Saturday, April 14, 2007

Marudio - Acheni Ushamba

Hii ni kati ya posts zangu za mwanzo:

Tuesday, October 18, 2005

Acheni Ushamba! Jamani, jamani, jamani! Siku hizi nikiona vijana waBongo hapa mitaani Boston nakimbia! Hao vijana siyo wale wa miaka ya nyuma waliokuwa tayari kufanya kazi mbili/tatu ili waweze kuishi vizuri na kupeleka zawadi nyumbani. Hapana vijana wa siku hizi wanataka vya dezo!

Wamekuja Marekani wakidhania maisha USA ni kama vile kwenye video za Rap. Hapana vijana, maisha siyo hivyo kabisa. Hapa USA kama hukuja na hela zako basi uwe tayari kuchapa hizo kazi mbili/tatu, utafanikiwa! Lakini kinacho niudhi hasa ni hao vijana wanaoenda madukani na kuiba, yaani shoplifting! Yaani mtu anaingia dukani anasomba vitu, tia ma-cap kichwani halafu wanatoka nje ya duka. Wanakamatwa halafu unaombwa uwawekee dhamana! Si waliiba wao wacha wakome huko jela! Tena jela za Boston ni nzuri kuliko kupelekwa Keko! Nasema hao vijana ni washamba maana ukiwauliza kwa nini waliiba, watasema, “Oh, sikujua kama wananiona!” Hawakuoni???? Heh!

Mjue mkifika kwenye mall tena parking lot, mnaanza kuchgunguzwa na makamera yaliofichawa kila mahala isipokuwa chooni! Yale mapambo na magololi yanayoing’inia si urembo tu, bali ni masecurity camera. Hivyo huwezi kusema, “Oh sikuiba!” huko store detective anakutolea kanda ya video ambacho wewe ndo star!

Wanaona kwa vile mlango huko wazi hakuna security, au watu wengi basi ni free for all. Kitu kingine hao vijana,utasikia wanaongea, sijui vitu gani, wakidhania English! Wanajaribu kuiga ma-slang wanaosikia kwenye movies. Nyie! Watu hawaongei hivyo!

Ukitaka kazi ya maana ujfinze kuongea English! Yaani inatisha maana huwezi hata kuelewa ansemaje na Slang zake zenye Bongo accent! Na acheni kuvaa kama gangsta! Kwanza ukikosea rangi utapigwa risasi na ma-gang au utasumbuliwa na polisi wakidhania wewe ni gang banga!

Na poleni vijana ambao wanashuka kwenye ndege wakidhania wanaenda kuishi kwenye nyumba inayofanana na ya P. Diddy, lakini wanakuta wanaenda kubanana watu 10 kwenye chumba kimoja.

Na kuna wengine wanafanya uhalifu kama kuingia kwenye biashara haramu ili wapate pesa za haraka. Sijui ni kwa kuwa hawajui au hawajali,lakini wanhatarish maisha yao na za familia na marafiki zao!

Ngoja niishie hapa ...maana!

5 comments:

Benjamin said...

kwa kweli dada Chemponda umechangia ushauri wa bure na wenye manufaa kwa jamaa zetu.

Anonymous said...

Chemponda vijana wengi wanaotoka Dar,Tanga I mean asilimia kubwa don`t get me wrong asilimia kubwa ndo wanajifanya mambo haya ila vijana wanaotoka mikoani wakifika hapa wapole kama nini kazi saaana sanasana watazama kwenye kuimba kwaya kanisa kwa sana.Ila kwa kweli kweli kingereza cha watu wanaojifanya kinakera mnooooo na mavazi ya kuiga.Eti kijana mshamba ile mbaya lakini sasa nguo zake za wal mart zinaembarass ile mbaya.

Anonymous said...

Wee Chemi chemponda acha zako, usijifanye askari kanzu wa wamarekani na wala usituletee ukambunga wako wako hapa. Usidhanie sote tumetoka tunduru kama wewe. Mwizi ni mwizi, kama ameiba dukani marekani basi hata kama angebakia bongo angekuwa anaiba kulekule bongo, (unless kama unatuambia kuwa bongo hakuna wezi). Wewe kama unakuwa "embarassed" na makosa yasiyokuwa yako, basi ujue una matatizo binafsi.

Samahani, lakini mimi m-bongo akipiga tiktaka ughaibuni, mimi naona hiyo ni moja tuu ya "struggle" ukizingatia wewe mwenyewe Chemi unajua kuwa sisi ni victim of the system, kwahiyo kufuata sheria zote za wakandamizaji siyo ujanja. Ingawa kama wewe ni mfuataji sheria mzuri hiyo pia ni nzuri vilevile.

Chanjeni chanjeni wanangu huko, rudisheni fweza nyumbani tuu, msijirushe kupindukia.

Anonymous said...

Hayo maisha ndiyo yameyahitaji wenyewe, ukizingatia hata hao ambao tayari wamekuja huku huwa hawasemi ukweli juu ya maisha ya huko. Wacha wafe tu mwizi mwizi tu na haki yake ni mauti. Nyamafuuuuuuuu

Anonymous said...

Jamani ustaarabunikitu cha bure. Wewe unayemtukana dada Chemi,huna mama, shangazi au dada? Mboa umepugukiwa heshima nama hiyo. Jirekebishe tafadhali maana haipendezi.