Saturday, May 17, 2014

Msanii Adam Kuambiana Afariki Dunia

Wadau, leo nimepokea habari za kusikitisha za kifo cha Msanii, Adam Kuambiana.  Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni. Amen.


 KUTOKA LUKWANGULE BLOG

The Late Adam Philip Kuambiana

HABARI  haziko wazi lakini marafiki w akaribu wamethibitisha kwamba dairekta anayekuja juu, muigizaji na mwandishi wa sinema Adam Phillip Kuambiana PICHANI amefariki saa chache zilizopita.

Mkali huyo mwenye tabia 'ngumu ' (hana simu ya mkononi) labda sasa, ameshiriki kama muigizaji au dairekta katika sinema Lukuki na amekufa akikimbizwa hospitali ya Sinza palestina.

    Hizi ni baadhi tu ya kazi zake njema:
    Danija
    Faith More Fire|
    Bad Luck
    Scola
    The Boss
    Mr.Nobody
    Radhi ya Mke
    Lost Sons
    Chaguo Langu
    My Fiance
    Jesica
    Life of Sandra
    Basilisa
    My Flower
    Regina
The Late Adam Kuambiana
    Born Again
    Its Too Late
    Fake Pastors


Nilimpenda sana kuambiana katika filamu ya Fake Pastors.

Vijana watanashati Vicent Kigosi (Patric) na Adam Philip Kuambiana (Petro) waliohitumu Chuo Kikuu cha Mzumbe, Morogoro Vichwani mwao wanaelewa kitu kimoja tu walichoambiwa tangu utotoni kuwa ukiwa na digree masiha yatakuwa rahisi jambo ambalo baada ya kuingia mitaani wanakuta ni tofauti kwani hakuna ajira na maisha yanakuwa magumu sana kwao.

Baada ya kutembea katika ofisi moja hadi nyingine wakitafuta kazi bila mafanikio, hatimaye wanagundua kuanzisha kanisa ndio suluhisho pekee walilobakiza hivyo wanaamua kuwa wachungaji wa uongo (Fake Pastors) na kuanzisha kanisa kwa lengo la kujitajirisha badala ya kumtumikia Mungu, kazi yao inakuwa ni kuwakamua waumini fedha na mali walizonazo. 
Kwakufanya hivyo wanajikusanyia utajiri mkubwa hasa baada ya misaada kuanzia kuingia kutoka nje kwa wahisani, baadala ya kufanya kazi ya Mungu wao wanazitumia fedha hizo katika anasa wakilewa pombe na kununua Malaya usiku na ifikapo asubuhi wanahubiri injili kama kawaida na kuwafanya waamini wazidi kuwakubali.  Baadae walijingiza katika biashara haramu dawa za kulevya ndipo Mungu Mbinguni alipoamua kuingilia kati na kuwaadhibu vibaya.

Cast: Adam Philip Huambiana (Petro), Vicent Kigosi (Ray),  Jokette Mwegelo (Jach), Lisa Jensen (Lisa), Blandina Chagula

Producer- Vicent Kigosi, Executive Producer- Eric Shigongo, Director- Gervas Kasiga


7 comments:

Anonymous said...

du! kweli bongo movies kunani? poleni xana wadau wenzangu wote,ila tusimsahau mungu. RIP

Anonymous said...

Hili jamaa ni Bonge la Actor na Director apa bongo, binafsi namkubali sana , level zake za majuu wala hakustahili kuwa bongo movie maana ni kichwa sana.

Tatizo kubwa alilonalo huyu mshkaji ni u much know sana, anajiona mungu mtu bongo movie, hataki kukosolewa na yeyote halafu mbabe, juzi tu katoka kuwapa kichapo heavy wema sepetu pamoja na mwenzie aunty Ezekiel kwa kosa la kijinga, pia alishawahi kuwapa kichapo Johari pamoja na rose ndauka kwa sababu za kipuuzi tu.

Tatizo lingine la huyu jamaa aiseeh ni mwizi kuliko hata neno lenyewe , wasanii wenzie wanamlalamikia sana kwa tabia yake , sema hawamwambii kwa kuwa ana mkono mwepesi kupiga, wanamuogopa ila aiseeh jamaa ni mwizi sana , mpaka wasanii wameshaambizana wakiwa nae location wawe waangalifu na vitu vyao maana jamaa hachagui cha kuiba chochote twende , kingine wana muheshimu kwa kuwa anajiheshimu ata yeye mwenyewe, so wanamkaushia ila kwa wizi jamaa ni noma sana. Kashawaliza wengi sana bongo movie especially mademu

Anonymous said...

What a sad news. He was really taking the art to the next level. What a loss, kwa tasnia ya filamu nchini. Poleni sana wasanii, ndugu, jamaa, marafiki na washabiki wote wa Bongo movie.

Anonymous said...

Adam Kuambiana amefariki dunia wakati akipelekwa katika hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam kwa matibabu alfajiri ya kuamkia leo.

Inatajwa kuwa kabla ya kuzidiwa marehemu alianguka chooni akiwa location katika hoteli ya Silver Rado iliyopo Sinza kwa Remy jijini humo ambapo kabla ya mauti kumfika, Adam alikuwa akilalamika kuwa anasumbuliwa na tumbo.

JP said...

Kwa kweli kifo chake hakipishani na kifo cha aliyekuwa msanii wetu steven kanumba kwani ni cha ghafla mno na kinasikitisha, mungu ailaze roho yake mahali pema popeni amina.

Mkandamizaji said...

Pipooooooooo! Chukueni tahadhari sana, tena sana. Msipuuzie hili jambo tena kuanzia sasa. Msije mkala vyakula kama :- Burger, Pizza, Birian, Pweza, Kababu, Chips Kuku, Sandwich, Chops, Supu ya Maini, Mishikaki ya kuku, Meat Cake, Mkate wa nyama na kuendelea bila kunichukulia na mimi maana na mimi napenda!!

Anonymous said...

I think he was the best director and one of the best Actor in #Tanzania...so so sad, REST in PEACE Adam Kuambiana!!