Monday, April 23, 2007

Maoni ya Wasomaji kuhusu Mgomo wa wanafunzi UDSM

Expelled UDSM students - pic from Michuzi blog

Nimeamua kubandika maoni machache niliopata kwenye blogu kuhusu mgomo wa wanafunzi wa UDSM. Karibuni mtoe maoni yenu.
Na sasa kuna habari kuwa wanalegeza masharti ya wanafunzi kurejea Chuoni. Kwa habari zaidi someni:
**********************************************************************************

Kithuku said...

Hili suala la kugoma kila mara tena kwa sababu zisizo na mantiki tumechoshwa nalo kabisa. Watu wenye matatizo Tanzania ni wengi tu, sio wanafunzi peke yao. Pesa zinazotolewa za huduma za jamii zinapaswa ziwafaidishe wote, si wanafunzi peke yao. Kwa nini wang'ang'anie 100% sponsorship bila kuwafikiria watanzania wengine wanaohitaji fedha hizohizo? Mbona wagonjwa mahospitalini wanachangia gharama za huduma za afya, wao nani atawasaidia kugoma ili watibiwe bure 100%? Kuna matatizo ya njaa, barabara, nishati, makazi, usalama, n.k, yote yanahitaji fedha. Mbona hawa vijana wanakosa uzalendo? Na hata hivyo serikali ilikwisha waahidi wawe na subira, hatua zinapangwa kuboresha hali iliyopo.

Kwa maoni yangu, vijana hawa wamekosa hekima na tena hawana adabu. Huwezi kumlazimisha anayekukopesha akukopeshe hela yote unayohitaji. Kopa kiasi kwake, nyingine jazia kutoka kwa mkopeshaji mwingine au kutoka vyanzo vyako vingine vya mapato. Na la zaidi, ni ukosefu wa nidhamu uliokithiri kumpa Rais wa Nchi ultimatum, ati atoe majibu ndani ya siku mbili! Wewe ni nani? Rais wetu yuko kushughulikia matatizo ya wanafunzi tu? Au hilo lilikuwa na dharura gani hadi likashindikana kusubiri?

Huu ni ulevi wa madaraka ya kitoto, mtu anachaguliwa kuwa rais wa wanafunzi, nafasi ya mwaka 1 tu, basi anajiona naye ni Rais kama Mh Kikwete, anaweza kumtishia hata Rais wa Nchi! Anampa ultimatum! Uchuro kabisa huu! Rais wa wanafunzi ni mwanafunzi, na urais huo unakoma anapokoma uanafunzi. Waelewe hivyo. Waache kuyumbishana wanafunzi kwa kutumia vyeo feki hivyo na kudanganyana ati "solidarity", hakuna solidarity hapo wakati huna cheti! Subiri upate cheti (degree) ndipo utaweza kumsumbua mwajiri wako kwa masharti kwa sababu atakuwa anahitaji utaalam wako. Sasa hivi huna utaalamu wowote unabwabwaja ati "solidarity"! Utaula wa chuya kwa uvivu wa kuchagua!

Nashauri UDSM wachambue vizuri wale waliosababisha fracas hii wapewe adhabu ya kukomesha kabisa. Wakomolewe kabisa hao, wala siwatetei ng'o! Uongozi uwe tu makini wasije wakaumiza wale wasio na hatia.

Kuhusu haya masharti mapya mie naona safi sana, kwanza wameyataka wenyewe hao wanafunzi. Nasema University ikaze uzi, masharti ndio hayo, naunga mkono kabisa na naomba serikali isimamie hilo. Hakuna jipya hapo, kwani hata wagonjwa hospitalini wanalipia gharama, sembuse hao wazima kabisa! Walipe hizo hela. Kama kweli yupo asiyeweza kulipa, abaki kwanza nyumbani tuone wangapi wanaweza tuendelee nao kwa kipindi hiki, tena itasaidia kupunguza fujo. Hao watakaoshindwa kabisa watafutiwe mpango wa kuwasaidia (mfano kama kampeni za michango mbalimbali n.k) na fedha zikishapatikana ndipo waitwe chuoni. Hata watoto wanaopelekwa kutibiwa India, ni fedha zinachangwa kwanza zikishatosha ndipo wanapelekwa. Tufanye hivyo kwenye elimu pia. Pesa mbele, hakuna huduma inayoweza kupatikana bila fedha.
Nasema tu poleni sana lakini mmevuna mlichopanda.
4:52 AM

*************************************************************************************
Maricha said...

Da Chemi,

Hakuna mahala ambapo kuna kazi za kumwaga, hata wale walio soma nje wanalijua hilo. Wanasoma by day na kufanya kazi za ajabu ajabu by nite.

Tumefanya kazi za kubeba mabox, kazi za kuosha vibibi, kazi za kuanmgalila taahira, kazi za kuosha vyomba nk ili mradi hela ya rent na shule ipatikane.

Hawa vijana wakiwa creative wanaweza kufanya kazi, hakuna kazi itayoenda kuwatafuta, hakuna! itabidi wao ndio wazitafute kazi. Nitatoa mifano ya kazi wanazoweza kuzifanya.

1) Wanaweza kuanzisha migahwa ya chakula ya kwao wenyewe. Kama watu wanasoma masomo ya biashara ni kwanini wasianze kupractice? Akina mama ntilie wanatengeza hela ya kutosha wao wanawaangalia tu kazi kugoma kila kukicha.

2) pia wanaweza kufanya kazi kama baa tenda. Inasound vibaya mwanafunzi kuw abaa medi lakini kazi ni kazi.

3) wanaweza kufanya kazi za ukarani na utalishi. Makampuni kibao yanahitaji watu wanaoongea inglish sasa wao si ni wasomi bana kwanini wasichukue kazi izo?

TATIZO
Tatizo nilionalo mimi ni Scheduling, jinsi vyuo vya kwetu vinavyopanga ratiba ni vigumu sana kwa mtu kufanya kazi na kusoma. manake utakuta masomo ni kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa 12 jioni.

Ni nini cha kufanya? Mimi naona Chuo kiamriwe na serikali au owner wake ili kiwe na flexible ya scheduling ya ratiba ya madarsa.

La pili ni lazima masomo yapewe credit ili wanafuinzi wachukue lodi wanayoweza na kwa gharama wanayoweza kuimudu.

NaLa tatu ni vyema chuo kikaanzisha Payment plan ya namna fulani ivi. Yaani hata kama unadaiwa laki nane ni vyema wakuruhusu kuendelea na shule huku ukilipa leo shiling elfu kumi kesho laki cha msingi by the end of the semester wanafunzi wawe wamelipa hela yote.
9:34 PM

13 comments:

Anonymous said...

hawa wanafunzi nĂ­ wabinafsi sana.mikopo inatolewa kwa wanafunza wavulana wenye division one tu na wasichana wenye division one na two,ni kwa nini wasiombe mikopo hiyo wapewe hata kwa asilimia fulani pia wale wasiopata grades hizo ambao wamepata admission ya chuo kikuu.badala yake wao wanaomba kuongezewa.naelewa kuwa ni vigumu kwa baadhi ya watanzania kumudu gharama hizo za chuo lakini huu mgomo umekaa kibinafsibinafsi sana,ndio maana SUA wanafunzi wa mwaka wa mwisho wamekataa kugoma wanataka kumaliza shule waingie zao mtaani.mwaka 90 wanafunzi wa chuo hichohicho waligoma ingawa walilipiwa asilimia 100 kwa madai kuwa pesa ya chakula waliyopewa na serikali ni ndogo.hii ne trend pale chuoni wanafunzi ni lazima kila mwaka wawe na sababu ya kugoma!zemarcopolo

Anonymous said...

Nafikiri wanafunzi wa vyuo vikuu wapo sahihi. Serikali inatumia hela nyingi sana kwa vitu ambavyo sio vya maana kama kununu mashangingi hata kwa wakuu wa wilaya wakati suzuki samuri tu zingewatosha. Hela zifanyiwe vitu vya maana kama elimu na huduma za afya.

Anonymous said...

Kama kweli wewe ni mwana-demokrasia naomba urudishe maoni yote uliyoondoa kuhusiana na huu mgomo!

Chemi Che-Mponda said...

Kwa anonymous wa 5:51am, wala sijua toa maoni yoyote kuhusiana na mgomo.

Yako kwenye blog niliyoandika kuhusiana na mgomo. Soma:

https://www2.blogger.com/comment.g?blogID=17229004&postID=2228567355941212162

Anonymous said...

Da Chemi,mimi simo kwani nimegundua wote waliochangia hapo hawakuwahi kusoma katika vyuo vya kwetu.Wanataka mageuzi makubwa ya ghafla wanashau kwamba migomo ndio njia pekee ambayo imekua ikitumiwa na wanafunzi katika vyuo vikuu tangu enzi kuibana serikali angalau kuboresha maslahi ya wanafunzi.Kama hujawa party ya wanafunzi wa vyuo Tanzania ni lazima utakua na mtazamo tofauti lakini sio kwa sisi ambao tumekwisha pigwa mabomu!!.

Anonymous said...

Mimi nina mawazo yanayo fanana na wanafunzi walalahoi hapo UDSM. Serikali iwape mkopo wa 40 asilimia,halafu 60% iliyobaki serikali ilipe bila kuwadai tena.. hapo kutakuwa na cost sharing ya kweli,sio kama ilivyo sasa serikali inazungumza uwongo kuhusu hilo.halafu huyu jamaaa anaye zungumza kuhusu mabox yake huko kwa wazungu sidhani kama ana zungumza kwa ufahamu kamili kuhusu hali ya watanzania walio wengi.kwanza maisha ya uzunguni unaweza kubeba mabox yako na ukaishi vizuri tu kutokana na hali ya kiuchumi ya mataifa ya magharibi au pengine japo nina mashaka sana na uzushi huu!! subutu hapa uone utakufa hata chupi huja nunua!!!sembuse ADA.

Pia kufanya kazi na kusoma hapa BONGO ni vigumu kutokana na mpangilio wa ratiba za vyuo vikuu hapa,ni asubui kwa jioni kama shule ya msingi,kazi utafanya saa ngapi???

Nashangaa sana baadhi ya wachangiaji wanatoa shutuma tu bila katafakari hali halisi ya wanafunzi wengi wa vyuo vikuu.

wengi wao walisha shindwa kulipa hata ADA za sekondari mpaka leo wana madeni.siku ya kuchukua cheti unamalizia ndio unapata cheti.suala la kugoma ndio njia muafaaaka kabisa bila hivyo hakuna kitu ni UBABAISHAJI TU NCHI HII.

ULIZA NI AHADI MARA NGAPI WAMEPEWA KUTATUA TATIZO LA ADA NA MKOPO WENYEWE.

AHADI ANATOA MWINGINE TAMKO LA MAREKEBISHO ANATATOA MWINGINE.

NDIO UJUE NCHI HII NI UZUSHI TU, LABDA WAKAATAE KUWA KILA MTU NA MATAMKO YAKE NA HAPO NDIO KICHEKESHO ZAIDI.

WATANZANIA WENGI TENA WENYE WATOTO VYUO VIKUU NI MASIKINI KABISA SIO TU VIJIJJINI HATA HUKU MIJINI.

HATA HAO VIONGOZI WENGI WAO WAMETOKA FAMILIA MASIKNI KABISA LAKINI WAMESHA SAHAU KABISA AMAWAJIFANYA HAWA ONI.

SINA HAJA YA KUWATAJA WANA JULIKANA
SANA TU.

Anonymous said...

namuunga mkono huyo anon wa 7:21

nyongeza:
1) kufanya kazi na kusoma sio rahisi-dunia nzima, hata nchi zilizoendelea wanafunzi wanachukua mikopo ya karo. na wale wenye ratiba ngumu kama wanaosomea udaktari wanachukua mikopo hata ya kula. Tofauti ni kuwa mikopo ya namna hii huwa inatolewa na Benki kwa kushirikiana na serikali.
Huyo anyeongelea maboksi analeta picha ambayo si ya ukweli-uliza ni vijana wangapi wanashindwa kumaliza shule huko Marekani, sababu ya kubeba mabox na kujisomesha??
2) Napinga swala la kuwaadhibu viongozi wa wanafunzi. Hapa unakuwa unuua viongozi wa kesho. Kuongoza wanafunzi ni kujitolea kwa hali ya juu, sasa ukiwafukuza chuo hawa vijana unakuwa umeuua generation. Vijana jasiri watakuwa wanaogopa kujitolea kuongoza. Kiongozi hatakiwi kuwa "YES MAN". Chuo Kikuu ndio sehemu ambayo viongozi wanaanza kuonekana na wanapata mazoezi ya uongozi kwa kutatua matatizo ya wanafunzi.

Anonymous said...

mlalahoi na anony wa 7:21 asante sana kwa maoni yenu yenye busara, siyo mtu anakurupuka tu eti wabebe maboksi. Huko majuu mnabeba maboksi kwa sababu watu wa huko hawataki kuyabeba. Kwetu watu wanataka kubeba maboksi lakini maboksi ya kubeba hakuna.

Anonymous said...

Da Chemi.
Mimi nadhani unyonge wa Watanzania ndiyo unaosababisha haya yote.Sishangai kuona mtu analaumu wanafunzi kwa kugoma na kuwafananisha na wagonjwa na wau wengine.Wagonjwa namna ya kugoma ningumu kwao.Lakini hawa wanafunzi mambo mengine wanayasoma shule ikiwemo hiyo migomo sasa wakianza kutekeleza hayo mnalaumu.
Wakati wa chama kimoja upinzani ulikuwa pale na walisaidia mabadiliko ya kisiasa nchini.Mbona waliwahi kugoma kupinga serikai ya Kambarage Wabunge wlipojiongezea misahara mwishoni mwa miaka ya 60?
AU NI WIVU TUNATAMANI SOTE TUWE WAJINGA.Mtu anasangaa Rais kupewa muda uliaka apewe nani,kwani Rais ni MUNGU.Amechaguliwa na watu kama huyo wa DARUSO tofauti ni madaraka na eneo la utawala.NADHANI TUAE UJINGA AU KAMA ATUNA CHA KUSEMA TUNYAMAZE.

Anonymous said...

Mimi nimesoma chuo kikuu cha DSM. Shahada mbili nimepatia hapo. Migomo hii ipo baadhi yenye msingi, lakini huu wa sasa hivi umesababishwa na akili za kitoto na kukosa subira na hekima. Kama kuna mtu anakuzuia kupata degree yako, huyo mgomee tu kwa kuwa hata usipogoma hiyo degree hutaipata. Lakini katika mgomo wa sasa wanafunzi wameendeshwa na mob tu za kijinga kujifanya wana msimamo na "rais" wao wa DARUSO. Kwa nini wasitulie wakaendelea kusoma wakati matatizo yao yanashughulikiwa, kulikuwa na dharura gani hadi kufikia kumpa Rais wa nchi ultimatum ya siku 2 ati awe ametoa tamko? Hapa ndipo kamwe sikubaliani nao. Matatizo wanayolalamikia yana msingi kweli, lakini mgomo haukuwa njia sahihi kwani muafaka ulikuwa haujakosekana. Na inatia kichefuchefu kuona ati wanafunzi wa chuo kikuu wanaandamana wamevaa kama vibaka wanapiga makelele ovyo na wamebeba mabango yaliyoandikwa kwa lugha za kihuni. Hii ni kudhalilisha na kushusha hadhi ya chuo kikuu. Enzi zetu hata zile daladala zinazopitia chuo kikuu abiria wengine wakipanda walikuwa wanajisikia kweli wako na wasomi, wamevaa vizuri (si nguo za bei mbaya, lakini angalau ni safi, wamechomekea, wako decent), ni watulivu na lugha zao ni murua, hata wale makonda walikuwa wanaona raha, hawapati usumbufu. Lakini majuzi nimeona kwenye TV maandamano ya hawa vijana wetu wa chuo kikuu sikuweza kutofautisha na kundi la vibaka wa Tandale! Sasa jamani hamuwezi kufikisha ujumbe kwa njia hiyo! Hamuwezi kusikilizwa kwa kuwatukana au kuwatishia viongozi wa nchi. Hebu jiulizeni wale waliogoma miaka ya nyuma kwa mtindo huo (mwaka 1990 walimtukana mzee Rukhsa matusi ya nguoni), wako wapi?

Vijana wetu wanapaswa kufikiri kabla ya kutenda.

Anonymous said...

Kithuku,
acha kujichanganya. Kama madai ni ya msingi unachopigia kelele ni nini? Kwanaza hukukutakiwa kuwe na ahadi, pesa zilitolewa bil 113/- sh Bodi ya mkopo ilipewa hizo. Wanafunzi wa elimu ya juu ni chini ya elfu tatu. Kama zikigawiwa kwa watu hawa wote ni karibia mil 3 kwa kila mwanafunzi. Hapa tunaona kuwa wote wangepata mkopo kwa asilimia mia moja. Zimekwenda wapi hizi pesa?
Halafu kusema ati kwenye maandamano walibeba mabango, maandamano gani unayooongelea wewe? Msijitungie mambo kuhalalisha hoja zenu. Katika sakata hili hakukuwa na maandamano.

KakaTrio said...

Anon wa 6:56 AM. Mimi nimesoma vyuo vya elimu ya juu nchini Tanzania. n a mfano wa mama ntilie nilioutoa ni wa kweli kabisa, kuna vijana kadhaaa walitumia ile hela tuliyokuwa tunapewa kwa ajili ya chakula na malazi kufungua mgahawa enzi hizo walikuwa wanapata kati ya elfu 20 na 30 net profit kwa mgahawa mmoja!

Ni lazima ukubali wanafunzi wengi wa tz hawako creative kutafuta hela, na wakizipata hata hizo za kupewa huishia kuzitumia vibaya tu, sio ajabu waliziita "buumu" wale waliotutangulia.

kitu kingine cha ajabu wengi wetu baada ya kumaliza chuo tuliparangana kutafuta kazi bila mafanikio, kilichonishangaza hakuna hata mmoja alikuwa akiongelea swala la kujiajiri. wasomi wachache sana nimewaona wakibendi backward na kufungua hata genge, bora wawe omba omba kuliko wafungue genge la aina yoyote.

je vijana wetu wana habari Kikwete analipia gharama zote za shule kwa wale wataosomea digirii za ualimu? au hio kauli ilikuwa kampeni tu?

Nilibahatika kusoma zile halfu kombi nikawa mwl, na izo hela za mshara wa ualimu zilinipiga tafu sana nikiwa chuo Tz. kama wadau wangine walivosema je hawa vijana hawawezi kufanya kazi ya ualimu kupunguza makali?

Unknown said...

Kama watu wasipo simama sasa hivi kutetea haki zao basi itakuwa sheria. Hakuna pahala palipoandikwa kwamba wanafunzi wa chuo kikuu watafanya cost sharing. Na hakuna taifa lolote wanafunzi wa nchi husika wakajisomesha kwa asilimia 100%, wanasiasa wa tanzania wengi wao ni waongo. Hasa hii serikali ya sasa maana kila mtu anatoa maamuzi yake binafsi bila kuwashirikisha wadau na wanafunzi wenyewe. Ktk serikali hii wamekusanyana washkaji watupu labda tulisoma wote, ndiyo maana ukitoa maamuzi yako cwezi kukupinga kwa sababu wewe ni mwenzangu au kwa sasa unaitwa mwana. Km mlikuwa zamani hamuwezi kuandika chochote kwenye mabango kwa sababu mlikuwa ktk monopartism na sasa na vyama vingi na demokrasia. Hivyo mtu yu huru kujieleza. Zamani mlikuwa mnazan chuo ni pahala pakuwa smart, kwa sasa si hivyo, nini umefuata na nini unajifunza hapa. Nyakati ndizo zinabadirisha watu, enzi ya raizon na bugaruu haipo tena, mshahara wa kima cha chini ni 80,000/- tena askari au mwalimu. Na watoto wa walimu ndo wengi chuo halafu mwalimu alipe laki 7 kwa mwaka, hii ni hatari kwa taifa hili changa. Si semi kuhusu matokeo ya mwaka huu ya form 6, yanaonyesha wazi kabisa yanawapunguza watu watakao lipiwa na serikali.