Monday, April 05, 2010

Ona Mambo ya Wahindi Cleveland, Ohio

Wadau hebu cheki wahindi wanavyokuza utamaduni wao huko Cleveland, Ohio. Wamefungua Bustani - Indian Cultural Garden. Wahindi wana sauti Cleveland, ns sisi waafrika tukiwa na umoja tunaweza kuwa na Sauti hapa Massachusetts. Umoja muhimu! Halafu eti hapa Boston tunasemwa na waafrika wenzetu kwa ajili ya kutaka kukutana na Gavana!


http://www.clevelandseniors.com/family/asian-indians.htm

6 comments:

Barafu said...

Hilo suala la kutaka kukutana na gavana kwa kisa tu kuwa ni mweusi mwenzenu ni ubaguzi tu, semeni msemalo. Mbona walipokuwa magavana weupe hamkutaka kukutana nao? Ukaburu tu!

Anonymous said...

kwa nini hamjengi kwenu....

Kaka Trio said...

Kazi kweli kweli. Kila mtu au kundi la watu wana haki ya kuonana na kiongozi yeyote kwa wakati wowote endapo kiongozi huyo ana nafasi au yuko tayari kutafuta muda wa kuonana na kundi hilo. Marekani Freedom of speend and expression kedekede sasa kwanini isitumiwe? mnataka weusi wa Massachusetts wasiombe kuonana na Gavana kisa mweusi mwenzao?

Barafu said...

Tatizo ni ukaburu. Alipokuwapo gavana mzungu hata siku moja hawakutaka kuonana nae. Leo yuko gavana mweusi basi watu hao msongamano kutaka kwenda kumwona, kuna nini kama si tu kutafuta kujipendekeza na kutafuta favour za kijinga? Uswahili tu, kama bongo. Swahiba wako akipata cheo kikubwa tu basi kila siku kiguu na njia ofisini kwake kwenda kumzonga na non-issues! Hilo suala la kuonana na gavana wameligundua wakati huu tu kwa vile kuna gavana mweusi? Na akija gavana mhindi, weusi mtataka kumwona au basi tu hadi awe mweusi? Ukaburu tu huu, sawa kabisa na ule wa Eugene Terreblanche!

Anonymous said...

Halafu nyie mtaweka nini bustanini kwenu mkijenga? nyerere statue?!

Barafu taratibu..... Summer hiyooo utayeyukaaa!

Barafu said...

Ndugu yangu! Wananiudhi sana jamaa na ubaguzi wao. Kila siku tunalalamikia ubaguzi wa wazungu, lakini kumbe hata sisi weusi tukipata nafasi tunataka kubagua wazungu!