Saturday, June 15, 2013

Sitaki kufa Masikini kama Mangwea! -Ommy Dimpoz

 Jamani, sasa hii kuita watu Celebrity sijui Supastaa huko Bongo Unawafanya wengine wawe na AKILI FINYU!
******************************************
KUTOKA FACEBOOK -   
Sheria ni Msumeno   

Ommy Dimpoz
 MAJANGA!!!!! --HUYU NDIYE OMMY DIMPOZ, MSANII WA BONGO ALIYEAMUA KUMTUKANA MAREHEMU MANGWEA!.

MATUSI : Sitaki kufa Masikini kama Mangwea!
NGWAIR,AMEKUFA AFRIKA KUSINI,HATA KUUSAFIRISHA MWILI KUULETA TANZANIA IMEBIDI MPAKA WATU WACHANGIE,ILE NI AIBU SANA",alisema Ommy kwa dharau.

... Vile vile Ommy baada ya kushinda tuzo ya video bora ya mwaka Ommy alibwabwaja:"jamani tumechoka kuzika wasanii maskini wenye majina makubwa",kama vile haitoshi Ommy alizidi kusisitiza kuwa HATAKI KUFA MASKINI KAMA NGWAIR,

Nikitazama sura yako ya upole,vidimpozi vyako hivyo yaani hata huelekeani na shombo hili ulilojipaka,
Kwa kweli nimesikitika sana hasa msanii kama wewe Ommy Dimpoz umekuja juzi tu umeshaanza kujikweza na dharau kiasi hiki?, ukweli nyimbo zako binafsi nazipenda na una kipaji ila utumbo huu uliotoa utaumeza maana Mungu hajaribiwi, hakuna mwenye mamlaka juu ya kifo,ni Msiba gani hukuona mchango?,

je Umasikini wa Ngwair ni lini uliupima? uliwahi kusikia familia yake imelala njaa?, alishawahi kukupiga mizinga?,
Ninachojua mimi Marehemu(Dead Body) kamwe hapewi tuhuma kwa sababu hayupo around kuji-defend,once ukiamua kushusha tuhuma dhidi ya dead body jiandae kujibiwa na Mungu aliyemchukua.

Kama unahitaji kuhamasiha utajiri kwa wasanii ni vema ukaandaa mikutano na Warsha na walio hai,sasa wewe unamuita Marehemu Fukara????? this is Shit!!!, Babu zako,wajomba zako,na woooooote wamekufa matajiri???, Once U talk again,talk in decent way.

### Aisee hiki ni kituko,sijui fans wangu mnaonaje hili!!!
 
 

4 comments:

Anonymous said...

Inawezekana huyu aliyepost utumbo huu ana akili finyu kama za huyu ommy zimpoz au afadhali hata ya ommy dimpoz. Mambo mengine ya kibwegebwege ukiyasikia unatakiwa uyadharau tuu kisha ukaendelea na hamsini zako.

Bunny Wailer alipoulizwa kwanini Wailers wenzake (Peter Tosh na Bob Marley) wamekufa mapema; Bunny akajibu: "Them brothers were so weak, thats why they are not with us today".

Kauli ile ingekuwa imetolewa na mswahili na kwa kiswahili; basi ingekuwa nongwa.
Ukisikia mtu ameongea kitu ambacho wewe unadhania ni uppuzi, basi achana na upuuzi wake endelea na maisha yako. Kuanza kubwabwaja "oooh sijui na wewe mungu atakuonyesha"; Mungu hafanyi kazi zake kwa kumfurahisha mwanadamu.
Binadamu ndiye anayetakiwa kufanya kazi zake kumfurahisha Mungu.

Anonymous said...

Naona Ommy Dimpoz keshapanga kwamba labda atakufa miaka 40 au 50 ijayo. Hajui kwamba anaweza kufa wakati wowote, hata leo. Kama akifa leo sidhani kama tunaweza kusema Ommy Dimpoz kafa tajiri.

Anonymous said...

Aliyeandika hapo juu next time fanye uchunguzi kwanza ndo aandike yy akuongea kwa maana mbaya kama ww ulivyoipost kwenye blog yako eeh jamani mbona unatupotosha ili tumchukie ommy D.kuna wapuuzi wasiopenda maendeleo ya wasanii wanataka kuvalia njuga suala hili kuipotosha jamii ili mtoto wa watu achukiwe.sisi ni mashabiki wake na tutaendelea kumsapot.mapokeo siku zote uja tofauti.FANYA UCHUNGUZI KABLA UJATUPOTOSHA WASOMAJI

Anonymous said...

Muh jamani watanzania mnapenda kushadadia maneno eeeee mtoto wa watu mumuache eeeh Ommy d.kuna wajinga wachache mnataka kumchafulia jina .una ushahidi gani ww uliyeandika hapo.