Thursday, May 29, 2014

Mtoto Shigella Afariki Dunia - Alizaliwa na VVU (HIV)

10342004_1886404071498512_8618777191309208307_n

Marehemu Shigela ezni za uhai wake akihojiwa na Mtangazaji wa Kipindi cha Mimi na Tanzania Hoyce Temu.

Mtoto Shigela amefariki dunia asubuhi ya leo tarehe 29/05/2014 nyumbani kwao mkoani Mwanza akisumbuliwa na maradhi ya Moyo.

Mtoto Shigela alikuwa ni mmoja kati ya watoto waliozaliwa na VVU na kipindi cha Mimi na Tanzania kilimtangaza na alipatiwa misaada mingi toka kwa Watanzania .

Bado msaada wako unahitajika kukamilisha mipango ya mazishi kwa mtoto wetu mpendwa Shigela.

Namba ya simu ya dadake Shigela 0758343178.

Bwana ametoa na bwana ametwaa,jina lake lihimidiwe.

Taarifa hii imetoka kwenye Akaunti ya Facebook ya Hoyce Temu.

10342503_1886404114831841_5868107759100328651_n

Mtangazaji wa kipindi cha Mimi na Tanzania Hoyce Temu akifurahi na Marehemu Shigela enzi za uhai wake.

No comments: