Thursday, March 18, 2010

Ray na Vincent Wanatafuta Waigizaji wa Kike Wapya!

Waigizaji wasichana wanahitajika RJ Company

03/18/2010


Kama unajihisi wewe ni mrembo basi kwa sasa tunatafuta wasanii wapya wa kike katika ofisi za RJ COMPANY zilizoko SINZA MORI. Lengo ni kuwapata wasanii wa kike ambao ni wapya katika tasnia ya filam nchini ili waje kushiriki katika filam mpya itakayoandaliwa na kampuni ya RJ. Umri ni kuanzia miaka 18 mpaka 28. Pia unaweza kutuma picha zako kabla hufika ofisini ili tuweze kukuona jinsi ilivyo.Muda wa ofisi ni saa 4 kamili asubuhi mpaka saa 12 jioni kwa siku za Jumatatu mpaka Ijumaa na siku za Jumamosi kuanzia saa 4 kamili asubuhi mpaka saa 8 mchana. HAKUNA GHARAMA ZOZOTE ZILE UTAKAZOLIPISHWA KWANI KAMPUNI INAJITOSHELEZA.

WASILIANA NA VINCENT aka RAY KUPITIA:Tel: +255 714 082729P.O. Box 11347
Email: vincentkigosi@gmail.com
Website: www.rjtanzania.com

*****************************************

Hapo napingana na Ray. Yaani watu zaidi ya miaka 28 hawawezi kuwa warembo? Angesema anatafuta kuanzia 18+. Katika sinema unahitaji waigizaji wa kila umri. Mambo ya vijana kujifanya wazee haipendezi. - Chemi

12 comments:

Fadhy Mtanga said...

Hapo umesema jambo la msingi sana da Chemi. Tabia ya vijana kuigiza kama watu wazima wakati wenye rika lao wapo haifai.
Pia filamu haipendezi tangu mwanzo hadi mwisho unakutana na vijana tupu.
Halafu kwanini wasichana tu? Wavulana wamejitosheleza?

ahmed said...

Mie kanishangaza hapo aliposisitiza kwamba hatowatoza malipo yeyote. Mbona nahisi hii imekaa kinyume yani anakusudia kwamba kama kampuni yao ingekuwa haijitoshelezi basi wangelipishwa ndio wapewe sehemu ya kuigiza kwenye filamu zao? ina maana hawatolipwa chochote hata allowance ya chakula na usafiri?

Binafsi nina ndoto siku moja nitengeneze filamu huko nyumbani, sina hata idea wanaingiza kiasi gani kwenye filamu moja, ila ninachojua kama hakuna incentives kwa hao waigiziji basi filamu haziwezi kuwa nzuri, au malipo ndio huo umaarufu wa kuonekana kwenye runinga?

Anonymous said...

Chemi wewe hujui mwenzio anajua wengi wa umri huo wana uelewa sasa atawabanaje katika mapato?

Anonymous said...

Bado sijakuelewa Chemi....hawa jamaa wanatafuta warembo au VIPAJI?

Anonymous said...

Upuuzi ndo maana sinema zao haziendi popote. Waalike watu waote wa kiume na wa kike na wa umri zote. Hao wanatafuta wachumba tu. Umewhai kusika casting couch.

Kaka Trio said...

Hilo tangazo sioni ni la ajabu hata kidogo kwani matangazo ya kazi yote TZ ni ya kibaguzi. Utakuta kampuni inatangazi kutafuta meneja lakini wanasema asiwe chini ya miaka 35 au 40, au lazima awe mwana mke. Nikiangalia CV za kibongo unaona hadi tarehe na mwaka wa kuzaliwa.

mbali na hilo inaonesha hawa jamaa wa filimu TZ wana matatizo ya kujiamini sana au wanaona aibu sana kuuliza kile wasichokijua. Kanumba alimsema ame "close" huyu Ray kwenye web yako anasema something like "Now ON stores, get your copy now" Kazi kweli kweli

Anonymous said...

Fani ya sanaa ina matatizo mengi lakini kubwa kuliko yote ni mafunzo,kwa wasanii,mafundi,waongozaji,waandishi n.k,mara zote hao wanaojifanya wataalamu wa filamu,ni watu ambao waliingia katika fani hiyo kama watu wanaojaribu maisha tu,ilipotokea wanafanikiwa kiasi wanaanza kutenegeneza njia ambazo watawapitisha wengine,katik njia hizo hizo walizopita wao na kuwanyonya kama walivyonyonywa wao,cha msingi ni kusisitiza mafunzo,kwa kiwango ambacho kitafanya filamu zetu ziweze kuingia katika maiingizo makubwa ya filamu.Ninasumbuliwa sana na hadithi za filamu zetu,jina la hadithi ni kuubwa sana unaweza kuamini kuna ujumbe mzito ndani,wapi bwana nenda kaiangalie,yaani madongolosho matupu,uigizaji matatizo,mwanga matatizo,muziki na `effects` ndio kabisa hakuna kitu,sasa jaribu kufuatilia kinachozungumzwa katika hizo filamu utagundua hao waandishi wana upeo mdogo sana wa kujua mambo na kuyachanganua,nadahni imefika wakati sasa waende shuleni kuliko kujitapa tapa,kiko iko taasisi ya sanaa na utamaduni bagamoyo inawza kuwasaidia katika uandishi na uongozaji wa filamu...filamu ni kiwanda kikubwa sana cha sanaa ulimwenguni,lakini unaingiza bidhaa gani sokoni? ndio kitu cha msingi cha kujiuliza kila wakati.

Fadhy Mtanga said...

da Chemi naomba nitofautiane kidogo na anon wa 12:15. Kiukweli sanaa ya filamu inapiga hatua japo ni kidogo. Tukisema ule ukweli kinachoangusha siyo ubora wa picha, wala mandhari wala effects. Ukitazama kwa makini filamu za Bongo utagundua kuwa wamejitahidi sana kutengeneza picha zenye ubora wa juu. Natazama sana filamu za America, Ulaya, Afrika Magharibi na Kusini.
Kwa mtazamo wangu, tatizo kubwa la msingi, ni ubovu wa hadithi. Hadithi hazifanyiwi utafiti wa hali ya juu. Kisha haziandikiwi screenplay yenye ubora. Hadithi ikashaandikwa ovyo, mchakato wote unaoendelea unakuwa mbovu. Tazama maeneo ya kitaalamu kama sheria, utabibu nk, utaona mambo yamerahisishwa mno.
Jambo la pili nionalo lina kasoro ni casting. Wanaitana wenyewe kwa wenyewe, wanapeana kazi. Unaweza kuwa mwigizaji mzuri, lakini kuna eneo usifit kutokana na hadithi ilivyo. Nadhani hilo walifanye kitaalamu badala ya kuangaliana machoni na kusema wewe kaa hapa.
Lakini siwavunji moyo, la hasha.
Nitasema kweli daima, hata hao walio juu sasa hawakuanzia hapo. Lililo muhimu kuweni makini kikazi zaidi na si ilimradi twende. Kutoa filamu kila mwezi ni tatizo kubwa ambalo hatimaye litadidimiza sanaa kwani hakuwi na ubobefu wa kimantiki na chanya katika tasnia. Mtalazimika kulipua ili kesho muanze kucheza nyingine.
Kazeni buti.
Ni hayo tu da Chemi.
Wikendi njema.

Anonymous said...

Hivi hawahitaji waigizaji wa kiume? Tumechoka kuoa sura zile zile khaa!

Anonymous said...

ndiyo yaleyale mtu ana mtoto ukimwangalia mtoto mwenyewe mkuuubwa unashangaa sasa alizaliwaje mkubwa kuliko mother au father.....alafu da chemi kuna hili jingine la kwamba movie bongo haz iuzi kama sura sii nzuri ndio unaona duh movie hii ya mapenzi nzuri kweli kweli kumbe hata wenye surA NA MAUMBO NDIO UHALISIA WA MOVIE UTAONEKANA. C

Anonymous said...

Hicho kichwa cha habari ni sahihi kweli? Mbona Ray na Vincent ni mtu mmoja?

Anonymous said...

Hilo tangazo limekaa la kutafuta changudoa ninavyoelewa mimi wacheza sinema unawatafuta kwa vipaji vyao sio sura.ACHENI KUTUMIA WASICHANA/WANAWAKE KAMA CHOMBO CHA KUUZIA FILAMU.