Saturday, May 31, 2014

Ukweli Kuhusu Ushuzi

 Kutoka Facebook:

Kujamba kunasababishwa na kubanwa kwa hewa,ambayo inaweza kutoka mwilini kwa njia nyingi.Baadhi ni hewa tuliyoimeza wakati wa kula au kunywa.

Hewa ingine husababishwa na gesi kuingia kwenye utumbo wetu kutoka kwenye damu,na baadhi ya gesi huzalishwa na kemikali katika utumbo au bakteria.

Kwa kawaida "ushuzi" unakua na asilimia 59 ya gesi ya nitrogen, asilimia 21 ni hydrogen,asilimia 9 ni carbon dioxide,asilimia 7 methane na asilimia 4 ni oygen.

Asilimia moja tu ya "ushuzi" inaweza kuwa hydrogen sulfide na mercaptans,ambayo ndio ina sulfur ndani yake,sulfur ndo hufanya "ushuzi" utoe harufu mbaya Kujamba huambatana na sauti,hii ni kutokana na "vibration" katika njia ya haja kubwa.

Ukubwa wa mlio wa kujamba hutegemea "presha" inayosukuma gesi itoke nje na pia ugumu wa misuli ya njia ya haja kubwa.

Harufu mbaya ya ushuzi hutegemea na ulaji wa mtu,vyakula vyenye sulfur kwa wingi ndio husababisha hili.Vyakula vyenye sulfur kwa wingi ni kama maharage,kabichi,soda na mayai.
Kwa Baadhi ya Tamaduni,Kujamba Sio Ishu

Wakati tamaduni nyingi zikichukulia tendo la kujamba lifanywe kistaarabu,kuna baadhi ya tamaduni hawaoni haya kujamba hadharani,na pia hufurahia tendo hilo.

Mfano kabila la Yanomami huko America ya Kusini,kwao husalimiana kwa kujamba,na China unaweza kupata kazi ya kunusa ushuzi! Katika Roma ya zamani,Mfalme Claudius akihofia kwamba kujizuia kujamba inaweza kuwa hatari kiafya,alipitisha sheria kwamba ni ruhusa kujamba kwenye "banquets".

Mtu wa kawaida hutoa hata nusu lita ya ushuzi kwa siku.Inasemekana mtu akijamba mfululizo kwa kipindi cha miaka 6,anaweza kuzalisha nishati ya kutosha kutengeneza bomu la atomiki.


3 comments:

Anonymous said...

Duh! Lakini wakati mwingine kweli unavimbiwa! Inabidi uachie.

Linda said...

Hizo za kimya kimya ndo zina nuka zaidi!

Anonymous said...

Noma kweli! Uko kwenye kundi la watu halafu unasikia ushuzi unaanza kutizama ni nani kaachia. Ni kweli vya kimya ndo vinanuka zaidi.