Wednesday, May 27, 2009

Liyumba na Kweka Waachiwa Huru!

Haya sasa!

*********************************************************
Kutoka ippmedia.com

Liyumba aachiwa huru...!

Na Kiyao Hoza
27th May 2009B

Amatus LiyumbaAliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba na mwenzake Deogratias Kweka ambaye alikuwa Meneja wa Mradi wa Majengo pacha ya BoT wameachiliwa huru leo asubuhi.

Vigogo hao wa zamani wa benki hiyo, wameachiwa huru katika mahakama ya Kisutu Jijini leo baada ya hati ya mashtaka kadhaa yaliyokuwa yakiwakabili kuhusiana na matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 221 kuonekana kuwa hayaendani na makosa yao.

Awali, kabla ya kufikia uamuzi huo, Hakimu Waliarwande Lema alisoma hukumu ya maombi yaliyowasilishwa na upande wa utetezi na kusema kuwa amefuta mashtaka ya wawili hao kwa sababu hati ya mashtaka haiendani na makosa yaliyotajwa.

Hakimu huyo akauamuru upande wa mashtaka kuandaa hati mpya ya mashtaka yatakayoendana na makosa yaliyotajwa katika hati.

Aidha, akauamuru upande wa mashtaka kuandaa upya hati ya mashtaka.

Wakati hukumu hiyo ikitolewa, uinzi katika mahakama hiyo ulikuwa mkali ambapo askari kanzu na wale waliovalia kiraia walionekana kutanda kila mahala.

Hata hivyo, baada ya kuachiwa huru, washtakiwa hao walikamatwa tena na kupelekwa katika vyumba vya mahabusu mahakamani hapo kabla ya kupandishwa kwenye karandinga aina ya Landrover Defender, lenye namba za usajili T 337 AKV.

Katika gari hilo, walipanda askari watano waliovalia kiraia, watatu kati yao wakiwa wamebeba bunduki.

Mapema asubuhi, katika viunga vya mahakama hiyo kulijaa watu wanaodhaniwa kuwa ni pamoja na ndugu za washtakiwa ambao hata hivyo, hawakudumu na furaha yao na kutawanyika baada ya ndugu zao (Liyumba na Kweka) kurejeshwa tena rumande.

Katika maombi hayo, upande wa utetezi ulidai kuwa sheria iliyotajwa katika shtaka la kuisababisishia serikali hasara ambayo iliwataka washtakiwa kutimiza majukumu yao kisheria ya kuchunguza uhalali wa malipo au majukumu ya kutoa ushauri wa kisheria kwa Menejimenti ya Bodi ya BOT kuhusu malipo.

Maombi hayo yaliwasilishwa na wakali Profesa Mgongo Fimbo mbele ya Hakimu Mkazi Hadija Msongo ambapo alisema shtaka la tatu linalodaiwa kusababisha hasara halionyeshi kosa lolote lililofanywa na washtakiwa.

Aliongeza kuwa shitaka hilo lina kasoro na halikuandikwa ipasavyo kwa mujibu wa vifungu namba 135 vya sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002.

Liyumba pamoja an Meneja wa Mradi wa Ujenzi wa Majengo Pacha ya BoT, Deogratius Kweka, wanashtakiwa kwa makosa tofauti yakiwemo matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia hasara serikali ya Sh. 221,197,229,200.95 kati ya mwaka 2001 na 2006.

CHANZO: ALASIRI

1 comment:

Anonymous said...

Walikamatwa tena palepale. waliachiwa katika ambalo nadhani linatusumbua sana watanzania TKO yaani unamfikisha mtu mahakamani mambo yanatofautiana na mashtaka kwanini hakimu asitupe kesi hiyo?