Tuesday, November 25, 2008

Yaliyompata Mdau Mlimani City

Nimeletewa hii na mdau huko Dar:

******************************************************

TAHADHALI WATANZANIA WENZANGU

Jumamosi ya juma lililopita tarehe 22 majira ya jioni,

Nilipata nafasi ya kutembelea duka la nguo lijilikanalo Mr.Price hapo mlimani city,

Katika kujichagulia nikapenda na top moja nyeupe,mi nikaenda kuijaribisha ile top,pamoja na nguo zingine nilizozipenda,wakati naangia na ile nguo,yule dada amabye yuko mlangoni kwenye chumba cha kubadilisha akaniambia angalia nguo yangu nyeupe usije ukaichafua,ah mi nikamwambia kwa mfano ikitokea ikachafuka itakuwaje akasema ah aha mi nakuambia tu,basi mie nikajaribu kwa umakini sana tena sana lakini haikunitosha so ikawa sio chaguo langu tena,ile nguo ilivyotoka nje baada ya dakika 10 wakati najaribu nguo nyingine na kunitosha ndo nikawa naelekea kaunta kulipa zile zilizonitosha yule dada akaniitia walinzi wao kuwa nimechafua shati lao jeupe kwa wanja(make up ya machoni),na sheria yao ni kwamba mtu akichafua nguo lazima alipe.basi wakaning’an’gania nilipe ile top ya thamani ya Tsh22,000/= .kwa kweli nilighadhilika na kuwaambia kuwa mimi sitaweza kulipa maana sikuona kuwa nimechafua na kama nimeichafua ni bahati mbaya na wala hamkuniambia kuwa kuna malipo iwapo mteja akitokea kudamage nguo,basi nikawaambia hapa kwenye kapu nina nguo ya thamani ya 150,000 na hii top moja mnayotaka kuninunulisha ni 22,000 tu sasa nilipie hizi zilizonisha nah ii niache au niziache hizi za laki na nusu,wakasema utajua mwenyewe,na hapo uku mie mteja napewa lugha za kashfa na dharau mtindo mmoja kutoka kwa hawa wafanyakazi wa humo MR PRICE..Basi mie nikaawaambia mie narejesha hizi za laki na nusu na kulipia moja ya 22,000/= wakasema kwa jeuri sawa.sasa sijui hapa nani kaumia ni mimi ambaye iyo Top nilimpa mdogo wangu hapo hapo maana ilikuwa inamtosha au wao kuleta sifa mbaya na kutokuwa na customer care na kupoteza laki na nusu na kuku bali 22,000 pia kupoteza wateja?

Maana sikatai kuwa kuna watu wananunua hadi laki5 but mteja ni mteja tu hata kama akiwa mweusi mwenzio na wewe uko unafanya kazi kwenye duka la mzungu sasa unajiona na wewe mzungu,na kudharau wabongo wenzio.

Hii ni tahadhari kwa WaTanzania wenzangu watembeleapo maduka ya MR Price pale mlimani city dar es salaam,unaweza ukapata kiherehere cha kujaribu nguo labda kwa lengo la kuja kuifata kesho then ukawa hauna pesa,utajikuta umegadishwa kwa muda mrefu na kupoteza muda wako kwa wabaguzi na wasiojua biashara ya nguo kama hawa.

Ni hayo tuu.

MDAU

14 comments:

Anonymous said...

pole sana dada yetu ndo maisha ya kibongo bongo yaaani inauma sana hii inatokana na wafanyakazi wengi kuwa malimbukeni wa hela na maisha maana mtu akiwa na fedha anajiona kafika , dharau nyingi yaani sijui tutafika lini ? ni kazi ya zaida sio hapo tu kila mahala ,dharau majivuno maana na mimi siku hiyo hiyo nilijaribu kununua simu n96 nokia ila mtu anakujibu kama ataki yaani anadharau akidhani sijui hauwezi kununua simu ya hiyo cjui wanunuzi wana chata ya fedha usoni , yaani sijui tufanyeje !ila ni mambo mengi yanachangia hali kama hizo .....nivigumu ,,,kueleza yote ila wewe ungegoma mimi nisingelipia chochote nikurudisha nguo zao zote ..

Anonymous said...

Naona bado tupo nyuma katika kuhudumia wateja.Mi nilikuwa bongo mwaka jana nikatembelea ile Supermarket pale Mlimani.nilikuwa nimebeba kibegi kidogo nikakiacha pale mapokezi kama inavyotakiwa.basi nikaingia ndani kufanya shopping yangu nilikuwa pamoja na dada yangu na mdogo wangu mmoja wa kiume.nilipomaliza shopping nikalipa kama kawaida,basi wakati tunaelekea malangoni kutoka nje akaja jamaa mmoja mlinzi wa pale na kuniambia kuwa natakiwa kwenda kwenye chumba cha kufanyiwa check up kwa sababu kuna kitu kimeonekana kwenye mifuko yangu ya suruali.nilikuwa na betri za camera ambazo niliingia nazo dukani na kusahau kuziacha pale mapokezi.kitu cha kipuuzi ni kwamba hawa wajinga kumbe waliona wakati naiingia kuwa nna kitu mfukoni kupitia sensor zao lkn hawakutaka kuniambia wakasubiri mpk wakati natoka ili wanidhalilishe kuwa nimeiba au something.na wakati wote nafanya shopping kulikuwa na mtu anamifuatilia kwa nyuma,yaani pamoja na kujua kuwa nimeingia na betri hizo kutoka nje lkn wakapoteza man power yote hiyo kunifuatilia duka zima kwa karibu saa nzima.bahati nzuri mi ni mwanasheria na najua haki zangu basi kwenye kichumba cha searching nikawatilia ngumu mpka waniambie tatizo hasa nini,kama wana uhakika kuwa nimeiba au la.ndio akaja msimamizi wa duka na kuniambia kuwa uliingia na kitu kwenye mifuko yako,basi ikabidi niwajie juu wakawa hawana la kujieleza zaidi ya kujiumauma tu.TATIZO NI KUWA WAMEWEKA WATU AMBAO HAWAJUI KITU CHOCHOTE NA HAWANA ELIMU YEYOTE KATIKA KUHUDUMIA WATEJA.INABIDI NA SIE WATEJA TUWE TUNAKOMAA KWA kujua HAKI ZETU za msingi..
Mdau Greece

Anonymous said...

Huna lolote ni kujishaua tu. Sasa kwa nini ulichafua na uliuliza 'ikichafua je?'. kwenda zako huko. hapa umeandika kwa upole lakini unaonyesha tu lugha yako kwa hao wahudumu ilikuwa sio ya kistaarabu. Unaonekana ulitaka kujionyesha kuwa umesoma au namna yoyote ya kujifanya matawi. ndio maaana walidharau laki na nusu yako na kuchukua 22,000. Mpunguze dharau kwa watu wasiosoma. utamaduni wa mteja ni mfalme hauna maana uwanyanyase wahudumu kwa kuwa wao ni vibarua na masikini wanatafuta mahitaji yao. Kweli mmiliki wa duka asingaliachia laki na nusu lakini walichokufanyia sawasawa. Bola lawama kuliko fedheha.

Anonymous said...

we umechafua na miwanja yako lazima ulipe,we unafikiri kila mtu atie mi-lip stick yake kwenye nguo si duka litakuwa kama linauza mitumba kariakoo.eti duka la mzungu,si ukanunue kwenye duka la wachaga kisutu,we vipi bwana,haa!

Anonymous said...

Hatutaendelea mpaka tufute ujinga,uswahili wote mliomponda huyu dada kuwa anajishaua upeo wenu wa kuchambua na kufikiri ni mdogo sana, na mtaendelea kuzikumbatia biashsra za chai maandazi hadi mwisho wenu na hata muingizwe darasani mtapoteza muda tu, endeleeni kuona leo wakati watu wanaona kesho, endeleeni kulalia vitanda ambavyo watu walikwisha amkia.

Anonymous said...

Ni kweli wengine wakifanya kazi kwa mzungu wanajiona kuwa wamefika. Wanajiona bora kuliko weusi wengine. Ni fikra za kitumwa hizo. Pole dada yangu.

Anonymous said...

..Hivi we dada nawewe ukichafuliwa na mwanamme halafu ukiachwa,lakini huyo alokuchafuwa akaowa mdogo wako utakbali...???

Naona unambwe mbwe tu huna lolote. Yaani nguo za watu uzipake masinzi (wanja) na mirangi ya mdomo, halafu uachiwe, eti mteja??? ebo, sasa na mimi niende na mijasho yangu nikavae mashati ya watu dukani niyachafuwe halafu niyarudishe kisa mteja niachiwe??? Kwa taarifa yako hapo wao ndo wamepata faida, sababu hiyo nguo wangekusamehe isingenunuliwa na mtu tena, sababu ya hiyo mirangi yako na miwanja yako + na kikwapa chako uvundo, wangepata hasara zaidi ya elfu 15, lakini sasa wamepata faida! Ukienda dukani kwa watu sharti uwe na adabu sio uchafuwe nguo za watu sababu ya kilaki chako!

Anonymous said...

Kuna maduka mengine kwan maeneo ya waspanish yana mabango, 'No Trying on Blouses' yaani hamna jaribu mablaus. Kisa wana vikwapa na kuzipaka make-up foundation lipstick etc. Kama kuna shida kwa Mr. Price basi naye aweke bango, 'No Trying on Blouses!"

Anonymous said...

Kwanza pole dada kwa yaliyokukuta.hao waliokandia hapo juu wanaonekana na wadada fulani washari wa kama sio buza kipera kwa muuza madafu basi manzese kwa mfuga mbwa.how come unatetea ushenzi aliofanyiwa mteja wa watu.eti basi wenzako wamepata faida.ni faida gani ya kuchafuliwa sifa.kama ninyi ni wafanyakazi wa hapo na mnajibu shutuma kwa matusi kweli bosi wenu akiwagundua kazi hamna.kwani vtendo hivyo bongo ni vingi mno watu wanajiona sana wakiwa na kazi yenye kakuweza kumcontrol mtu ni shida.siku ikiota nyasi majuto ni mjukuu.tujifunze kutoa huduma kwa wateja vzuri jamani.we embu fikiria ukikutana na wadada wanauza dukani kama hao juu na midomo inayonuka matusi kweli utatoka umepona kweli?.hiiiiii mihayo.....

Anonymous said...

Kha bongo tambarale.mi ni mchaga nina duka na lina nguo quality kuliko hapo Mr.price.uyo anayesema kwadharau eti aende kwa mchaga.usidharau mwiba bwana utakuchoma.we mwenyewe hata kibanda cha mkaa huna.tuwe watanzania sio kuleta mambo ya kikabila hapa.kama mnashidwa kuhudumia wateja.njoweni tuwafundishe customer care.ndio maana mchaga unayemdharau leo utamkuta na kijibanda kesho nalijiduka.sasa wewe kalia ilo bao eti mteja anamashauzi.mteja akiondoka ndio mseme kwa mwezio tena asisikie.lakini sio kujibizana na mteja.kama vpi fungua duka lako then onesha madharau uliyotaja ukifanikiwa nitafute hapa kwa Chemi mie nitakuongezea m taji.

Anonymous said...

umenifurahisha sanna mdau wa mwisho hapo kutoa comments..yaani kama mtu anadharau wateja sasa si afunge duka na atuoneshe hicho kiburi chake ..hajui kuwa wateja ndio wanampa pesa ya kwenda chooni.unaamka asubuhi unawahi daladala kwenda kusubiria wateja afu unaleta dharua..aaagh.
mdau wa juba,
sudan

Anonymous said...

umenifurahisha sanna mdau wa mwisho hapo kutoa comments..yaani kama mtu anadharau wateja sasa si afunge duka na atuoneshe hicho kiburi chake ..hajui kuwa wateja ndio wanampa pesa ya kwenda chooni.unaamka asubuhi unawahi daladala kwenda kusubiria wateja afu unaleta dharua..aaagh.
mdau wa juba,
sudan

Anonymous said...

huduma kwa wateja ni jambo muhimu sana katika biashara,nikiwa kama mteja mzuri wa bidhaa tofauti kutoka kwenye maduka ya mr price(home,and clothing) hapa south africa,..customer service ni muhimu sana katika biashara,(customer retaining and retantation tool)...silaumu mfanyakazi wa mr price tz,nalaumu management ya mr price tz,management inawajibika katika ku-train wafanyakazi na issue nyingine zinazohusiana na huduma kwa wateja...ijapokuwa sometimes kibongobongo,sio tu matajiri viburi(kama mzee wa vijisenti)hata masikini jeuri wapo pia...kitu kimoja nilichojifunza na ninachojifunza kwa wenzetu,ijapokuwa ni weusi kama sisi,inapokuja swala la biashara na huduma bora wapo makini sana...

Anonymous said...

huduma kwa wateja ni jambo muhimu sana katika biashara,nikiwa kama mteja mzuri wa bidhaa tofauti kutoka kwenye maduka ya mr price(home,and clothing) hapa south africa,..customer service ni muhimu sana katika biashara,(customer retaining and retantation tool)...silaumu mfanyakazi wa mr price tz,nalaumu management ya mr price tz,management inawajibika katika ku-train wafanyakazi na issue nyingine zinazohusiana na huduma kwa wateja...ijapokuwa sometimes kibongobongo,sio tu matajiri viburi(kama mzee wa vijisenti)hata masikini jeuri wapo pia...kitu kimoja nilichojifunza na ninachojifunza kwa wenzetu,ijapokuwa ni weusi kama sisi,inapokuja swala la biashara na huduma bora wapo makini sana...