Monday, May 11, 2009

Tumemaliza Harlem Renaissance Play 2009

Wadau, wiki iliyopita nilikuwa kwenye mchezo wa kuigiza (tamthiliya)hapa Boston. Tulicheza May 7-9. Show ya mwisho ilijaa watazamaji mpaka ilibidi wengine wasimame. Show inahusu kipindi cha Harlem Renaissance miaka ya 1920-39. Ni kipindi ambacho wasanii waMarekani weusi walistawi Marekani na Ulaya.
Mtunzi na Producer wa mchezo, Haywood Fennell Sr. Nyuma yake mnaweza kuona mlango wa stage
Kabla sijavaa costume. Kwenye mchezo mimi niliigiza kama Mama, Bibi na Ms. Thelma.
Joe Banks (Steve Lucky) na Mwongoza mchezo Lee Smith wakitaniana

Ron Murphy (Father Africa) akipumzika Dressing Room kabla ya kwenda stage

Ona nilivyokuwa tajiri kwenye mchezo, binti Sidney ananiibia.

Ron Murphy, Ruby Hill (Bag Lady) na Charles Jackson

Ms. Thelma (Mimi) na Joe the Bartender (Charles Jackson). Kwenye mchezo Joe anampenda Ms. Thelma lakini namkataa halafu baadaye namkubali.

"Mko Tayari!" Mwongoza mchezo Lee Smith na msaisdizi, Stanley Everett (Weldon Johnson) wakihakisha wachezaji wako tayari.

Ms. Thelma
Baba Afrika (Ron Murphy) na Mama Afrika (Irene O'Bannon)

Mimi na Lee Smith (Hapo nimevaa costume ya kwanza. Mimi ni mtumwa na tunafanyakazi shambani, halafu ghafla mwanangu wa kike anachukuliwa kwenda kubakwa, naishia kulia na kuzuiliwa kwenda kumfuata mwanangu)
Mapacha Dariana na Dashiana na Nia (Katikati)

Costume yangu kwenye scenes za mwisho. Ms. Thelma amekubali kufunga ndoa na Joe.

Kwa habari zaidi someni:

http://www.dotnews.com/2009/harlem-renaissance-revisited-three-shows-lilla-g-frederick

http://oscarmicheauxrep.tripod.com/id13.html

17 comments:

Anonymous said...

Good work Dada Chemi!

Anonymous said...

Congratulations Chemi..naziona juhudi zako kila wakati niingiapo katika blog yako.

Anonymous said...

You look beautiful sister! Keep it up! You also look good with the guy hehehe!

Baraka Mfunguo said...

Dada Chemi hongera sana. Nakumbuka jinsi nilivyokuwa nasoma articles zako front page ya Daily News. Wakati huo nilikuwa mdogo hata kiingereza kusoma sijui vizuri Mama ananiambia umeona article ya Dada Chemi. Humwoni akienda pale kwa Kadete enzi hizo tuko Ubungo flats. Hongera Dada Chemi sisi tunaiga tuu lakini nyinyi ni malegend.

Anonymous said...

Hey Dada Chemi congratulations nyingi sana and thank you for sharing with us.

MOSONGA RAPHAEL said...

Nakutakia kila la heri ktk fani!

Pia napenda kukushukuru kwa kutufundisha misamiati ktk uwanja wa kuigiza. Kwa mfano, ulinifundisha maana ya neno 'extra(s)', siku hizi nikiliona au kulisikia nakukumbuka ....

Anonymous said...

Congrats Chemi. You look Fabulous!

Da N
London

Anonymous said...

Nilibahatika kuishuhudia hii "Play"
Da'Chemi alinidhihirishia kuwa mambo yake si mchezo kabisa.......
Alicheza vizuri kweli...KEEP IT UP

Chemi Che-Mponda said...

Asanteni sana. Thanks everyone.

Mzee wa Changamoto said...

Kilicho cha kipekee kwako Da Chemi ni kuwa unashiriki katika mambo haya mema na kisha unatukaribisha kila uonapo "delas" za kushiriki.
Kwa hili na kwa mengine mengi mema. NAKUHESHIMU NA KUKUTAKIA KILA LILILO JEMA.
Baraka kwako

Anonymous said...

Hongera Dada Chemi

Anonymous said...

Hongera sana Da Chemi kwa hatua kubwa uliyopiga katika kile unachopenda.

kingo said...

anti chemi hongera thanaaaa!ila anti mi ninewaona 'MAPACHA!'.

Varsity College TZ said...

Hongera Da Chemi. Unawakilisha vizuri.

Bongo Pixs said...

Big up Sis Chemi.

Anonymous said...

Chemi nakupenda

Lady Gladys said...

Dada Chemi, habari na hongera sana nakumbuka mara ya tulisafiri wote na ATC kwenda Harare,wakati ule Harare ni Harare kwelikweli. Wishing all the best.


Gladness