Saturday, May 31, 2014

Tumshukuru Mungu


Kama una Chakula kwenye fridge yako,
Nguo mwilini mwako,
Paa juu ya kichwa chako na sehemu ya kulala,
Wewe ni tajiri zaidi ya 75% ya watu dunia nzima!


Kama una hela kwenye pochi yako
na unaweza kwenda popote utakapo,
Wewe ni mmoja kati ya 18% ya watu matajiri wa juu duniani.

Kama upo hai leo
na afya zaidi ya maradhi,
Umebarikiwa zaidi ya watu milioni
ambao hawatamaliza hii wiki bila ya kufa.

Kama unaweza
kusoma huu ujumbe na kuuelewa,
Una bahati zaidi ya watu bilioni 3 duniani
ambao hawawezi kuona,kusoma ama wana ugonjwa wa akili.

Maisha sio kulalamika
maumivu na huzuni.
Ni kuhusu sababu nyingine
nyingi sana za kumshukuru muumba wetu.

MSHUKURU MUNGU WAKO KWA YOTE


No comments: