Monday, June 24, 2013

Askofu Kakobe Amaliza Ziara Yake Toronto, Canada

Wadau, nimekuwa hapa Toronto, Canada kwenye mkutano wa Askofu Kakobe. Maelfu ya watu wa kila rangi na hata waislamu walitokea. Kulikuwa na wahindi, wachina, wakorea, wazungu pamoja na waafrika wengi. Tumeshuhudia miujiza!  Jana kijana wa kiChina aliyekuwa kwenye wheelchair aliweza kutembea. Bibi ambaye alikuwa kwenye wheelchair miaka 18 aliweza kutembea, viziw walisikia!  Watu waliolewa mapepo! Hapa Toronto, Askofu Kakobe amefanya mengi! Mkuanta huo ulikuwa  June 20-23, 2013 Rexall Centre, York University.  Kweli Mungu anamtumia Askofu Kakobe!

Nimepiga picha hizi kwenye mkutano jana na juzi.

Askofu Kakobe Jukwaani

Walioamua kuokoka

12 comments:

Anonymous said...

Dada Chemi

Ubarikiwe Sana, Kazi yako ni njema mno,Kwa jinsi ulivyosimamia ukweli kuhusu mtumishi wa Mungu Askofu Kakobe na kuamua mwenyewe kwenda katika mkutano huu Toronto na kuacha kusikiliza maneno ya vijiweni ya watu ambao hata hawamjui Askofu Kakobe ambao wanashindwa kufanya utafiti kidogo hata kuamua kwenda pale kanisani Mwenge.

Umemtangaza Bwana YESU kwenye Blog yako, Mungu akuzidishie maradufu afya tele, uzima na mafanikio. Amen

Anonymous said...

Tunaomba picha ya mlemavu mmoja tuu aliyepona kwa miujiza ya bwana. Tupatie picha yake kabla hajapona na picha nyingine baada ya kupopna ulemavu wake.
Bwana asifiwe.

Anonymous said...

hayo 'maelfu' yko wapi?

Anonymous said...

Atarudi lini Tanzania? Au ndio ameondoka moja kwa moja?

Anonymous said...

Atarudi wiki ya kwanza ya Julai 2013

Anonymous said...

Atarudi wiki ya kwanza ya Julai 2013

Anonymous said...

Dada Chemi,

Tunakupenda sana, na Kwasababu umemwinua Bwana Yesu, naye akuinue katika maisha yako.

Anonymous said...

duh ndugu zangu kwa jinsi ninavyoijua toronto,ni watu wenye dharau kubwa hasa kwa ngozi nyeusi,lakini kama wameweza kuja kwa wingi wao hivyo na kuokoka kwa wingi,hakika huyu ni Bwana.kule toronto walishawai kabisa kumnyima viza raisi nelson mandela eti kwa kuwa aliwai kufungwa miaka 27 jela

Anonymous said...

Da Chemi wetu angalia usipotee.

Anonymous said...

Jamani askofu kakobe amerudi jumatatu hii.hivi kwa nini waandishi wengi wa habari wa hapa tz ni wanapenda kuandika habari za uongo? Kwa nini wanawapumbaza watz kwa uongo wao..wa habari wasizozifanyia uchunguzi..hivi wangeenda ulaya wangeandika habari gani? Mfano wangekuwa raia wa kwa obama wangetambulika kama waandishi kweli? Mbona wanashusha hadhi ya taaluma ya uhandishi wa habari? Waliandika kakobe katoroka wakati alienda canada kiinjili na aliondoka kwa baraka zote toka kwa washirika wake sasa amerudi jumatatu wasema uongo wana la kuandika tena? Ni aibu imewashika..mimi ningekuwa waziri wa habari kwa kweli ningewachania vyeti vyao waandishi wa habari wanaoandika habari kwenye magazeti n.k ambazo hawajazifanyia uchunguzi...waandishi wa habari mbadilike tena mkamuombe msamaha askofu kakobe...kwa ujinga mliofanya.Asante dada chemi kwa kutujuza ya huko toronto.

Ditrick Mkinga said...

Najivunia kuwa na Baba yangu wa Kiroho kakobe ambaye anatumiwa na Mungu kwa viwango vya juu sana. Mungu ambariki sana.

Ditrick Mkinga said...

Najivunia kuwa na Baba wa kiroho Askofu Mkuu Zachary Kakobe ambaye anatumiwa sana na Mungu. Mungu azidi kumbariki katika huduma aliyoitiwa ya kuipeleka Injiri hata miisho ya dunia.