Saturday, April 21, 2007

Poleni Wanafunzi wa UDSM lakini....

Students trying to Leave UDSM Main Campus
Ofiice Notice about UDSM Closing
Wanafunzi wa Uuniversity of Dar es Salaam (UDSM), waliofukuzwa majuzi wataruhusiwa kurudi Chuoni lakini kwa masharti:

From Michuzi Blog:

" Taarifa za redio mbao zilizonifikia punde ni kwamba wanafunzi wa udsm waliofukuzwa juzi kwa kugoma kuingia darasani wametakiwa waandike barua ya kujieleza ikiwa imeambatanishwa na 100,000/- ya matibabu pamoja na ada asilimia 40 (kama laki nane hivi) kupitia benki na wawe wamezipeleka barua na risiti za malipo hayo ya benki kwa makamu mkuu wa chuo kati ya aprili 23 hadi mei 4 ili kuweza kufikiriwa kurudi chuo. nafanya juhudi kupata waraka kamili wa masharti yote. "


Nimesoma kwenye ippmedia.com, kuwa wanafunzi waliofukuzwa na wasio na familia DSM, wameishia kuuza vitu vyao kama simu na TV ili wapate hela ya chakula na nauli ya kurudi makwao. Wanasema kuwa wasichana 'wanajiuza' ili wapate mahitaji yao. Ama kweli hali inasikitisha.

Nani aliwachochochea wagome? Je, wako wapi? Nikikumbuka miaka ya nyuma na migomo mingine anayeumia ni mtoto wa mkulima, au mtoto aliyetoka kwenye familia enye kipato kidogo. Watoto wanaotoka familia zinazojiweza wanapelekwa 'abroad' kumaliza masomo yao.

Kuhusu eti zamani watu walisoma bure, lazima niseme si kweli. Kumbuka kuwa kulikuwa na JKT, ilikuwa njia moja ya 'kutoa shukurani' kwa serikali kukusomesha. Pia ilikuwa ukianza kazi unatakwa mshahara kwa muda fulani. Kwa kweli ilikuwa si bure. Pia enzi zile wasomi walikuwa wachache. Je wakiamua kurudisha ule utaratibu wa kusomesha mamia kwa mwaka badala ya maelfu hali itakuaje?

Ni mwaka 2007, na siyo miaka ya 1960's au 1970's na hata 1980's. Na wajue maisha ni magumu duniani pote. Hata hapa USA kama huna full scholarship utafanya kazi mbili tatu, huko unasoma ili kuweza kumudu fees. Wenye wazazi wanaoweza kuwalipia 'full' ni wachache sana ukilinganisha na idadi ya wanafunzi. Wanafunzi wengi wanasoma kwa mchanganyo wa mikopo, grants, scholarships na kazi.

Na kumbuka enzi zile wengi walipelekwa Eastern bloc, yaani Urusi, Poland, Bulgaria, East Germany, Yugoslavia etc. kusoma bure lakini hakuna tena. Dunia umebadilika.

REMEMBER LIFE IS NOT EASY.

18 comments:

Anonymous said...

Chemi: Hizo kazi za kufanya wanafunzi wa Bongo(ili wajilipie ada), watazipata wapi wakati hata wahitimu kadhaa hapo hapo Bongo bado hawana ajira?

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 4:39PM, umeuliza swali nzuri sana. Ni kweli kazi ni shida kupata Bongo.

Naomba watu wachangie maoni kuhusu hiyo swala.

KakaTrio said...

Da Chemi,
Hakuna mahala ambapo kuna kazi za kumwaga, hata wale walio soma nje wanalijua hilo. Wanasoma by day na kufanya kazi za ajabu ajabu by nite.

Tumefanya kazi za kubeba mabox, kazi za kuosha vibibi, kazi za kuanmgalila taahira, kazi za kuosha vyomba nk ili mradi hela ya rent na shule ipatikane.

Hawa vijana wakiwa creative wanaweza kufanya kazi, hakuna kazi itayoenda kuwatafuta, hakuna! itabidi wao ndio wazitafute kazi. Nitatoa mifano ya kazi wanazoweza kuzifanya.

1) Wanaweza kuanzisha migahwa ya chakula ya kwao wenyewe. Kama watu wanasoma masomo ya biashara ni kwanini wasianze kupractice? Akina mama ntilie wanatengeza hela ya kutosha wao wanawaangalia tu kazi kugoma kila kukicha.

2) pia wanaweza kufanya kazi kama baa tenda. Inasound vibaya mwanafunzi kuw abaa medi lakini kazi ni kazi.

3) wanaweza kufanya kazi za ukarani na utalishi. Makampuni kibao yanahitaji watu wanaoongea inglish sasa wao si ni wasomi bana kwanini wasichukue kazi izo?

TATIZO
Tatizo nilionalo mimi ni Scheduling, jinsi vyuo vya kwetu vinavyopanga ratiba ni vigumu sana kwa mtu kufanya kazi na kusoma. manake utakuta masomo ni kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa 12 jioni.

Ni nini cha kufanya?
Mimi naona Chuo kiamriwe na serikali au owner wake ili kiwe na flexible ya scheduling ya ratiba ya madarsa.

La pili ni lazima masomo yapewe credit ili wanafuinzi wachukue lodi wanayoweza na kwa gharama wanayoweza kuimudu. Na

La tatu ni vyema chuo kikaanzisha Payment plan ya namna fulani ivi. Yaani hata kama unadaiwa laki nane ni vyema wakuruhusu kuendelea na shule huku ukilipa leo shiling elfu kumi kesho laki cha msingi by the ende of the semester wanafunzi wawe wamelipa hela yote.

Anonymous said...

wanafunzi waliomaliza form six wako wengi tu mitaani wanafundisha tuition na wanajipatia kipato.wapo pia wanafunzi wa mlimani wanaofanya kazi(kaka yangu ni mfano).tatizo la migomo pale shuleni lina usugu wake na tatizo hapa sio ada.embu tujiulize,je kuna mwanafunzi alifukuzwa shule kwa sababu hajalipa ada?alichokisema maricha juu ya payment plan ndio kilichokuwa mlimani.wale wanaodaiwa waliachiwa kuendelea kusoma na hawakupewa hata deadline ya kulipa hizo pesa.sasa kulikuwa na haja gani ya kugoma.kila mwaka pale mlimani wananfunzi wanatafuta sababu ya watu kugoma tangu miaka ya 70.sasa wamefanya tatizo liwe gumu wamelazimika kulipa deni kabla hawajarudishwa shule,deni ambalo lingeweza kusubiri hata miaka kadhaa ikapita!chuo chenyewe kina ajira ambazo wanafunzi wengeweza kuomba zitengwe kwa ajili yao.kazi kama kumwagilia maua,kulinda geti,part time driver,versity hospital paramedic,kupaka rangi,kufuata na kupeleka barua posta,kufua nguo na kupiga pasi,kusafisha viatu zingeweza kusaidia kuongeza kipato cha wanafunzi na kujenga utamaduni ya kujitegemea miaka mingi iliyopita.hata hivyo bado hatujachelewa tunaweza kuanzisha tamaduni hizi sasa.kugoma kwa nchi inayoendelea sio mtindo mzuri,kila sekta inapwaya na kwa mtindo huu inamaanisha kila sekta itakuwa inagoma na badala ya kufikiria maendeleo tunakaa kutatua migomo.halafu wanafunzi wa mlimani ni vyema watoe mawazo ya jinsi wanavyodhani pesa ya kuwasomesha itakavyopatika kuliko kung'ang'ania tu wapewe pesa ambayo wanaonyesha hata hawataki kujiuliza inatoka wapi.pesa wanayotaka kwa asilimia kubwa inakuja kama misaada na mikopo toka nchi za nje,iwapo tutaendelea kutegemea misaada na mikopo vizazi vijavyo vitageuzwa watumwa kwa madeni tuliyowaachia.tuamshane sisi kwa sisi,watu wa nje wanafurahi jinsi tunavyozidi kulala.kwa nini watanzania tuna moyo wa juu kuchangia harusi lakini swala la shule tunaliacha kila mtu kivyake?tungesaidiana pia katika ada za elimu tatizo hili la chuo kikuu lingepungua kwa kiasi kikubwa.zemarcopolo

Anonymous said...

Hili suala la kugoma kila mara tena kwa sababu zisizo na mantiki tumechoshwa nalo kabisa. Watu wenye matatizo Tanzania ni wengi tu, sio wanafunzi peke yao. Pesa zinazotolewa za huduma za jamii zinapaswa ziwafaidishe wote, si wanafunzi peke yao. Kwa nini wang'ang'anie 100% sponsorship bila kuwafikiria watanzania wengine wanaohitaji fedha hizohizo? Mbona wagonjwa mahospitalini wanachangia gharama za huduma za afya, wao nani atawasaidia kugoma ili watibiwe bure 100%? Kuna matatizo ya njaa, barabara, nishati, makazi, usalama, n.k, yote yanahitaji fedha. Mbona hawa vijana wanakosa uzalendo? Na hata hivyo serikali ilikwisha waahidi wawe na subira, hatua zinapangwa kuboresha hali iliyopo.

Kwa maoni yangu, vijana hawa wamekosa hekima na tena hawana adabu. Huwezi kumlazimisha anayekukopesha akukopeshe hela yote unayohitaji. Kopa kiasi kwake, nyingine jazia kutoka kwa mkopeshaji mwingine au kutoka vyanzo vyako vingine vya mapato. Na la zaidi, ni ukosefu wa nidhamu uliokithiri kumpa Rais wa Nchi ultimatum, ati atoe majibu ndani ya siku mbili! Wewe ni nani? Rais wetu yuko kushughulikia matatizo ya wanafunzi tu? Au hilo lilikuwa na dharura gani hadi likashindikana kusubiri?

Huu ni ulevi wa madaraka ya kitoto, mtu anachaguliwa kuwa rais wa wanafunzi, nafasi ya mwaka 1 tu, basi anajiona naye ni Rais kama Mh Kikwete, anaweza kumtishia hata Rais wa Nchi! Anampa ultimatum! Uchuro kabisa huu! Rais wa wanafunzi ni mwanafunzi, na urais huo unakoma anapokoma uanafunzi. Waelewe hivyo. Waache kuyumbishana wanafunzi kwa kutumia vyeo feki hivyo na kudanganyana ati "solidarity", hakuna solidarity hapo wakati huna cheti! Subiri upate cheti (degree) ndipo utaweza kumsumbua mwajiri wako kwa masharti kwa sababu atakuwa anahitaji utaalam wako. Sasa hivi huna utaalamu wowote unabwabwaja ati "solidarity"! Utaula wa chuya kwa uvivu wa kuchagua!

Nashauri UDSM wachambue vizuri wale waliosababisha fracas hii wapewe adhabu ya kukomesha kabisa. Wakomolewe kabisa hao, wala siwatetei ng'o! Uongozi uwe tu makini wasije wakaumiza wale wasio na hatia.

Kuhusu haya masharti mapya mie naona safi sana, kwanza wameyataka wenyewe hao wanafunzi. Nasema University ikaze uzi, masharti ndio hayo, naunga mkono kabisa na naomba serikali isimamie hilo. Hakuna jipya hapo, kwani hata wagonjwa hospitalini wanalipia gharama, sembuse hao wazima kabisa! Walipe hizo hela. Kama kweli yupo asiyeweza kulipa, abaki kwanza nyumbani tuone wangapi wanaweza tuendelee nao kwa kipindi hiki, tena itasaidia kupunguza fujo. Hao watakaoshindwa kabisa watafutiwe mpango wa kuwasaidia (mfano kama kampeni za michango mbalimbali n.k) na fedha zikishapatikana ndipo waitwe chuoni. Hata watoto wanaopelekwa kutibiwa India, ni fedha zinachangwa kwanza zikishatosha ndipo wanapelekwa. Tufanye hivyo kwenye elimu pia. Pesa mbele, hakuna huduma inayoweza kupatikana bila fedha.

Nasema tu poleni sana lakini mmevuna mlichopanda.

MTANZANIA. said...

Chemi! Asante kwa kunikaribisha ktk mjadala huu.

Yawezekana kabisa kusoma na kufanya kazi.Tofauti na maoni ya wengi, mimi naona kazi zipo kama mtu atahitaji kufanya kazi. Isipokuwa tatizo ni uchaguzi wa kazi miongoni mwetu Watz.

"Kabisa mimi second year nikauze chakula cafteria?" Aka unikome! Hiyo ni kauli ya kawaida kabisa toka kwetu wanafunzi wa elimu ya juu. Lakini ni mfumo mbaya uliojengwa na wakoloni. Nilibahatika kutembelea baadhi ya vyuo, wanafunzi wa M.A na Phd wanafanya kazi za ufagizi na kudeki bila kinyongo. Hili kwa TZ ni gumu? Cha msingi tuamke kwanza na ndipo milango ya kazi itaonekana. Ila kama kila mtu akitaka kiti cha kuzunguka basi patakuwa hapatoshi.

Asante.

Anonymous said...

Jamani watu muache kuongea kama hamjui Tanzania ikoje, niambie ni wapi utapata hizo kazi za part time?, ni vibibi vya wapi utakwenda kuviosha?, vyombo vya nani utaosha kwa mshahara upi?, house girls anaosha vyombo , anapika, nk. analipwa elfu 10 kwa mwezi, utakusanya hizo elfu kumi kwa miezi mingapi upate hela ya kulipa fees.
Nashangaa sana watu mnaongea kama vile hamijui nchi yetu, pesa unayolipwa huko kubeba mabox kwa siku 5 huku ni mshahara wa graduate aliyeajiriwa mwezi mzima. haya niambie hao wanafunzi mnaowashauri wafanye kazi part time? si watafanya miaka 100, ili wapate hela ya kutosha ada???.
Kufanya kazi yaweza kuwa suluhisho lkn si la kutegemewa, nafikiri ni kwamba Bodi ya mikopo iainishe ni kina nani wanastahili kupata 100% na kina nani wana ka-uwezo ka kujilipia hiyo 40% iliyobaki wapewe 60%.
Kuna watu nina uhakika pesa wanayopewa chuoni ni kwa ajili ya anasa tu, nikiwa na maana kwamba mzazi anamgharamia kila kitu japo anapewa nyingine na chuo, na kuna mwingine hiyo hiyo ndio atunze familia na kusomesha wadogo. Ushauri wangu ni kwamba waangalie nani anapaswa kupewa 100% na nai 60% na wengine hata 40% sawa tu.
Mama Ushauri

Anonymous said...

HIKI KIUNGANISHI NI CHA KISIASA ZAIDI.

HIVI MTU UNAWEZA KWELI KUSEMA HAPA TANZANIA KUNA AJIRA YA MUDA KWA SIKU!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

MWENYEENZI MUNGU AMETUPA MIDOMO WOTE, AKATUPA UFAHAMU, BUSARA NA HEKIMA. NADHANI SI BUSARA KUONGEA AU KUANDIKA ILIMRADI TU. YAANI KWA KUWA UNAFAHAMU KUANDIKA BASI WEWE UNAANDIKA TU, HAPANA.

NAWAULIZA,

HEBU FANYENI UTAFITI AMA KWA KUSIKILIZA VYOMBO VYA HABARI AU NYIE WENYE FEDHA NENDENI VIJIJINI MTAFITI KIPATO CHA WADANGANYIKA WA HUKO.

UNAPOKUWA UMEKWISHAVUKA JARIBU KUWA NA BUSARA, HUENDA BABA ZENU NDIYO HAO WANAINGIA MIKATABA YA RICH, RAD.. nk. HAWA HATA KAMA KUWASOMESHA WAJOMBA ZAO, SI SHIDA

5 5 5

Anonymous said...

AU FANYENI UTAFITI NI KIASI GANI HAWA VIJANA WANACHOIOMBA SERIKALI YAO IWAONGEZE.

SIDHANI KAMA KINAVUKA KILE KIWANGO CHA KMJ KWA MKOA MMOJA!!!!

NA SASA HAWAPO CHUONI HIZO MILLION 100 KILA SIKU, KWA MUDA WATAKAOKUWA NJE ZITAPONA KWELI!!!

HEBU VIONGOZI WA NCHII HII JITOENI MUHANGA MUIJALI ELIMU HASA YA JUU ILI NCHII HII ANGALAU IPIGE HATUA KWA KASI.

HIZI TAARIFA ZA "MAFUTA TAYARI"
MWAMBAO MWA TANZANIA, NI NANI ATAKUJA KUFANYA KAZI KATIKA MAKAMPUNI HAYO???

MNATAKA TANZANIA IJE KUWA KAMA JIMBO LA OGONI!!!!! MSIJENGE MATABAKA TAFADHALINI.

WIVU UBINAFSI NI MBAYA SANA.

Anonymous said...

Serikali inao uwezo wa kulipia hiyo asilimia 100!!! Msiwatese watoto wa walala hoi...
Hiyo hela ya tume ya kukusanya maoni ya ku-fast-track shirikisho ndio ziende huko kwa wanafunzi kwani nani anataka hilo shirikisho... Yaani rais anaunda tume kuuliza uharakishwaji wa shirikisho (kwani nani alimwambia Kikwete kuwa tunalitaka shirikisho?) Serikali iache kuharibu pesa za umma, badala yake iwekeze ktk vijana - elimu!!!

Anonymous said...

Chemi,
nilikuwa nasubiri uweke hii mada nyeti-ahsante sana.
1) kuhusu 100% au 60% ya mkopo-mie naungana na mdau hapo juu kuwa kuna wengine wanastahili kupewa 100%, wakati wengine hawastahili. Serikali inabidi ifanye busara ya kuchanganua makundi ya wanaostahili na wasiotahili.
3)(Nasikia-sina data)kuwa wanafunzi walihaidiwa 100%-kama ni kweli-ahadi ni deni.
2) kuhusu kufanya kazi ili kuongeza kipato-hii jamani sio kitu rahisi dunia nzima sio Tanzania tu. Hata huku ulaya sio rahisi, kulingana na ratiba za masomo-hasa ya undergraduate. Ndio maana vijana wengi wanaokuja huku kusoma degree ya kwanza wanachukua miaka hata kumi, na wengine hata hawamalizi shule. Ingekuwa ni rahisi kama wadau wanavyoongelea hapo juu, vijana wengi wangemaliza hizo shule basi.
3)nafikiri vingeundwa vyombo vya usuluhishi-arbitration-badala ya kutumia migomo kama chombo cha kutatua matatizo. Migomo inaathiri wale anaojilipia.

4) ni kweli maisha yanabadilika, na vijana wa chuo wameshaelewa hilo-sijasikia kuwa wanaomba kupewa pesa ya bure-bali wanaomba MKOPO. kwa wale tuliosoma zamani inabidi tuwape 'credit' hawa vijana kwa kuyakubali haya mabadiliko -FROM FREE EDUCATION TO LOANS!

Chemi Che-Mponda said...

Nami na kubaliana na kithuku. Hao wanafunzi walioanzisha huo mgomo wachukuliwe hatua kali.

Nimesikitika sana kusikia kuwa kulikuwa na makundi ya wanafunzi waliotishia eti kupiga maprofessa na wanafunzi darasani. Walioshiriki kwenye hayo makundi nao wachukuliwe hatua kali.

Na ni kweli kama wewe ni denti ni denti hata kama ni kiogozi wa madenti. Mambo ya kutishia serikali ya nchi hayafai kabisa.

Anonymous said...

hawa wanafunzi nĂ­ wabinafsi sana.mikopo inatolewa kwa wanafunza wavulana wenye division one tu na wasichana wenye division one na two,ni kwa nini wasiombe mikopo hiyo wapewe hata kwa asilimia fulani pia wale wasiopata grades hizo ambao wamepata admission ya chuo kikuu.badala yake wao wanaomba kuongezewa.naelewa kuwa ni vigumu kwa baadhi ya watanzania kumudu gharama hizo za chuo lakini huu mgomo umekaa kibinafsibinafsi sana,ndio maana SUA wanafunzi wa mwaka wa mwisho wamekataa kugoma wanataka kumaliza shule waingie zao mtaani.mwaka 90 wanafunzi wa chuo hichohicho waligoma ingawa walilipiwa asilimia 100 kwa madai kuwa pesa ya chakula waliyopewa na serikali ni ndogo.hii ne trend pale chuoni wanafunzi ni lazima kila mwaka wawe na sababu ya kugoma!zemarcopolo

Anonymous said...

Chemi,
samahani sana kwa nitakayosema. Lakini wakati mwingine wewe ni mkurupukaji wala hutafakari kwa kina unachotaka kusema. Mambo ya delinyuzi bado unayo sana. Inaonyesha huijui UDSM.
Kwanza tu JKT ilikuwa ni baada ya form six au vyuo vingine kabla ya chuo kikuu. Kudai ilikuwa ni kulipia kwa kusomeshwa ni kutunga lengo lako mwenyewe. Kama ni hivyo kwa nini pia walienda wale waliosomea shule za kulipia?
Wewe sijui uko Marekani gani, Financial loan unaifahamu? Si kweli kwamba watu wote wanajaisomesha wengine wanachukua hizo loans.
555 asante sana watu wanadai wanafunzi wafanye kazi hivi ubaa tender wa kulipwa 10000 kwa mwezi ndio tuseme utawafanya watu walipe ada?

Anonymous said...

YAANI HIVI MNAJUA KIMA CHA CHINI CHA MTANZANIA? NI 60,000 HAYA ALIPE SASA ADA YA MWANAE.
KAMA SI KUKUZA RUSHWA NINI????

Chemi Che-Mponda said...

meja, asante sana kwa mchango wako nashukuru. Na wengine wote asanteni pia.

Mimi nimeweka maoni yangu hapa ili watu wachangie, na nataka kusikia kutoka pande zote.

Kuhusu swala la JKT, naona ni nyeti kidogo, maana uisema watu waende baada ya Form 6 ni kama vile kuna Break katika masomo yao. Na ukisema waende baad ya kumaliza UDSM, wengine watu kimbia nchi. Na kama wata lazima misha watu kwenda kama zamani, itakuwa balaa.

Nina ndugu yangu alizamishwa kuacha mume na watoto wanne nyumbani ili aende JKT. Na walimwambia, "ukipata mimba nyingine tutapasua hilo tumbo!" DUH!

Anonymous said...

WAZO LA HAO WANAOTAKA WANAFUNZI WALIPE ASILIMIA 40 JE WENYEWE WALILIPA HIZO NA WAMELIPA HUO MKOPO? SITAKI KUSIKIA MTU ANASEMA TANZANIA HAINA PESA, KODI TUNAYOKATWA WAFANYAKAZI NI KUBWA MNO KWA NINI WATU WASIKOPESHWE? KWA NINI WANATHAMINI KUNUNUA GARI LA MAMILIONI YA PESA ETI LA MKE WA WAZIRI MKUU!? KAMA SIO KUTUONA SIE NI MAKUKU NINI? WATANZANIA MNAPIGA VIGELEGELE KIKWETE! KIKWETE! AMEFANYA NINI CHA MAANA ZAIDI YA USWAHILI NA UONGO KWA JAMII! MTU GANI ASIYE ONA WATENDAJI WANAKOSEA AKAINGILIA KATI?
WATU WANAINGIA MIKATABA FEKI WANAPOTEZA HELA ZA UMMA, HAKUNA HATUA WANAYOCHUKULIWA! JE HAYO MABILIONI YANAYOPOTE KWENYE MIKATABA YENYE MASLAHI YAO? UNAWEZA KULINGANISHA NA VIJISENTI AMBAVYO WANAFUNZI WANAHITAJI TENA NI KWA MKOPO?
VIJANA MUELEWE KWAMBA HAWA JAMAA WANATAKA WATU WAJINGA ILI WAENDELEE KUWA TAWALA NA WATOTO WAO WAJE WAWATAWALE, SERA KUBWA NI HIYO KWAMBA KUWEPO NA TAIFA LA WAJINGA ILI WAENDELEE KUTUTAWALA NA HATIMAYE WATOTO WAO WAJE WATUTAWALE.
WATANZANIA ACHENI MAMBO YA KUSHABIKIA VITU BILA KUCHUNGUZA! WE UNAMSHANGILIA MTU ANAYEKUTESA! HIVI UNA AKILI KWELI? MTOTO WAKO AMEJITAHIDI KUSOMA HADI HAPO ALIPOFIKIA BADO ANATAKA KUNYIMWA KITUAMBACHO NI HAKI YAKE, ETI BABA, MAMA UNADIRIKI KUSIFIA UONGOZI MZURI!
ANGALIENI NCHI ZINGINE KWA NINI HAKUNA AMANI!? NA KWETU BADO KIDOGO VURUGU ZINAKUJA,MAANA TUNAWANYIMA HAKI YAO WALE WENYE NGUVU,IKIFIKA WAKATAKA HAKI YAO KWA NGUVU UTAFANYA NINI WE WAZIRI,MBUNGE,RAISI UNAYE NYAMAZA KUONA WATU WANANYIMWA ELIMU.
WATU WANACHOKA JAMANI... MUWE WAELEWA SIKU ZOTE WAJINGA HAWAPENDI KUENDELEA KUWA WAJINGA WATATAFUTA KWA NINI WAO NI WAJINGA.
NJAA ITAWAUMA, WATAULIZA KWA NINI WENGINE HAWAUMWI NJAA!? JIBU WATAKALOPATA MTAKIONA! WATU TUKIOMBA HAKI KWA AMANI MNAJIFANYA HAMSIKII,TUKIANDAMANA OHH! HAWAJAMAA WANAFANYA VURUGU!
VIJANA SASA WAKATI WAKUNYANYASWA NAOMABA UISHE.. KAMA VIPI TUPAMBANE KUKFA NA KUPONA LA SIVYO TUTAKUWA VIBARAKA, MASIKINI WAKUTUPA TUSIO NA ELIMU,NA TUTAWANYENYEKEA WATOTO WAO WANAOSOMA KWA UDHAMINI WA SERIKALI NA SIO MKOPO KAMA TUNAVYOKOPESHWA SISI.
NASEMA HIVI KAMA KIJANA, JE KWANI RWANDA WALIPIGANA KWA NINI,BURIUNDI KWA NINI? SIO WAJINGA WALE!
JAMANI HUKU KWETU HAKI HAIJI BILA MAANDAMANO WALA MIGOMO!
SASA ILI WASIZOEE TUPIGANE NA VITA KABISA. BORA TUFE ILI VIZAZI VIJAVYO VIISHI MAISHA YA NIDHAMU NA KUTHAMINIANA.
SIO KAMA SASA ETI MTOTO WA RAISI SIJUI MBUNGE ANALETA DHARAU! WANACHUO ENDELEENI NA MGOMO, MSILEGEZE UZI,HAKUNA KUTOA ASILIMIA 40. KAMA NI MKOPO SI MTALIPA KWA NINI ISIWE ASILIMIA 100?
MBONA WAKE ZAO NA WATOTO WAO WANAFUJA MABILIONI YA SEREKALI?
HAKUNA SULUHU MPAKA MKOPO UWE ASILIMIA 100.

Anonymous said...

NAHISI HASIRA NA HUZUNI PIA.

Watanzania walio wengi ni mbumbumbu au hawafahamu kabisa kinacho endelea katika serikali yao na ndio maana ikiwadangaya hawana Namna ya kuhoji.

Wanaofahamu ukweli ni waoga kama mbwa koko wanafiata MIKIA yao mapema nakudai hawafaham kitu au ndio msimamo wa serikali.

Ni ambao hawakubali na kuhoji sana ufanyiwa mbinu za kijinga na kubambikizwa kesi kunyamazishwa.

Nataka mfahamu kuwa serikali ina uwezo kamilifu wakulipa hizo ADA bila hata mkopo,ila hao walio kalia maamuzi hayo yani VIONGOZI WAKUU wanafikiria je watanufaika vipi na malipo hayo.

Nadhani hamjaelewa....kila fungu la fedha linapo idhinshwa kutoka lazima liwe na panga fulani kwenda kwa waheshimiwa fulani sasa bado ina angaliwa kama itafaa..kama ni ngumu basi ujue haitowezekana kwa urahisi kupata huo mkopo wa asilimia 100%.

Serikali serikali hii ina uwezo ambao ukiambiwa huta amini.Angalia jinsi gani viongozi wake wanavyo ingia mikataba na manunuzi feki sana ya MADINI,RADA,NDEGE YA RAIS,UMEME NA MINGINEYO.

AMBAYO ETI HATURUHUSIWI KUIJUA!!! NDIO UJUE KUWA WIZI,RUSHWA NA KILA AINA YA UFISADI UNA FANYWA NA VIONGOZI WETU,THEN WAKIWA WANAFAHAMU VIZURI WANASIMAMA NA KUPANDIKIZA UONGO NDANI YA VICHWA VYA WATANZNIA KUWA ETI SERIKALI NI MASIKINI.....WAONGO WAKUBWA HAOOO.

WASHINDWE KABISA NA LAAANA ZAO WANAZO TUOMBEA WAKATI NI MARA NYINGI TU UTASIKIA KAULI ZA DHARAU KUTOKA KWA BAADHI YA MAWAZIRI WALIO WEZI WAKUBWA KUWA:

NDEGE ITANUNULIWA..HATA KAMA MAJANI MTAKULA,MAWAZIRI LAZIMA WAPANDE MAGARI YENYE HADHI YAO...na nyingine nyingi tu za kuuza nchi msisahahu ile kubwa kabisa ya mheshimiwa mkapa:NET GROUP ITAFANYA KAZI KWA NGUVU na MAKABURU WAACHE WAJE NINAWATAKA HAPA TZ.
Matokeo yake mmeyaona sina haja kusimulia.

MWAJUA HIZO FEDHA NI KIASI GANI ZIMEPOTEA???HALAFU NCHI NI MASIKINI!!!!!!!???

Hivi kweli inaingia akilini mwanaichi wa kipato cha chini(60,000 kwa mwezi)akaweza kulipa Ada kubwa kiasi hicho???
Hii si ndio dalili za kubariki WIZI na RUSHWA MAOFISINI????

Hata kama mshahara ungekuwa 120,000 kwa mwezi bado kabisa kuweza kulipia ada na kutunza familia.

NA HAPO sija zungumzia wale wakulima wakawaida yaani wanategemea mazao ya msimu,wakyapata tu vyama nya ushirika vina watia ndani.

MIMI SIKUBALIANI KABISA NA WANAOSEMA KUWA WANAFUNZI WAMEKOSEA KUGOMA.AHAHADI NI NYINGI MNO HAZI TEKELWEZWI.

HATUWEZI KUWA WAJINGA NA WANYONGE KILA SIKU...TUMECHOKA...KAMA SI KWA USTAARABU BASI KWA NGUVU KUPATA HAKI.

VIONGOZI WETU WAACHE LONGO LONGO WANAFUJA FEDHA MNOOO NA DHAHIRI TUNAJUA...WAVUMILIE WATU WANAPO DAI HAKI ZAO.


Sasa WANAPOTOSHA UMMA KWA KILA MBINU... WAJINGA SANA.

MARTIN...