Tuesday, June 18, 2013

Saida Karoli ni Mzima! Hajafa!

Wadau, ndo Uselebriti huo, Uzushi mwingi! Saida Karoli yu Hai!  Mungu azidi kumbariki!

Hakuwemo kwenye boti iliyopata ajali, Ziwa Victoria!


*********************************************
Taarifa ya Neville Meena kuwa ingawa ni kweli kuna ajali ya boti iliyotokea, mwanamuziki Saida Karoli hakuwa mmoja wa waliokuwemo kwenye boti hiyo na yuko hai!Taarifa hiyo imetoa angalizo kutafuta uhakika kwani inasemekana kuwa Saida Karoli ni mzima, yupo jijini Dar es Salaam: “Nimetafuta namba yake ya simu sijaipata, ila taarifa kutoka Bukoba na ofisi ya Ofisa Utamaduni Muleba zinasema siyo kweli…” ameandika Meena.
Kuhusiana na ajali ya boti, Meena amesema, “…ni kweli kwamba kuna boti imezama katika Ziwa Victoria, na kulikuwa na uvumi mwingi mjini Bukoba na Wilayani Muleba kuhusu mwanamuziki huyo kufariki lakini baadaye ikathibitika kwamba hakuwa mmoja wa abiria.”Nayo Upland FM radio, Kwa kupitia Facebook page yake, imekanusha taarifa za kufariki Saida kalori na kusema msanii huyo ni mzima wa Afya. “TAARIFA: Kumezuka habari zisizo rasmi juu ya mwanamuziki SAIDA KALORI. Tunaomba kuthibitisha kwa Mwanamuziku huyo ni MZIMA wa afya kabisa. Usidanganywe na uzushi wowote. ASANTE.” imesema taarifa hiyo ya Upland FM

4 comments:

emu-three said...

Wanamuombea maisha marefu...Tupo pamoja mpendwa

Anonymous said...

Hizi redio nazo jamani! Sasa wanarusha hewani habari bila hata confirkation.? Mie niliogopa hata kutoa pole maana moyo uliniuma sana.
Mungu ashukuriwe Karoli ni mzima

Anonymous said...

RUMOURS THAT HIT THE SOCIAL MEDIA LAST NIGHT HAVE BEEN PROOVED TO BE LIES BY SAIDA KAROLI HERSELF.'I AM ALIVE AND WELL AND DO NOT HAVE PLANS TO DIE YET' THATS WHAT SHE SAID. AFTER BEING IN DAR ES SALAAM LAST WEEK SHE HEADED FOR MAKONGOROSI , CHUNYA WHERE SHE STILL IS UP TO THIS MORNING, HUNDREDS OF MILES FROM LAKE VICTORIA
RUMOURS THAT HIT THE SOCIAL MEDIA LAST NIGHT HAVE BEEN PROOVED TO BE LIES BY SAIDA KAROLI HERSELF.'I AM ALIVE AND WELL AND DO NOT HAVE PLANS TO DIE YET' THATS WHAT SHE SAID. AFTER BEING IN DAR ES SALAAM LAST WEEK SHE HEADED FOR MAKONGOROSI , CHUNYA WHERE SHE STILL IS UP TO THIS MORNING, HUNDREDS OF MILES FROM LAKE VICTORIA

G. Sengo said...

Ni habari za uzushi, ni habari zisizo makini kutoka vyanzo visivyomakini, mara baada ya uzushi nimeongea na meja wake jana majira ya saa 4 usiku akashangaa kuhusu habari hizo, halikadhalika producer (mtayarishaji wa muziki wake) toka Tivol Studio Mwanza wote wanashangaa juu ya taarifa hizo wakisema si za kweli.

Kwa hivi sasa Msanii Saida Karoli yuko salama salmin ndani ya vijiji vya mkoa wa Mbeya akisambaza sanaa yake kwenye majukwaa ya pande hizo.

Nikazama zaidi zsubuhi hii Nimezungumza naye live kwa njia ya simu amekanusha taarifa hizo akilalamika juu ya taarifa hizo kuzua huzuni, usumbufu na taharuki kubwa kwa ndugu zake na mashabiki wa muziki wake nyumbani kwao mkoani Kagera, ambapo wake kwa wanaume hata watoto wamefurika nyumbani kwao kukesha wakiweka msiba.

Kibaya zaidi simu yake ilikuwa haipatikani hivyo ikawa vigumu kuhakiki.

Saida amewapa pole kwa usumbufu ndugu, marafiki na watoto wanaompenda.

Mwenyezi Mungu ibariki sanaa ya mikono ya Saida Karoli.
Mpe maisha mwanamuziki huyu mwenye karama ya muziki asili.
Mungu ibariki Tanzania.
Zaidi sikiliza sauti yake mwenyewe kupitia www.gsengo.blogspot.com
By G. Sengo