Tuesday, January 15, 2008

Remembering Nellie Kidela 1946-2007

Mtoto wa marehemu Nellie Kidela, Nuru Mkeremi, kaburini mwa mama yake (Oct. 24, 2007).

Nellie Kidela (wa pili kutoka kushoto) na familia yake June, 2007


Nuru Mkeremi akipewa rambirambi kutoka mwakilishi wa TAMWA, Ichikaeli Maro. Hapo ni kwenye mazishi ya Dada Nellie October 12, 2007.

Dada Nellie akiwa na Violet Weinberg, ambaye alikuwa mpigania uhuru wa African National Congress, January 11, 1981.

Dada Nellie Kidela, alifariki dunia mwezi Oktoba mwaka jana 2007. Alikuwa ni mtangazaji maarufu wa Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) miaka mingi. Mwanae, Nuru Mkeremi wa Boston ameniletea picha na habari zaizi nizi - share na wadau.

Nellie Kidela, alijuinga na RTD 1976 kama mtangazaji (radio broadcaster). Aliwahi pia kuwa mwalimu katika shule za msingi za Oyster Bay na Olympio mjini Dar es Salaam.

Alivyokuwa RTD alifanya kazi katika Idhaa za Kiswahili na ya kiingereza (External Service). Aliandaa vipindi kama Face the Mike, Ugua Pole, Chei Chei Shangazi, From Me to You, Potpourri, Songs to Remember, na Majira.

Alikuwa Mwanachama wa Amnesty International, Tanzania. na alifanya kazi nao kila akipata nafasi.

Dada Nellie ni mmoja wa waanzilishi wa Chama cha waandishi wa habari wanawakeTanzania (TAMWA). Mkutano wa kwanza kabisa ulifanyika nyumbani kwa Dada Nellie.

Miaka ya 80, Dada Nellie alihusika sasa na chama cha Tanzania Cerebral Palsy and Mental Retardation. Alikuwa na mtoto ambaye aliugua na kuathirika na Cerebral Palsy akiwa na miaka 6. Mtoto alifariki miaka ya 90.

Mwaka 1999, Dada Nellie, alikuja kumtembelea mwanae Boston. Ndo hapo alienda hospitali na waligundua anaumwa kansa ya ziwa. Alipata matibabu Boston University Medical Center. Baada ya matibabu walidhania amepona. Alikaa miaka sita katika 'remission'. Kansa ilivyorudi mwaka juzi walikuta umeingia kwenye mifupa.

Dada Nellie alijitahidi sana kuendelea na shughuli zake, japo alikuwa na maumivu makali sana shauri ya kansa.

Dada Nuru anasema mama yake alivyofariki alikuwa anatabasamu. Kabla hajakata roho aliwaambia watu kuwa wasiwe na wasiwasi atakuwa okay.

Dada Nellie atakumbukwa daima na familia, marafiki, na wasikilizaji wa Radio Tanzania Dar es Salaam.

REST IN PEACE

5 comments:

Anonymous said...

Oh pole sana dada Nuru,Mama kidela alikuwa mama yetu na jirani yetu hapo Upanga mtaa wa Mfaume,tunamkumbuka sana,na wote tulishtushwa na kusikitika kwa kuondoka kwake but yote ni mambo ya Mwenyezi Mungu,

Mungu azidi kuwatia nguvu

Jirani

Anonymous said...

Pole sana Nuru, I am so sad i didnt come to the funeral lakini ni kazi tu rafiki yangu nilikuwa mikoani, lakini namkumbuka sana mama, she was very charming and loving. Sote tumetoka mavumbini na tutarudi mavumbini, Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi. Amen please kiss merrymbeyu for me!

Hellen

Anonymous said...

Pole sana Nuru.. It's a long time tangu JKT hatujaonana.Pole sana my dear yote ni kazi ya Mungu.
Tuwasiliane jamani..

Rehema

rchonde2002@yahoo.com

Anonymous said...

kunawatu wazamani jamani yaani walipitia JKT nabado wako freshh

Anonymous said...

Nakumbuka kile kipindi cha Chei Chei Shangazi na sauti ya Mama Nellie.

Rest in Eternal Peace Mama Nellie.