Wednesday, April 18, 2007

Mauji Chuo Kikuu cha Virginia Tech


Sura ya Muaji Cho Seung-Hui

Poleni waKorea wote. Sasa asante Cho Seung-Hui, itakuwa vigumu wapate visa za kuja kusoma Marekani bila kuchambuliwa kila kitu toka walichofanya toka wazaliwe mpaka wanakunya saa ngapi.

WaMarekani waoga sana na wabaguzi sana na sasa wamepata kisingizio cha kunyanyasa waKorea wote Marekani. Msisahau kabla ya 9/11 jinsi waarabu walivyokuwa wanathaminiwa Marekani shauri ya pesa zao.

Kama hamjasikia, vituko na visa vya kijana, Cho Seung-Hui, mwenye miaka 23, na mwanafunzi aliyekuwa anasoma Chuo Kikuu cha Virginia Tech nitawasimulia kwa ufupi. Siku ya jumatatu akili zilimruka na aliua wanafunzi na walimu wa chuoni hapo. Watu 32, walioamka na kufanya shughuli zao kama kawaida siku hiyo walipoteza maisha yao.

Cha ajabu, watu walijua kuwa huyo jamaa ni mwendawazimu siku nyingi. Hata mwalimu wake alienda polisi kumshitaki kuwa ana wasiwasi naye. Lakini polisi hawakufanya kitu.
Na wote tunajua mweusi angekuwa na vituko kama vyake, angefukuzwa shule zamani. Cho alikuwa anadika michezo ya kuigiza na mashairi zenye plots za kutisha kama kubaka, kuua, na kujiua.

Nani asiyejue kuwa waMarekani wanasema kuwa hao wenye asili ya Asia wana akili sana. Na si ajabu ndo maana huyo Bwana John Markell, alimwuzia bastola bila maswali mengi. Alisema, “he looked like a clean cut College student”, yaani alionekana hana matatizo. Je, kijana mweusi anayesoma Chuo Kikuu angeweza kununua bastola kwenye duka lake kwa urahisi hivyo? Na leo asubuhi nilikuwa nabishana na bosi wangu kuhusu hiyo swala, nikamwambia, huyo Markell asingeniuzia mimi mwanamke mweusi hiyo bastola, lazima angetafuta kisingizio cha kutokuniuzia maana sionekani kama clean cut college student au clean cut period.

Kati ya hao waliouliwa siku ya jumatatu kulikuwa na weusi kadhaa. Mmoja ni Ryan Clark, aliyekuwa na akili sana na kusoma Major tatu (haya nyie wazungu mnaosema kuwa weusi hawana akili). http://www.wrdw.com/news/headlines/7071667.html

Na jambo lingine kinachoniudhi. Wansema kuwa haya ndo mauaji makuu yaliyowahi kutokea nchini Marekani. Wamekosea, au wansema hivyo kwa vile weusi siyo watu kwao. Miaka ya nyuma huko Florida (1923) walikuwa mamia ya weusi, na mauaji ya weusi yalitokea Arkansas (1919) na Oklahoma (1921) pia.

Karibuni mtoe maoni yenu.

3 comments:

Anonymous said...

Hapo mafunzo yako mengi tu. Maonyo yanayotolewa juu ya watu waliorukwa na akili miongoni mwetu yanapaswa kuchukuliwa uzito unaostahili. Na prejudice ni mbaya. Wazungu wanadhani ama wanaamini mkorea ama mtu mwingine mweupe hana madhara hata kama kuna shaka. Ndio maana hawakudhani kama huyo mkorea angefanya mauaji hayo, wakapuuzia taarifa za awali. Angekuwa mweusi (au hata mwarabu siku hizi) kweli angeshahamishwa siku nyingi. Nasikitika kuna watu wamekufa, lakini hao jamaa huko wazichukulie tahadhari kwa makini.

Anonymous said...

Mie nafikiri tuache kuangalia kila tukio kwa kurunzi la uzungu (white) au uafrika (black). Kwa maneno mengine, kama mtu utaishi kwa kufikiria kuwa kila kinachofanyika ni ubaguzi wa rangi (racism), basi unaishia kuwa 'sensitive' na wakati mwingine unashindwa kuyakabili matatizo yanayokusiba na kuishia kulaumu ubaguzi wa rangi.

Mawazo yangu juu ya hili tukio la Mauuaji ya wanafunzi ni haya
1) umilikaji/ununuzi wa bunduki Marekani ni rahisi sana-watu wananunua bunduki kama peremende. 2)matatizo haya yataendelea kama utamaduni wa vurugu (violence) na bunduki-utakuwepo kama sehemu ya burudani (entartainment)-kwenye sinema, au video games. Sinema isiyo na bunduki sio za kawaida siku hizi!!
3)kwa sababu biashara ya bunduki ni kubwa, sidhani kama itapitishwa sheria ya kudhibiti bunduki kirahisi. Bwana Cho alinunua bunduki yake kwa shilling (dollar) 560)!!!!
4)wengine wamelaumu vyombo vya habari-mfano kusisitiza kuwa haya ni mauaji makubwa kuliko yote-inaleta ushawishi kwa vijana kutaka kuvunja hiyo rekodi!

Ahsante Chemi kwa kuleta mada mbalimbali.

Anonymous said...

Haya ni mauaji makubwa kwa kuangalia mauaji ya aina hiyo, nadhani hapo Chemi umekwenda kushoto. Haijawahi kutokea mauaji ya shuleni au kazini ya mtu kucharuka na kuwatwanga risasi wenzake kiasi hiki. Hii ni sahihi lakini ukianza kuangalia mauaji bila kuainisha, basi ni kweli haya si makubwa. Wamarekani waliandaa vifo hivi wenyewe kutokana na ujinga wao wa kuruhusu silaha, pia utamaduni wao wa individualism na ubaguzi dhidi ya wageni. Huyu kijana alizidi kutaniwa kutokana na upungufu wake wa uwezo wa kuongea. Aidha, tabia ya walimu kumfukuza, kumlazimisha aende kwenye ushauri nasaha, kumsusia, ilimfanya ajione upweke, nusu mtu na anayedharauliwa. Mwalimu hapaswi kumlazimisha mtoto aende kushauriwa, kwa kuwa atajisikia vibaya. Mtu anayeshauriwa tayari ana matatizo sasa ukimsukumia huko unaharibu zaidi.

Kati ya mwaka 1996 na mwaka huu, duniani kote mauaji ya mashuleni yameshatokea mara 55, ambapo kati ya hizo mara 41 ni Marekani. Huu siyo unywanywa kweli?

Pia ni kweli alipata silaha kirahisi kwa sababu ni Muasia, angekuwa Mwarabu au Mswahili isingeenda kilaini hivyo.

Ukiamua kuishi kwa bunduki utakufa kwa bunduki, na huu ndio urithi wa Wamarekani.