Wednesday, May 08, 2013

Charles Ramsey Shujaa!

Charles Ramsey(43) wa Cleveland, Ohio amekuwa shujaa Marekani baada ya kumsaidia mama wa wa kizungu aliyetekwa miaka kumi iliyopita kutoroka katika nyumba ambako alifichwa.  Huyo mama ni Amanda Berry ambaye sasa ana miaka 27. Alitekwa akiwa na miaka 17 akitoka kazini.  Nakumbuka walitangaza kupotea kwake hadi hapa Boston.  Baada ya yeye na binti yake wa miaka 6 kutoroka polisi waligundua kuwa akina dada wengine wawili waliotpotea miaka mingi iliyopita walikuwemo ndani ya hiyo nyumba pia. Kwa vile walipotea muda mrefu watu walidhani wamekufa.  Kuna jamaa, Ariel Castro (52) na kaka zake wawawili waliokuwa wanawaficha na kuwabaka na kuwafanyia matendo ya ajabu! Baba wa mtoto wa Amanda ni Mzee Ariel.

Hao akina Castro wana asili ya Puerto Rico na MaRican wenzao wamekasirika na kusema wamewaibisha vibaya sana!  Wanyongwe!

Kwa habari zaidi BOFYA HAPA:


2 comments:

Anonymous said...

Huyo ni ghetto bro! Lakini kafanya kitendo cha kishujaa.

Anonymous said...

From zero to hero. Jamaa keshakuwa shujaa.