Thursday, April 19, 2007

Kwaheri Sanjaya!









American Idol Judges Randy Jackson, Simon Cowell, & Paula Abdul

Kwa wapenzi wa American Idol naomba maoni yenu. Huyu kijana Sanjaya aliwezaje kukaa kwenye American Idol kwa muda wote huo? Jana alivyotolewa nilibakia nashabikia kwa furaha maana hakustahili kufika hadi kuwa namba 7 kati ya waimbaji kumi na wawili bora.

Sanjaya ni shombe wa kihindi kutoka Washington State. Ana miaka 17. Mama yake ni mzungu na baba yake ni mhindi. Ana nywele nyingi nyeusi, na sauti yake ni ndogo na ya kike kike kama ya Michael Jackson. Anaweza kuimba nyimbo za stevie wonder vizuri. Akiimba wasichana wadogo wadogo wanaanza kulia shauri ya kuingiliwa na kiwewe fulani. Watu wanasema baba yake kamfanyia dawa za kihindi maana hana sauti ya kuwa American Idol.

Watu kama Howard Stern na wengine wenye chuki walifanya kampeni za kupata watu wa kumpigia kura ili ashinde. Mungu ni mwema na wameshindwa! Sanjaya katoka jana kwa majonzi. Alivyoambiwa ndo siku yake ya mwisho, alibakia analia kama mtoto mdogo.
Kitu kilichowafanya wasichana wadogo wadogo wampende ni, kutabasamu kwake, nywele nyingi (kila wiki alibadilisha staili ya nywele), na eti ana sura nzuri yaani handsome. Lakini kuimba hawezi. Watu waliokuwa wanaimba vizuri kama Stephanie Edwards, Brandon na Gina Glocksen walitolewa kabla yake.

Picha aliyepiga dada yake, Shyamali, akiwa uchi huko anapiga gitaa ilimsaidia pia. Shyamali aliwahi kufanya kazi kwenye restaurant ya Hooters. Alitolewa zamani wakati walivyobakia waimbaji 48.
Bora hakushinda maana kuendelea kuwepo kwake ungehatarisha maisha yake, maana nchi hii kuna vichaa. Angepigwa risasi na mtu mwenye chuki eti kawa nini Sanjaya anaharibu show.

Na leo naamini kuwa producers wa American Idol wanapumua vizuri. Maana Sanjaya angeshinda ingekuwa mwisho wa American Idol maana ushindi wake ungehibitisha kuwa American idol siyo kamchagua anayejua kuimba, bali anayependwa na watu.

Lakini huo si mwisho wa Sanjaya. Kwa vile kapendwa sana lazima tutamwona kwenye matangazo ya TV, au akiigiza kwenye sinema za mateenager.

5 comments:

Anonymous said...

Why do you care so much about American Idol. I think you forgot that phone calls are the one that control the winner. If you have enough phone calls you can win the competition regardless of your singing skills.

Chemi Che-Mponda said...

To Anonymous of 11:47am, obviously you didn't understand the gist of what I was talking about. The reason I care about AI, is that I have been a fan of the show since it started (When Kelly Clarkson wona). I always vote for the ones I think are the best. In this case Sanjaya was far from the best but he seemed like a nice kid. I was voting for him when he was amongss the top 24 but when it came to the Top 12, I did not vote for hime once because I thought some of the others were better.

Anonymous said...

Chemi we don't give a fuck about American Idol. We kama kuna watu ungependa washinde hizo ni issue zako na usilazimishe mambo na kusema vitu visivyo na ushahidi. we unajuaje angeuliwa au unavyoandika kuna ubaguzi wa rangi na bla bla. Wat wanampigia simu mtu wampendae.
Nothing personal but try to be more interesting.

Anonymous said...

To Anonymous of 1:29 am, hivi hii blogspot ni ya nani, nilidhani ni ya Chemi, na kama hivyo ndivyo she posts ( and should post about )things that are of interest to HER. if you are not interested in any topic, move on to another topic, website, blog or whatever.Hebu chukua muda uweke na wewe blogspot yako uone urahisi/ugumu wake. Usisahau pia kuwa katika ulimwengu wa leo ni lazima kwenda na wakati. Way to go Chemi, nakuunga mkono kwa juhudi zako

Anonymous said...

sikiliza we anonymos wa 7:31pm hapo juu. kama unaanzisha blogspot inabidi ulenge wasomaji na sio wewe. Kwenda na wakati si kuwaelezea watu mambo ambayo hayawahusu kama lengo lake ni wabongo basi aandikemambo yahusuyo wabongo. Who cares about american Idol.