Saturday, May 16, 2009

Sinema mpya ya 'Kutisha" Bongo

Naona Bongo wameingia katika genre ya sinema za Horror (Kutisha). Tunapiga hatua!
Asante Kaka Beda Msimbe (Lukwangule Blog)

Kampuni mama ya kutayarisha, kudurufu na kusambaza sinema Tanzania inayokwenda kwa jina la Tollywood Movies, imechukua dhamana ya kusambaza movie mpya ya kutisha iitwayo Roho Sita, Joseph Shaluwa anashuka nayo.

Roho Sita ambayo imetayarishwa na Koga Film chini ya Mkurugenzi wake Thomas Simon, itakuwa sinema ya kwanza ya kutisha ambayo matukio mengi yanaonekana halisi tofauti na nyingine zilizotangulia.

Mkurugenzi wa Filamu za Tollywood Movies, Hamie Rajab, aliliambia Ijumaa kwamba, katika sinema zote za kutisha za Tanzania, hakuna iliyowahi kuifikia ubora wa Roho Sita.

“Mpaka Tollywood tumeamua kuichukua basi mashabiki waamini kwamba kitu kimetulia, ni sinema ya kwanza ya kutisha ambayo kila kitu kinaonekana halisi, kubwa zaidi ni kwamba program iliyotumika katika uhariri ni ya kisasa duniani, ndiyo maana imeifanya kuwa bora na yenye kiwango cha Kimataifa.

Wadau wasubiri kidogo, siku si nyingi ngoma itaingia mtaani,” alisema.
Baadhi ya wakali walioonyesha uwezo wao katika kitu hicho ni pamoja na Ndumbangwe Misayo, Charles Magali, Juma Kankaa, Chuchu Hans na Evans Komu ambao wameigiza katika kiwango cha hali ya juu huku uhusika ikiwa ni kitu cha kwanza.

NB - Promo hii nimeinyaka kwa kaka abbycool ndani ya http://abdallahmrisho.blogspot.com/

3 comments:

Anonymous said...

Bongo kwa kuiga wazungu jamani!

Anonymous said...

mdau hapo juu umesema kweli kabisa asante .roho sita-sounds like a cliche fulani hivi.Kwa kweli sitaki kuendelea zaidi ya hapa lakini It makes me wanna puke .inasikitisha -kazi yetu ni kuiga iga tuu,tena basi hatuigi kutoka kwa mastadi.Kweli kabisa roho sita ni cliche .heard it before from somewhere isipokuwa haikuwa ktk kiswahili.
Tatizo letu sisi wabongo ,ni ma-oportunists.tengeneza nyingi,fanya kama ile ya nigeria .watu wengi watannunua ,kabla wajanja wengi hajaingia,italipa.period.
Tunasubiri kwa hamu,tuione hiyo movie(video),na tutai-criticise( fairly and constractively) ili waweze kujiona na kutuelewa sisi kama fans wa sinema za nyumbani - cant be taken for a ride/fools so the next time they ever decide to make a movie wafanye home work yao better kwanza.
halafu kinachonishangaza sinema (japokuwa zipo ktk format ya video) zilitengenezwa kwa ustadi wa hali ya juu kama za bwana KIbira hazipati publicity au reviews ya sana kama hizi za kukopi wanigeria hapa nyumbani .kweli jamaa anatengeneza sinema nzuri kweli by any possible standard na hata theme zake zina resonate na issue zetu za kila siku za watanzania lakini mmmh! Sijui whatever is going on.Lakini pia on the upside ,kuwaponda tuu completely would be unfair bila kutoa credit pale wanpofanya vizuri.kwanza japokuwa ni mambo yao ya zima moto ,bwana kile kitendo tuu cha kuthubutu ,kuwa na courage ya kutengeneza filamu regrdlessly,kwa kweli ni jambo la kuwapongeza.nawapongeza kwa sababu ,regardlessly inaonyesha kwamba wana nia japokuwa aethetics na utaalamu hawana au wanao lakini hawajajua namna ya kuu-fit ktk mlolongo mzima .wanajitahidi na nina imani kabisa labda akina shigongo ,hami na kanumba leo hii kwao ni sula la inalipa na ionekana kama ya nigeria lakini vijana watakaokuja miaka ya baadaye watafanya vizuri zaidi ya hapo kutoka kwa msingi uliochwa na the likes of Kanumbas.Pili nawapongengeza kwa sababu mazingira ya kutengeneza sinema nyumbani ni magumu sana hakuna resources kabisa .It's so easy kwetu kusema tuu lakini tunajisahau kwamba wanajaribu ktk mazingira duni mno ya kisinema.Pia Muda .sanaa ya utengenezaji sinema imeingia juzi juzi tuu .naamani kwamba ni lazima watengeneze hizo mbaya kwanza kabla ya kufikia ktk top viwango .Anything takes time. Haya tunasubiri hiyo sinema tuione tuiponde -kiendelevu na tutoe sifa pale ionekanapo
USHAURI.
Folks nawaombeni mumtafute Kibira kwa ajili ya ushauri (Consultance) pindi mnapokuwa na project zenu .Kibira ni mtengenza sinema endelevu am sure atafurahi sana kupata nafasi ya kushare utaalamu wake na folks wa hapa nyumbani.Maria Sarungi anautaalamu mzuri sana ktk sinema pia wako wengine wengi tuu akina Kiyungi nk.
Jamani hivi haiwezekani kutafuta majina mengine ya utengenezaji wa sinema mpaka tuseme WOOD kama nigeria walifanya sio lazima na sisi tufanye hivyo mbona ziko nchi nyingi zinatengeneza filamu nzuri zaidi hata ya hollywood na haziitwi WOOD.Hii pia indhihirisha ni jinsi gani tusivyo creative,hata kwenye majina tuu, hoi!
NIJUAVYO MIMI
DOLLYWOOD - Ni jina la theme park inyomilikiwa na dollyparton huko tennesee marekani na imekuwa ktk bishara na jina hili kabla ya Dollywood ya kitanzania ( naomba mnisahihishe kama nimekosea)
TOLLYWOOD-Jina la film industry huko india ktk jimbo la AP zinatengenezwa ktk lugha ya Telegu
na hii pia imekuwa ktk biashara kabla ya Tollywood ya Tanzania
Hivi majina jamni yamekwisha au ni sheria au ni lazima kutumia wood? mnifahamishe wenzangu. Creativity Jamani!
Kwa heri
Sasaman

Anonymous said...

LOL...tehehehehe. hii kitu gani tena?