao huchinjwa na kuchanganywa na wale wazima. hata baadhi ya mifugo hufa haitupwi bali utumbo uliooza ndio hutupwa. Mizoga hiyo huuzwa kwa bei rahisi na ikaingia mahotelini tukajilamba kuku wa kukaanga, mbuzi etc na supu ya ndizi asubuhi. Wakati mwingine unaona nyama imebunda inanuka au kuku yupo pink babisa na harufu mpaka unamwita mtoa huduma na kumrudisha unaona hapana pink colour na harufu imezidi. Haya-hapa panan udini kweli?

Hawa watoa huduma wa kupika kwenye sherehe, mahoteli unafikiri vyote wapikavyo ni vipya halali hakuna haramu? kama ni vipya-haijatokea ukala ukaharisha? Hebu fika Shoprite na supermarket nyingine ukae nje unapunga upepo na kuangalia magari na mizifi Canter na Pickups. utaona ya Hoteli yamekuja kuchukua chakula kilicho expire kinakwenda kupikwa vyakula vya kisasa mahotelini. Kisa wanunue ghali wasipate profit. havitupwi hivyo vya supermarket si bongoland hata Ulaya. Na sote wakristu na waislamu tukiwa ulaya ughaibuni husubiri mpaka vime-expire muda wake vimeshuka bei sana badala ya $10 kuku kawa $ 1 au 0.50 ndio twanunua kwa wingi na anakaa miezi kadhaa january hadi June katika fridge lako chumbani na unamuangalia kuku daily kwa tabasamu la kuupiga chenga ukata na umasikini wa kukufanya utembelee wenzako kudowea kula. Unamla huyo hujui kachinjwaje na ame expire unamuongezea muda wa kuexpire.

Ukikuta kuku, nyama zilizopita muda wake, matunda etc wametupa nje ndani ya dustbin la supermarket mnawahi wazungu na waafrika kuzoa kabla mbwa hazijaja kupindua na kuziharibu. Ombaomba wa mitaani ndio wanazoa makuku na nyama hizo kichizi. Hata hapa TZ ukienda maeneo ya kutupa taka-utakuta wachakura takataka wanaokota nyamba zilizotupwa kule kutoka mazizi ya watu au machinjioni zinaokotwa na kuingia vilabuni zinapikwa subu. Nyanya zinaokotwa nan kuingia magengeni.

Ulaya-Wanyama wanachinja kwa kisu cha umeme kumpa shock mnyama kwanza akazirai kisha kumchinja. Twala wakristu na waislamu huko vyauzwa supermarket na tupo hai hadi leo. Na wengi wakimbiao vita vya Boko-haram na vita vinginevyo nchi za kiislamu (Afghanistan, Iraq, Egypt etc) na nyinginezo zisizo vita wahamiaji hukimbilia zaidi huko Ulaya na USA kwenye mataifa ambayo ni ya Katiba za dini za kikristu-mbona hawaogopi kwenda huko kwenye nguruwe na madhehebu hayo ya kukaba wanyama?

Binadamu wote mahitaji yao mamoja-Uhuru, Upendo, Amani; kula kushiba, Starehe na haja. Usishangae kuona kuwa mmewa utoao unga wa kulevya (cocaine) unapandwa na kutumika na kuuzwa au kupatikana kwa waswalihina sana na wanalinda mashamba yake kwa mtutu na huku wanasali kwa Mungu wao kila muda unapofika; wanakosali sana au kusema hivyo kuna maovu kibao ambayo yatakupa maswali mengi-ubakaji, mauaji ya watu kwa kujilipua; killing for family honour; mtu wa dini kubaka na kulawiti vichanga au watoto; kunywa pombe kwa kificho; kubaka watu wazima au wasichana kimtandao na kuwazika; kuua watoto wako au mwenzi wako ili upate bima etc.

Dini ni kama OPIUM. Mbona maovu ni mengi tufanyao watu wa dini na wa kusali sana sasa huko kuchinja ndio kutuletee uzoba mpaka tuuane? Kuna lililojificha hapa litaonekana tu muda si mrefu!!

2 comments:

Mbele said...

Lo, hiyo makala safi sana. Inafikirisha na inathibitisha jinsi ujinga ulivyoshamiri katika jamii yetu wa-Tanzania.

Anonymous said...

Vurugu mnaanzisha nyie wenyewe wakristo halafu hapa unatoa mifano ya Afghanistan kunakolimwa Cocaine. Mbona hutoi mifano ya mapadri na maaskofu wa kanisa katoliki walio na scandal za kulawiti watoto wadogo wa kiume?

Nilitegemea kama msomi wa Sociology usingekuwa biased ungeeleza wazi hizi vurugu zimesababishwa na nini na zimeanzishwa na nani. Tunajua mnaanzisha hivi vurugu ili kuzima na kututoa nje ya mada, inayohusu madai ya waislamu ya miaka mingi, HATUDANGANYIKI, wala hatuna mpango wa kugombea kuwachinjia nyie nyama. Nadhani umeshaona waislamu wameshaanza kuchukua hatua za kujiandaa na machinjio yao yatakayosimamiwa na waislamu wenyewe na ambayo tutanunua nyama ambayo tuna uhakika kabisa kuwa ni HALAL kulikoni hivi sasa ambavyo hatujui hayo machinjio ya serikali kama yanafuata taratibu za kiislamu.

Vurugu zenu ni neema kwetu maana hapa tulipo tukienda kwenye mahoteli hatuli hovyo kama unavyofikiri, mara nyingi tunakula samaki au mboga mboga. Isitoshe tutakuwa na maduka au mabutcha maalum ambayo tutakuwa tunanunua nyama iliyo HALAL. Ajabu gani waislamu kula halal meat? Mbona wayahudi wanakula Kosher meat na hamuleti zogo? Iambieni serikali yenu iwape Waislamu uhuru wa kufanya mambo yao ikiwemo uhuru wa kuabudu kwa kuruhusu kuwa na machinjio yao kisha hayo machinjio ya serikali nendeni mkakate nyama mnavyotaka au hata mkitaka kuwanyonga poa tu kwani wakati huo sie tutakuwa na uhakika wa kula halal meat. Tunakula halal meat kiafya zaidi kwani kuchinja kwa kiislamu kunapelekea kudrain damu ambako kunapunguza acidity kwenye nyama.

Kuhusu Ulaya si kweli eti hakuna machinjio ya halal meat au hayafuati taratibu. Ninaishi Norfolk UK ambako kuna machinjio makubwa yanayofuata kanuni za kiislamu na nyama kutoka hapo inasafirishwa mpaka France na nchi nyingine za UK. Nina uhakika wa kula halal meat nikiwa nje ya Tanzania kuliko Tanzania. Na nina uhakika wa kuwa na uhuru wa kuabudu dini yangu nikiwa UK kuliko Tanzania ambako watu hupewa mpaka kazi kwa ajili ya dini yao. Tena hapo UDSM ndipo kumezidi maana kama mtazamo wa mwalimu wa Sociology ndio huo wa kuwa biased unategemea zaidi.

Naomba nikuulize ni kwanini sasa hivi wakristo wanadai wawachinjie nyama waislamu? Kwanini zamani walikuwa nyama iliyochinjwa na waislamu bila kuleta vurugu? Ni kitu gani kinaendelea sasa hivi? Kama ni OK kula vibudu au mlikuwa mnakula vibudu kinawashinda nini sasa hivi kula nyama iliyochinjwa na waislamu? Na je mmeshikiwa mitutu ya bundiki muende mkanunue hizo nyama? Si muache tu kununua hasara itakuwa juu yao, kitu gani kinawafanya muanzishe vurugu kwa ajili ya nyama?