Tuesday, June 25, 2013

Picha Zaidi za Miracle Crusade wa Askofu Kakobe Toronto

Watu wakimpokea Yesu kama Mwokozi wao - Picha Kutoka Kakobe International Ministries

Watu wakimpokea Yesu kama Mwokozi wao - Picha Kutoka Kakobe International Ministries
Watu wakimpokea Yesu kama Mwokozi wao - Picha Kutoka Kakobe International Ministries



Halleluyah!


Baadhi ya Waumini

Baadhi ya Waumini

Huyo kijana wa KiChina kwenye wheelcahir alitoka kwenye mkitano akitembea mwenyewe na furaha kubwa!


Wagonjwa wakiombewa

Gari la  Mama Nuru wa Toronto!



Baadhi ya Walinzi

8 comments:

Anonymous said...

Ubarikiwe dada Chemi kwa kutujuza na kutuwekea picha. Wale waliokuwa wanahoji maelfu ya watu wako wapi, nadhani kwa picha hizi wamepata majibu sahihi.

Watanzania tuwe na desturi ya kuwa-support watumishi wa Mungu badala ya kuwa na roho ya kaa na wivu wa kijinga.

Bwana Yesu akubariki sana dada.

Anonymous said...

!!!!!

Anonymous said...

Hizi picha zimepigwa kisanii. Kwa nini wametumia camera ya 1959 wakati zipo digital camera? Huyo mchina "aliyepona" ulemau wake; tuwekeeni picha yake kabla hajapona na baada ya kupona.
Kwa sisi tunaoishi nchi za magharibi; kama ni kweli mlemavu angepona ulemavu kwa jina la yesu, basi hiyo ingekuwa habari kubwa kwenye tv na magazetini. Wangeitwa ma profesa, ma -physiotherapist, na wataalamu wengine wa aina hiyo kujadili uhusiano wa imani na kupona ulemavu.

Wewe endelea na desturi yako ya kuwasapoti hao unaowaita watumishi wa mungu, na mimi sina matatizo na watumishi wa mungu. Tatizo langu ni "organised deception".

Wizi mtupu.

Anonymous said...

Hawa labda tuseme ni mamia, si maelfu. By the way, mbona Chemi kila unapo-post habari za Kakobe mtu wa kwanza ku-comment lazima atamsifu Kakobe na kukumwagia sifa kemkem pamoja na kukuombea? Is this thing stage-managed or what?

Anonymous said...

Askofu Kakobe ni mtumishi wa Mungu. Ningekuwa na hela nami ningeenda Toronto kumsikia. Bwana Yesu Kristu Asifiwe sana. Amen.

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 6:57am, watu wanatuma comments zao, they are approved in order received. Check the time stamp. No, this is not stage managed, sorry to disappoint you. There are believers and supporters.

Anonymous said...

Tusaidie ndugu, maelfu inaanza na idadi ya watu wangapi? Basi sema makumi ukipenda ili roho yako ifurahi. Lakini mbele za Mungu hata angekuwa mtu mmoja na kumpokea Bwana Yesu basi mbinguni kunakuwa na furaha kubwa.

Anonymous said...

Asante sana Chemi. kazi yako ni njema kwa kutupasha habari za Toronto. Kuhusu idadi ya waliohudhuria, mimi nasema, idadi hiyo ni kubwa sana, ukizingatia kuwa watu wa magharibi, wengi wao kwa sababu ya maendeleo waliyo nayo wanaona kuwa neno la msalaba ni upuzi! Isitoshe, mikutano mingi inayofanywa huko haina miujiza mikubwa. Si ajabu walifikiri hata huo mkutano wa Askofu kakobe utakuwa wa kawaida!