Thursday, June 06, 2013

Khadija Kopa Afiwa na Mume Wake!

Nimepata taarifa kuwa mume wa malkia ya mipasho, Khadija Kopa,  Mr. Jaffari Ally amefariki dunia saa 9 usiku wa kuamkia leo. Nitabandika updates nikipata. 

Pole sana Dada Khadija Kopa.   Mungu akutie nguvu katika kipind hiki kigumu.  Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi. Amin.

Naona salamu za pole zinamiminika kwenye Facebook page yake: https://www.facebook.com/MalkiaKhadijaKopa?fref=ts 
  
Jafari na Khadija Kopa, walifunga ndoa mwaka 2008.
 
 Wakati kifo hicho kinatokea mke wake hakuwepo jijini Dar, kwani alikuwa safarini Rukwa alikokwenda na kundi zima la TOT kwa ajili ya kusherehesha Sherehe za Siku ya Mazingira Duniani zilizofanyika Kitaifa mkoani humo, ambapo leo anatarajia kuwasili jijini. 

Ratiba kamili ya msiba huo bado hadi sasa haijafahamika lakini inadhaniwa huenda msiba huo ukawa  maeneo ya Chaline au Lugoba ambako ni nyumbani kwa wazazi wa Marehemu.
***********************************************
Khadija Kopa (kulia) mume wake na watoto wao mwaka jana kwenye tuzo.

Khadija Kopa akiwa na mumewe kabla ya kupanda jukwaani kutoa burudani  (picha ilipigwa 2012)


MUME WA KHADIJA OMARY KOPA"MALKIA WA MIPASHO TANZANIA"AMEFARIKI USIKU HUU MIDA YA SAA TISA USIKU POLEE SANA KHADIJA KOPA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI

BWANA AMETOA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE!
"AMEN"

No comments: