Monday, January 07, 2008

Barack = Baraka


Obama alivyomaliza High School


Kwa wasiojua jina la mgombeaji wa rais wa Marekani kutoka chama cha Democrats, Senator Barack Obama, ni 'uzungunization' wa jina Baraka.

Kwenye taarifa ya habari wanawaambia watu kuwa Barack ina maana ' Blessed' (aliyebarikiwa).
Na sisi waswahili tunajua katika lugha yetu hakuna neno inayoandikwa Barack. Hivyo naona kwa vile walikuwa Marekani, na ni jambo ya kawaida kufupisha majina, au 'kuzungunize' jina walibadilisha jina, Baraka kuwa Barack. Na alivyokuwa shule alikuwa anatumia jina 'Barry Obama'.

Kwa wanaokaa hapa Marekani wanajua wakati mwingine kusudi usonge mbele inabidi kuzungunize majina. Wayehudi wamefanya hivyo miaka mingi, na wahamiaji waliofika Ellis Island enzi za 1900's wengi walikuwa majina yao yanabadilishwa hapo hapo. Wayehudi walifupisha au kubalisha majina kusudi watu wasijue asili yao, mfano jinaGreenberger ilikatishwa kuwa Green.

Hebu tajeni majina yaliyokuwa Kizungunized. Kuna machache hapo chini

Osama = Sam
Suleiman = Sal
Mohamed = Mo/Mike
RutaXXXXXXX = Ruta
Rashid = Rick/ Rich
Abbasi = Abe

5 comments:

Anonymous said...

Che Mponda --- Cher

KKMie said...

Habari da' Che Mponda. Nasikia huyu bwana Baraka anaasili ya Kenya kuwa baba yake ni Mjaluo hivi ni kweli na Obana ni jinala Kijaluo na lina maana yake (nimesahau nikikumbuka nitasema).

Chemi Che-Mponda said...

Hi Dinah,

Ni kweli kuwa marehemu baba yake Obama, ni Mjaluo. Sijui Obama ina maana gani. Wamefanya mahojiano na familia yake huko Kenya hivi karibuni.

Anonymous said...

Dada Mija,
Hii story yako inanikumbusha kijana wetu mmoja ambaye Juzi tu mitaa ya Sinza pale alifahamika kwa jina la Hashim Thabit na sasa yupo Marekani na amewika sana kwa Kikapu katika anga za Vyuo.

Hivi sasa vyombo vya Huko vinamripoti jina lake kama Hasheem Thabit( tayari wamezungunize/"tohoa" sijui) Jina halisi.

Anonymous said...

lol, nilivyokuwa Undegrad, kuna kaka mmoja African American ambaye alikuwa ni Math tutor akijualikana kwa jina la "Keejay." Mimi na rafiki zangu tulimzoea kwa vile tulikuwa tunaenda kukaa huko Math lab kusoma. Siku moja niko huko, nikawa naangalia schedule ya Math tutors imebandikwa mlangoni, nikasoma jina la tutor in charge nikaona "Ambakisye." Nikajiuliza huyu mnyakyusa katokea wapi, maana waTanzania tulikuwa wawili tu kwenye shule yetu (at that time), mimi na cousin wangu. Basi nikaingia huko lab nikauliza "who's Ambakisye." watu wakawa wananishangaa hawaelewi, mwishowe "Keejay" akasema who? nikarudia Ambakisye, the name is over here. Basi akasema kuwa ni yeye. Nikamuuliza amelipata wapi hilo jina akasema baba yake kampa, it's supposed to be African.
Basi nikacheka, nikamueleza hilo jina linatokea wapi, he was just like oooh!!

Anyway, "uzungunization" wa majina upo. Sema hawa wamarekani weusi wanapenda kuwa na majina halafu wanasema ni "African" hata hawayaelewi.

Kuna mwingine shuleni kwetu huko alikuwa anaitwa "Kimba." My cousin and I used to laugh all the time.