Tuesday, November 04, 2008

Mr. Universe Tanzania 2008 - David Nyombo

Wadau, tumezoea kuona wanawake katika mashindano ya urembo. Sasa cheki huku kaka kwenye mashindano ya Mr. Universe! Na sisi wanawake tunataka kuona eye candy pia!

********************************************
Kutoka Michuzi Blog:

Mwakilishi wa Tanzania katika Mr Universe David Nyombo (pichani) akionyesha jinsi anavyoweza kuifanya vitu vyake. Mwamba huyu ni mshindi wa Afrika mwaka 2008 katika kategori ya kilo 70 kwa mchezo huu, sasa anakwenda Bahrain, kufanya vitu vyake.

Huko anakwenda kuiwakilisha Tanzania na Afrika katika mashindano ya 62 ya watunisha misuli ya ridhaa ya Dunia yanayofanyika kuanzia Novemba Mosi mpaka 7.

Mwamba huyu ambaye alizaliwa Mei 13, 1975, jijini Dar es Salaam ni mtunisha misuli wa kwanza Tanzania kushiriki katika mashindano ya Mr Universe Afrika kutoka mwaka 2002.

No comments: