Monday, March 07, 2011

Simba Hajatoroka Dar es Salaam Zoo!

Kumbe ule uzushi kuwa simba wa Dar es Salaam katoroka na anazurura mjini Dar es Salaam si kweli! Ifuatayo ni Tamko Rasmi kutoka Dar es Salaam Zoo
**********************************************************************
Habari

Napenda kuchukua nafasi hii kuwataarifu wananchi wa maeneo ya kibanda, kigamboni na maeneo ya jirani na Zoo na Dar es Salaam nzima kwa Ujumla, Kua Taarifa za kutoroka kwa kati ya Simba wetu kwenye Zoo sio za kweli.

Simba wetu wote wako salama pamoja na Wanyama wengine wote. Simba alie patikana maeneo ya Mbagala na huyo mwingine anaesemekana kuepo maeneo ya huko hatoki kwenye Zoo yetu.
Kuhusisha Dar esSalaam Zoo na wanyama hao ni Uzushi na Tetesi za mtaani.

Karibuni Sana Dar es Salaam Zoo
Akhsanteni Sana.

Mr. Salim Hassan
Marketing manager
Dar Es Salaam Zoo
+255 784 524285

2 comments:

emu-three said...

lisemwalo lipo kama halipo laja!

Anonymous said...

Ndugu yangu anilitumia SMS kuwa kweli kuna simba anatembea mjini Dar majira ya usiku.