Tuesday, April 03, 2007

TAMWA

Bila shaka mmesikia majina kama Fatma Alloo, Leila Sheikh, Edda Sanga, Maria Shaba, Pili Mtambalike, Wema Kalokola (marehemu), na Ananilea Nkya. Hao ni kati ya waanzalishi wa chama cha waandishi wa habari wanawake nchini Tanzania, TAMWA. Na mimi ni mmoja wa waanzalishi wa TAMWA (Tanzania Media Women's Association).

Tulitoka mbali maana mwanzoni tulipata pingamizi nyingi kutoka kwa wanawake na wanaume. Tulitukanwa na kuitwa majina ya ajabu kama, 'frustrated women, na malesbo'. Hivi sasa wanaume wakisikia jina la TAMWA wanatetemeka. TAMWA imefanya mengi kutetea haki za akina mama nchini Tanzania na inaendelea kwa nguvu! Tulianzisha kwa ajili ya kusaidia akina mama waliokuwa waandishi wa habari lakini ilikuwa mpaka kutetetea haki za akina mama Tanzania.

TAMWA Oyee!

Hii picha ilipigwa mwaka 1992. Tulikuwa kwenye safari Zanzibar na wageni wetu kutoka vyama vya akina mama mbalimbali barani Afrika. Mimi niko kushoto kabisa na miwani! Pia wamo Edda Sanga (3rd from left, Maria Shaba 5th from left, Halima Shariff 2nd from right). Wengine ni wageni kutoka nje.
Ndo baada ya hii safari iliyofana ilitokea kasheshe kubwa kutokana na picha fulani aliyopiga Muhidini Michuzi, na kuwekwa kwenye front page ya gazeti ya Daily News mpaka ilibidi viongozi wa TAMWA warudi Zanzibar kuomba radhi. Picha eneyewe ilipigwa kwenye shughuli ya mpendwa somo na kungwi mkuu wa Tanzania, Bi Kidude.
Kwa habari zaidi kuhusu TAMWA someni:

21 comments:

MICHUZI BLOG said...

hahahaa! chemi umenirudisha mbali kweli. sintokaa nikasahau hiyo siku kwani ilikuwa ni mmoja wa msukosuko mkubwa wa kiuandishi nilopata. lakini baadaye nikaja kushukuriwa kwani nilianika hadharani kwamba tendo la unyago linaelekea hadharani, wakati haikubaliki

Chemi Che-Mponda said...

Yep, siku ile ilikuwa kashehshe kweli kweli. Mbona watu walilia! Na picha enyewe kwa sasa isingekuwa na neno. Au siyo?

Anonymous said...

Leo hatimaye tumeona!! Kumbe huko nyuma hujambo. hahaha

Anonymous said...

Naomba tu mniwie radhi, lakini hadi sasa hivi hiyo tamwa naiona kama genge la wanawake jeuri wanaopigania mambo yasiyo na msingi kabisa, k.m kushindania kuvaa suruali kama wanaume (ati huu ndio usawa!), kutaka wanawake nao waoe na wanaume wapike nyumbani (kisa ati mbona hotelini wanapika!) Wameshindwa tu kudai kwamba wanaume wabebe mimba, wajifungue, wanyonyeshe, waitwe MAMA na wanawake waitwe BABA. Typical utopia. Goddamned feminists! Wanawake wenye akili timamu wako TAWLA na MEWATA, hao nawakubali. Lakini tamwa? Horse shit!

Anonymous said...

ha ha ha.
tamwa sielewi mwanamke gani huyo wanayedai wanamsaidia!!! pleeeaaaase! wanawake mpka leo wasio na mbele wala nyuma wananyanyasika na hakuna chochote anachosaidiwa na tamwa.mwanaume anaacha mkewe bila sababu yoyote ya msingi.anakimbilia tamwa.tamwa hakuna msaada wa aina yoyote.mume anachukua watoto,mke ana mwaka wa tano hajaona watoto wake.tamwa iko tu.tamwa ni majanja tu km majanja mengine ya kula.haya kuleni vizuri tu na acheni kujifanya mna dai haki ya mwanamke,endelezeni tu deal zenu za kukamua kuelekea mbele.

Anonymous said...

Tatizo wanawake wengi wa TAMWA hawajaolewa au wameachika, jamani wanawake msidanganywe na hawa waachikaji. Halafu hao wenyewe ndo wanaiba waume za watu, nani hasiyeitaji kunani......... Shame on you. Kwanza hizi NGOs ziko mijini tu kazi kudanganya sponsors, wakipewa pesa kitu cha kwanza ni kupendeza tu ili kuvutia kwa men. Shenzi taipu

Anonymous said...

Tatizo wanawake wengi wa TAMWA hawajaolewa au wameachika, jamani wanawake msidanganywe na hawa waachikaji. Halafu hao wenyewe ndo wanaiba waume za watu, nani hasiyeitaji kunani......... Shame on you. Kwanza hizi NGOs ziko mijini tu kazi kudanganya sponsors, wakipewa pesa kitu cha kwanza ni kupendeza tu ili kuvutia kwa men. Shenzi taipu

Anonymous said...

Mlianza mbali harakati zenu pamoja na kupigwa vita na wapinga demokrasia Maana Demokrasia Tanzania hupigwa vita sana.
Ushahidi nenda Blog ya Issa Michuzi kaangalie ameweka picha ya Christopher Mtikila ili watu watoe maoni.

Lakini maoni yale watu wasiopenda uhuru wa maoni wameyaingilia na yanasomeka kama kichina hivi.Wataalamu wa Technologia ya habari mtusaidie hivi huo nao sio uingiliaji wa uzuiaji demokrasia ya habari kwenye blogs?

Sio ufungaji mdomo kwa watu ili wasitoe maoni?

Kuna watu wanamwogopa sana Mtikila maana na mpigania demokrasia halisi anayeheshimika Tanzania.
Yameanza yaleyale ya Mugabe ya kubana vyombo vya habari zikiwemo Blogs.

Anonymous said...

Wewe anony wa 7:48AM, ulichukuliwa bwanako na mwanatwamwa nini? Una hasira sana na hao akina mama. Kwa maoni yangu wanafanya kazi nzuri Tanzania.

Anonymous said...

Chemi tunaweza kurudia topic ya matako makubwa?Mi ni mwafrica halisi

Anonymous said...

Tunashukuru Blog ya Issa Michuzi pale penye picha ya masuala ya Mtikila iliyokuwa imevurugwa na wapinga demokrasia ya blog kwa kuifanya isomeke kichina wameiachia na sasa iko Ok.

Anonymous said...

Hii picha inaonyesha ilipigwa na Lucas Lukumbo wa Shihata na sio michuzi wa D/News!!!!
Pia kuna alama au maandishi kuwa ilikuwa page 5 (Jan 23, 1992)na sio 'front page'
Chemi unasemaje... who's wrong and who's right???

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 8:46AM, picha enyewe iliyotoka Daily News front page siyo hiyo, na wala hakuna negative, wala gazeti iliyobaki. Ilikuwa destroyed kabisa maana ilikuwa kasheshe kwa kipoindi kile. Picha niliyobandika ilipigwa kwenye safari ambayo ile picha iliyoleta mzozo ilipigwa. Samahani kama sikueleweka vizuri.

Anonymous said...

Hivi hebu Chemi nikumbushe.....huu ndio wakati ule Michuzi alipomnanihii huyo mwenzenu mpaka huyo mwenzenu akachanganyikiwa na kuanza kumsifia Michuzi mitaani kuwa anajua kunanihii? Du! Mpaka leo nikimwona huyo dada nashindwa kummaliza!

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 1:29PM, hiyo habari unayosema sina habari nayo kabisa! Ndo nasikia kutoka kwako.

Kwa kufafanua zaidi ile picha nayo zungumzia ilipigwa tukiwa safarini Zanzibar. Tulikuwa kwenye shughuli ya Bi Kidude. Sidhani kama kuna copy ya hiyo picha iliyo-survive, maana ilikuwa kesi mpaka huko top! WaZanzibar waliona kama wametukanwa. Maskini ya Mungu, mbona Michuzi alikipata. He is a Survivor!

Anonymous said...

Nimepitia upya stori na nimeona kuna sehemu nilipitiwa au sikupasoma vema.
Ni kweli ktk habari yako, ulifafanua juu ya picha ya Michuzi; na hii picha ya L. Lukumbo (SHIHATA) haihusiani na ile ya Michuzi wa D/News. Samahani kwa kuchanganya kuhusu wapiga picha na page iliyotokea ktk gazeti!!!

Anonymous said...

Kweli kabisa wazee, hawa TAMWA wahuni tu tena wabomoaji na siyo wajengaji. Hata huyo mkurugenzi wao wa sasa kwa kweli namhcukia sana, maana na mimi nilishapita Radio Tanzania miaka ya 1999-2002, kabla ya huyo mama kuwa kingunge wa TAMWA alikuwa anamshauri girlfriend wangu, kwamba eti asikubali kunipa vitu mpaka nimuoe, lasivyo yeye anatasema kwa wazazi wake. TAMWA washenzi tu hawana lolote

Anonymous said...

Wewe Anonymous wa 2:29AM, ulinyimwa siyo. Huyo mkurugenzi wa TAMWA alimshauri huyo girlfriend wako vizuri. Kwa nini ununue ng'ombe wkati unaweza kupata maziwa bure? Koma na nyege zako!

Anonymous said...

Kweli ndo maana Chemi aliweka topic ya matako makubwa, mimi sikujua kama naye yumo kwenye hilo kundi. Wapenzi wa matako makubwa wana cha kutueleza, labda na wengine watavutika. Lakini vile vile tungelipenda kumsikia Chemi naye anasemaje.

Anonymous said...

I wish ningeiona hiyo picha. Hata hivyo naamini pamoja na kuwa destroyed copy itakuwepo mahala, japo kwa Michuzi mwenyewe. Acheni kutubania, hebu iwekeni wazi nasi tuione kwani naamini kwa sasa hamna noma!

Anonymous said...

Chemi. Umenikumbusha mbali. Hizo ndizo zilikuwa siku za harakati! Kasheshe la Zenj. Mimi nilikuwa mmojawapo wa viongozi wa TAMWA tuliolazimika kwenda omba radhi kwa Waziri wa Habari, Utamaduni n.k. Mpaka leo sijajua tulivunja maadili gani ama ya kiuandishi au kiutamaduni. Nadhani ulikuwa ubabe tu. Miaka michache baadaye nilikuwa nafanya utafiti kuhusu watoto wanaoishi katika mazingira magumu. nikakumbana tena na huyohuyo dada ambae alikuwa sasa ni waziri wa wanawake, watoto nk. tulienda kumpa taarifa kuhusu utafiti tuliokuwa tunafanya. nilikuwa unicef kipindi hicho. akatwambia Zanzibar hakuna watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu! lakini utafiti ulidhihirisha vingine- kuwa walikuwepo watoto wanaotumikishwa, watoto wanaouzwa kwa ngono wakike na wakiume, mimba za utotoni na kuozeshwa kwa nguvu. kwa hiyo wakati mwingine ni hulka tu za watu wakalikuza jambo ambalo halistahili! Pili