Tuesday, April 10, 2007

Awatukana eti ni Malaya wenye nywele za kipilipili!

Captain wa Timu ya Rutgers, Essence Carson, akiongea na waandishi wa habari leo 4/10/07.

Mbaguzi Don Imus

Ubaguzi hauishi Marekani. Wiki iliyopita kuna huyo mtangazaji maarufu wa Marekani, Donald Imus, kasema eti wasichana wanaocheza basketball kwenye timu ya Chuo Kikuu cha Rutgers ni nappy headed hos (malaya wenye nywele za kipilipili). Alikuwa anaongea na meneja wake kwenye hicho kipindi na walizidi kusema wamejaa matatoo na pia wamekaa kidumedume. Kisa timu ya Chuo Kikuu cha Tennessee iliwashinda katika mashindano ya Basketball ya wanawake.

Mazungumzo enyewe ni hayo:

Imus started the firestorm after the Rutgers team, which includes eight black women, lost the NCAA women's championship game to Tennessee. He was speaking with producer Bernard McGuirk and said "that's some rough girls from Rutgers. Man, they got tattoos . . ."

"Some hardcore hos," McGuirk said.

"That's some nappy-headed hos there, I'm going to tell you that," Imus said.
Pia walisema kuwa eti hiyo timu ya Rutgers inafanana na timu wa wanaume ya NBA, The Toronto Raptors!"

Jana alikutana na Reverend Al Sharpton kuomba msamaha lakini Sharpton alikasirika baada ya Imus kusema, "You People!" (Nyinyi watu weusi). Na Reverend Jesse Jackson naye amekasirika ana anataka Imus afukuzwe kazi. Jackson kasema hiyo siyo 'Slip of the Lip' (Utelezi wa ulimi).

Lakini kwa hapa Marekani kusema kuwa mtu mweusi ana nywele za kipilipili ni tusi kubwa mno! Hii inatokana na asili ya utumwa Marekani. Pia nywele za kilipili inahusishswa na watu wesui hasa weusi tii. Na kama unataka kuelewa kwe undani zaidi ni kuwa hapa USA, unavyozidi kwa weusi ndo unavyoshushwa kwenye hadhi ya ubinadamu. Insikitisha! Weusi wenyewe wanadharau weusi na hasa weusi tii. Unasikia, "You Too black" yaani wewe ni mweusi mno. Ama kweli Imus, kachokoza watu.

Haya mambo ya nywele ni mjadala mkubwa maana utasikia weusi wanasema, yulekichwa chake kimejaa 'naps' (Kipilipili), na yule ana good hair (nywele nzuri), zimekaa kizunguzungu. Biashara ya ku-perm na ku-relz nywele kusudi zinyoke kama mzungu imeshamiri duniani. Hata Bongo watu hawaridhiki na nywele waliozaliwa nayo, unatukuta watu wanakimbilia saluni kupata 'relaxer'.

Na huyo Captain wa timu leo kaonekana na nywele ambazo zimetiwa Relaxer! Zimenyoka kabisa. Ningemheshimu zaidi kama angetoka na Afro. Ni kama vile wanaona haya kuwa na nywele za kiafrika.

Tangu enzi za utumwa hapa Marekani wanasema kama una hata tone moja ya damu nyeusi basi wewe ni mweusi. Unakuta watu ambao ungedhania ni wazungu lakini la, ni weusi! Na kama umetazama ile sinema ya School Daze ya Spike Lee, utaona mgogoro kati ya wanafunzi weusi. Weupe wanajiona bora kuliko wale ambao ni weusi zaidi.

Haya sasa Imus amesimamishwa kutangaza redioni kwa kipindi cha wiki mbili. Watu wanataka afukuzwe maana wanasema kuwa si mara yake ya kwanza kuongea mambo ya kibaguzi. Siku zijazo tutasikia hii 'issue' inaishia wapi.

Kwa habari zaidi mnaweza kusoma hii tukio:



13 comments:

Anonymous said...

Chemi, ebu tuletee stori hevi sio hizo za watu kutukanwa wakati wao kwa wao pia wanatukanana sana mitaani.Sasa wapi noma akisema mzungu ndio noma ,lakini akisema mswazi sio noma.Noma ni noma tu au sio!!.Zile stori za matako umepeleka wapi ama za maafande enzi za ukuruta?Achana nao hao.

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 10:47AM, asante kwa maoni yako.

Ucheki kushoto utaona Archives, kwa hiyo cheki February 2005, utaona story ya matako makubwa. Nyingine mpya inakuja. Nafikiria nizungumzie 'angle' gani.

Anonymous said...

Kweli kabisa Chemi, hayo marumbano ya watu weusi Marekani hayana haja ya kutuchukulia muda wetu. Ilitakiwa wenyewe waheshimiane na ndipo waheshimiwe. lakini kama wao kwa wao wanadharauliana unategemea mzungu atakuwa katika nafasi gani ya kuwaheshimu hao weusi. Kwa mfano wanaitwa hivyo, halafu weusi wasiige kuwa na nywele za kizungu ingekuwaje. Rahma-Ukraine

Anonymous said...

Wote weusi tusi kwa mmoja tusi kwa wote huu sio wakati wa kukubali matusi na kushabikia matako makubwa peke yake. Mtu mweusi amka!

Anonymous said...

Chemi sijui kwa nini weusi waliobaguliwa huwa hawako proud na rangi yao nakumbuka nilikuwa nasoma capetown watu wengi na machotara na wale weusi tii walikuwa wanabaguliwa hata kwenye discussion group,hata marafiki hawana wengi,kama umefika south Africa utanote wenyewe wasouth Afrika hawako dark kama waafrika wengine hasa cape town,kiasi kwamba pale chuo weusi sana walikuwa majority wageni mfano wazambia,nigeria walchokua wanakoma na waafrika wenzao ni umoja wao halafu wanapesa zaidi,na kuna kabila moja wanaitwa wavenda wenyewe ndio wako dark zaidi basi ukiwa mvenda unadharaulika kwa ajili ya ngozi wengine wanaficha na wenyewe wasouth wanasema wavenda ni product ya mozambique na sio wasouth halisi,sio europe tu au america bali hata africa ubaguzi upo ,waafrika tuna tabu sana.

Anonymous said...

Chemi,sikuanza kutoa maoni ili kuleta marumbano,isipokua nilitaka kukufanya ujue tunaofuatilia blog yako labda tunapendelea nini.Sasa hoja kama hiyo ya kusema akitukanwa mweusi tumetukanwa wote inatoka wapi?yaelekea huyo mwenzetu hajawa karibu na hawa wenzetu.Labda kwa kumsaidia hawtukubali kabisa sie tunaotoka afrika,hata kwa sasa angalia eti wanadai kwamba hata Obama sio wa kwao kwa sababu tu baba yake ni mkenya!!Sasa huu weusi wa kutu-unite utoke wap!!??.Chemi kazi kwako,najua wewe hunifahamu ila mwenzio nakufahamu sana na mwezi ujao semester inakwisha naenda zangu Dar tutaonana nikirudi,nitajitambulisha kwako.Tchao

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 10:03am, asante sane kwa maoni yako. Na nitafurahi sana kukufahamu zaidi ukirudi kutoka Dar.

Na ni kweli insikitisha ukisikia wanasema eti Obama siyo Black American. Tena weusi wanasema hivyo. Mimi nimeolewa na Black American, na kwa kweli wengi wa familia yake wananipa shida sana mpaka tumeamua tujitenge nao. Basi, tunaonana siku moja moja na shemeji zangu, baba mkwe nakadhalika japo wako karibu Roxbury. Mpaka mwanangu kaniuliza kwa nini wanatuchukia. Ukisikia comments zao kuhusu Africa utasikitika, eti wataliwa, waafrika wana kula watu. Kuna mtu ana tunga script ya sinema kuhusu uhusiano kati ya Black Americans na waafrika nami nachanga story zangu.

Kama una nafasi tazama ROOTS, utaelewa zaidi historia ya wao kuchukia waafrika na uweusi.

Simon Kitururu said...

Ni wiki moja imepita tu.Nilikuwa naongea na Marekani mmoja mweusi. Ilipofikia pointi ya Obama akasema ni aibu kwa Wamarekani weusi asili kuzidiwa bao na nusu Mzungu nusu Muafrika katika siasa ya Juu. Hivyo anaamini kabisa Obama hawawakilishi.Cha ajabu anamke Mzungu na watoto kama Obama.Nilikosa cha kumwambia.

Anonymous said...

Sasa sijui niseme waafrika tuna pepo la kuchukiana? Habari ninazopata za huko Marekani zinafanana tu na ninazoona hapa kuhusu waafrika. Kila mara tunatafuta sababu za kutengana badala ya kuungana. Sasa huko Marekani ilianza na watumwa "wazawa" (waliozaliwa huko) kuwapuuza watumwa "wakuja". Sasa nasikia Obama si black American! Yaani hata mimi nikipata uraia wa Marekani, weusi wenzangu huko wataniita "wakuja"! Na hapa Afrika tunabaguana bado kwa rangi na wahindi, waarabu,hata wasomali! Na tunapobaki weusi peke yetu tunakumbuka makabila yetu, ubaguzi unaendelea! Hili ni pepo, nadhani si kingine. Tuna nini?

Anonymous said...

Nina hamu ya ku-email hii stori kwa rafiki yangu, je nitafanyaje ili niweze kui-email?

Anonymous said...

Chemi, sishangai kabisa ninaposikia habari za racism hasa Marekani, ingawa Don amefika mbali, hope he gets what he deserves, wamezidi sana hawa. Wakati wanatoa comments zao they always mean what they say, kiti kikishakuwa cha moto utasikia eti slip of the toungue shenzi kabisa.
Hata hivyo racism haitaisha Marekani hata iweje, hope he rots in Hell!!

Anonymous said...

Chemi, haya mbaguzi Imus kazi hana kuanzia leo sasa majibizano yamebaki kwa wenzetu,kuna mchangiaji mmoja anadai kitendo cha mabinti kulia mbele ya Imus walipokutanishwa jana kwa ofisi ya Gavana(maskini Gavana mwenyewe hakuweza hudhuria alipata ajari)ni kumpa sifa mzungu mmoja(Imus)na kuonyesha kwamba weusi ni udhaifu.Haya kazi kwao sie tunashuhudia tu.Pole nawe na shemeji zako waambie watanzania hatuli watu,kwani wakati wa safari yako uliandamana na shemeji yetu?Kama mlikua wote yeye sasa ndio anakazi ya kuwaonyesha ndugu zake wafrika wakoje.Lakini kumbuka ndugu zake wataona kama ushamtwanga limbwata na vile ulisoma Unyanyembe akhaa,mie simo.

Anonymous said...

Huyu mzungu shenz taip!!!, chaemi mfikishie ujumbe, hivi Nelson Mandela angewalipizia kisasi kle sauz ingekuwaje!! Shenz taip we mzungu mbaguzi!!