Wednesday, April 25, 2007

Konyagi


Hata Boston, tunakunywa Konyagi! Ni pombe ya aina ya pekee duniani na waTanzania tunaweza kujivunia kuwa na sisi tuna kikali chetu! Inatengenezwa na Tanzania Distillers.

Jana niliamua kustarehe kidogo na kikali. Huwa napenda wine, au bia baridi! Lakini jana nilipata hamu ya Konyagi! Nilivyoenda Bongo mwaka jana nilirudi na kachupa ya Konyagi. Siku moja moja nikitaka kukumbuka 'home' nakunyawaga. Konyagi ni pombe enye ladha ya pekee. Halafu ni clear kuliko hata maji ya kunywa ya hapa Marekani.

Nashangaa haijanywa kinywaji kikuu ng'ambo kama vodka, najua unaweza kununua Uingereza lakini bado sijauona kwenye maduka ya pombe hapa USA. (Wasomaji mnishahishe kama nimekosea) Je, watengenzaji wamefanya international marketing?

Konyagi inatengenezwa na mabibo. Mnakumbuka tulivyokuwa tunaharibu nguo zetu na juisi ya mabibo. Doh! Pale UDSM, kati ya Hall 3 na Hall 2, kuna orchard kubwa kweli ya mikorosho. Tulikuwa tunashinda huko tuna chuma maikorosho, una kula ile bibo enye juisi kibao na korosho unatupa kwenye mfuko. Mfuko ukijaa unachukua kipande cha bati, halafu unatengeneza moto juu! Tia hizo korosho, na kaa mbali maana moshi huo! Nyie korosho zile za kuchuma na kuchoma wenyewe ni tamu.

Basi niwape story. Mara yangu ya kwanza kunywa Konyagi nilikuwa JKT. CO (Commanding Officer) alikuja Officer's Mess na kunipa offa. Nilmshukuru lakini ilibidi nikatae maana nilikuwa sijaozea kunywa pombe.

OHOOO! Si jamaa kanipa amri sijui adhabu ninywe nusu glass straight mbele yake! Niliinywa kama sumu, baada ya hapo nikaenda bweneni kulala hadi asubuhi huko tumbo na kichwa kinaumwa!

Lakini Konyagi kwa kiasi si mbaya hasa ukichanganywa na soda. Msinywe sana maana inalewesha haraka!

Konyagi JUU!

22 comments:

Anonymous said...

lakini wewe si ni mama mchungaji?

Anonymous said...

Che mponda kumbe sio mbaya sana,hii picha yako ya recent.Uko sawa mama nani.

Anonymous said...

Chemi inabidi uingie gym maana huo mwili kiafya si safi. Zoezi la kitandani halitoshi mama.

Anonymous said...

Punguza ubaguzi basi. Kama unalalamika kuhusu ubaguzi jaribu kuwa mfano. Sipendi kila saa ukiwa unaelezea kitu basi lazima uweke aidha mweusi au mzungu kwenye mabano. Kuna vitu vingi kwenye maisha kuliko rangi ya ngozi yetu. Muda mwingine unaonekana mshamba kuanza kubagua kuhusu nani mzungu au mweusi. Fikiria ukute blog ya mzungu imeandikwa hivyo si utachukia. Bora utaje jina tu linatosha. Mara nyingi tunaweka tofauti zetu mbele yetu kiasi cha kufanya tusifurahie maisha..!!!

Anonymous said...

Da Chemi,
ahsante kwa ku-promoti kinywaji chetu cha Konyagi.
Je unakunywa kweli au umepiga picha tu??

Chemi Che-Mponda said...

Asanteni kwa waliotoa maoni.

Anonymous wa 10:04PM, jibu ni ndiyo.

Anonymous wa 11:04PM, picha hiyo ni kati ya picha nilizopiga nyumbani April 23, 2007.

Anonymous wa 11:47, usiwe na hofu napata mazoezi zaidi ya ile ya 'kitandani'.

Anonymous wa 6:08AM, kama unakaa USA unajua maisha ni white/black. Kama unatarajia kuja USA basi utegemea maisha yatakuwa hivyo black/white. Hapa wanaona rangi ya ngozi yako kwanza halafu ndo wanakuona mtu.

Mkereketwa, nashukuru. Ndio nilitaka ku-promote kinywaji chetu Konyagi, maana ni unique. Ila nilikuwa nimechanganya na 7-UP!

Anonymous said...

fagilia kinywaji chetu dad

MzeeMzima said...

Nikikumbuka maisha ya JKT nashindwa kuelewa jinsi ambavyo CO wa JKT alivyokupa wewe ofa ya konyagi. Mbona yalikuwa makubwa.

Chemi Che-Mponda said...

Kibri,

CO aliambiwa kuwa eti naringa sinywi pombe. Sasa ilikuwa kama show kwake. Si baada ya kunilazimsha kuinywa mbele yake na maafande wengine alinilazisha kusimama attention mbele yake kama dakika tano hivi halafu ndo kaniruhusu niende! LOH! Nilikuwa naona kizunguzungu. Acha tu, kule tulikuwa hatuna haki kabisa hasa kama wewe ni Kuruta/Service!

Hata hivyo nilizoea kuinywa Konyagi baada ya kutoka JKT! Siku hizi hapa USA ni kama vile kinywaji cha anasa kwangu.

GAME THEORY said...

sista vipi mambo?

by the way nilifikiri kuwa wewe ulisoma Al Haramain ...back in 90's

anyway

na mimi nina blog lakini tofauti kidogo...

http://burudani.wordpress.com/2007/04/26/13/

Anonymous said...

dada chemi ujue nakuonea huruma na hiyo mikonyagi?siku hizi ina rifti valee bado tunakuhitajI! alafu anonymous mmoja aliesema kumbe wewe sio mbaya ana maana gani?wabongo tabia mbaya kupenda kuwachambua watu wakati nyie hamjioni! Mungu hapendi. asanteni
-maaaa wa maglobuuu-

Anonymous said...

Nachosema sio basi na sisi ndo tukuze huo ubaguzi bali tuwe mfano wa kuudharau. Nakaa UK lakini sasa hivi wananiheshimu maana nimewaonyesha kuna zaidi ya rangi ndani ya mtu. Ukiendekeza sana unakuta unakosa vitu vingi sana kwenye maisha...

Anonymous said...

http://burudani.wordpress.com/
hiyo ndiyo correct address ya kule kwenye burudani

Anonymous said...

Chemi naomba simu yako

Anonymous said...

Mtumzima,
Pombe na Uzinzi huharibu akili njema dada Chemi. Sikutarajia mdada kama wewe uifagilie konyagi.Pia ulituambia kuwa u mama mchunagji. Si utumie nafasi yako na jukwaa lako hili kusaidia vijana kuacha pombe na maovu.
Naomba ukanushe kusema konyagi juu kwa kuwa ni sawa na kusema shetani juu

Anonymous said...

na mumeo anatumia konyagi, je washirika wa church yenu nao si watakuwa walevi?

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 3:08AM, nikisema "Konyagi Juu" naisifia kama kinywaji cha kiTanzania, na siyo kuwa ni pombe kali.

Na kama ningepiga picha nimelewa huko nimeanguka chini sijijui ndo ungekuwa na haki ya kusema kuwa napenda ulevi. Ukweli nakunywa siku moja moja. Na hiyo Konyagi ni anasa kwangu ndo maana inatoka siku maalum. Hakuna ubaya kukumbuka nyumbani.

Kuhusu waumini wa kanisa kuwa walevi, hiyo ni kati yao na Mungu. Lakini kanisani hatusemi nendeni mkanywe mipombe mkalewe.
Hata Bwana Yesu alikunywa Mvinyo. Kunywa pombe haijakatazwa ila kulewa ndo dhambi.

Anonymous said...

Unajua one of miujiza aliyofanya Bwana Yesu ni kubadilisha maji kuwa Mvinyo ili wanafunzi wake wa-Enjoy?
Do u kno imeandikwa kilevi si kwa wafalme pekee.....inaendelea kusisitiza MPE MASIKINI KILEO ASAHAU TABU ZAKE?
By. MBWAKACHOKA, BHAM UK

Anonymous said...

Dada chemi mi nakushauri uache kabisa kunywa konyagi na vileo kama mmeamua kufanya kazi ya Mungu.
Wale waliojitoa kwaajili ya kumtumikia MUNGU HAWAKUTAKIWA KUONJA KILEO,kidogo kidogo iko siku utalewa!! halafu itakuwa soo,aliyotengeneza Bwana ilikuwa kinywaji kisicho na kileo.Kama usingependa siku moja wanao waje kuwa wanywaji basi wewe maza wao acha kabisa, ndo kuwa mfano.Siku hizi watu husifiana kwa maovu.Utasikia duh jamaa anakunya huyo!, sorry anakunywa huyooo!!, kama vile ni sifa nzuri. Utumishi wa Bwana na pombe havichanganyiki chungu kimoja.
Upo hapo dada yangu mpenzi.Msalimie mumeo mwambie n yeye asome hii comment!

Anonymous said...

dada chemi, kwa kuwa umesema u mke wa mchungaji nimekasirishwa na kunya kwako, oh sorry dada kunywa kwako konyagi!!,au hgata pombe nyingine yoyote!! hembu soma Hosea 4:11, usisake biblia, nanukuu,'Uzinzi na divai na divai mpya huondopa fahamu za wanadamu",misho wa kunukuu, si jambo jema mama ,mchungaji kuondolewa fahamu yake kwa mambo haya mawili.Naendelea pitia na hapa, Waamuzi 13:4," ......., usinywe divai wala kileo, wala usile kilicho najisi"
Duh!
Cheki na hii, Luka 1:15"Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana hatakunywa divai wala kileo;......." Kuwa mama mchungaji ni kuwa mkuu mbele za Bwana hivyo dada yangu acha kunywa kileo. Msaidiane na mumeo kuchunga kondoo wa Bwana hatimaye wafike mbinguni.

Chemi Che-Mponda said...

Jamani, mbona watu wanachekesha. Kuna tofauti kati ya kunywa pombe na kulewa. Mimi siyo mlevi.

Asanteni kwa ushauri wenu lakini.

Kuhusu Konyagi, ndiyo ni kikali, wala sikatai, na hiyo ya swala ya akina mama eti wasinywe ndo sielewi kabisa. Maana nimeshuhudia wanawake wengi, wa makabila mbalimabli wkaiinya. Na wazungu wanaipenda kweli mbona hamsemi wanawake wa kizungu wasinywe?

KONYAGI OYEE! Je, Tanzania Distillers wanasamaj? Wanataka wanaume wafaidi peke yao?

Anonymous said...

yeah chemi mimi nakuunga mkono juu ya suala la kunywa pombe na kulewa kuna tofauti kubwa sana hapa na hakuna hata sehemu moja ya biblia kama hao wachache wanvyosema kwamba pombe imekatazwa pili lakini ulevi ndio umekatazwa
isitoshe nini maan ya kuwa mkristo?
ninavyoelewa mimi ni kwamba mkristo ni mtu anyefuata dini ya kristo kabla ya kristo hakukuapo na dini inyoitwa ukristo wakristo tunajitambulisha kwa jina la mwanzilishi wetu yaani kristo yaani sisi nni WA- kristo
sasa basi nitawapa mfano hao wanjifanya kukucritisize kwa kutoa scriptural quatations
imagine kama unataka kuwa raia wa marekanai.kuna mambo na tartibu fulani itakupasa uyafanye ili uweze kuhalalishwa kwamba wewe umekubaliwa na sasa unaitwa ni M-marekani na isitoshe utakula kiapo kwamba utatii na kufanya yale wanayofanya wenye taifa lao yaani wamarekani wenyewe.kwa kufanya hayo yote watu watakutambua kama wewe ni M-MAREKANI
kama unisema wewe M-KRISTO je si vema kufanya yale ayanyoambatana au tuliyagizwa na kristo ? si yote sababu mengine aliweza yy tu kuyafanya.je,si vema kutenda mambo kwa kufuata principles za U-KRISTO ili tuitwe WA-KRISTO
sasa kam kristo mwenyewe kwa mujibu wa scripture aliweza kutengeneza mvinyo ktk parrty iliwatu wanywe na kufurahi na siyo kwa lengo la kulewa .je hapa kuna principle gani tunaweza kufuat hapa ?ni kweli kwamba yeye kama mwanzilishi wa U-KRISTO amekataza pombe? kitu kimoja nafahamu kwamba yesu amepinga ulevi.ulevi si wa pombe tuu. nini maana ya ulevi? unfikiri ulevi unatokana na pombe tuu? je unafahamu kuna wangapi out there hawanywi pombe na lakini wanalewa wanavyo vilewa mpaka akili zao kupoteza uwezo wa kutenda haki na mema ambayo yesu ametuagiza ?
dada kata kirauli chako kwa afya ya matumbao yako na magonjwa mengineyo na faya yako kwa jumla
tafadhali kuwa mwangalifu tuu kwamba usije kulewa tena si pombe tuu hata lolote lile ufanyalo ktk maisha yako
pombe ni nzuri kwa afya zetu tena ile ya nyumbani maana ni pure!! na tumeizoea.
raceisnobar