Wednesday, May 29, 2013

Mwanamke Auawa na Majambazi Dar

Hii ilitokea Mei 5, 2013 Mjini Dar es Salaam
 
 
 
 
Majambazi yamempora mama mmoja kiasi cha shilingi milioni kumi na kutokomea kusikojulikana....

Tukio hilo limetokea leo saa 5:16 jioni na inavyosemekana ni kuwa mwanamke huyo alikuwa akitoka benki ya CRDB tawi la Uhuru ambapo majambazi yakiwa na pikipiki yalikuwa yakimfuatilia..

Alipotoka ,majambazi hayo yalimfuata na kuligonga gari lake makusudi na ndipo dada huyo aliposimama ili angaalie nani kagonga gari yake ambapo jambazi mmoja alishuka na kumpiga risasi ya kifuani na kutokomea na kiasi hicho cha pesa. ..

4 comments:

Anonymous said...

@ Chemponda...Hiyo habari ni ya kitambo!!

Anonymous said...

Hiyo habari ni ya kitambo!!!

Chemi Che-Mponda said...

Iliokea lini? Mimi niliona kwenye blog fulani inasema 5/5/13.

Anonymous said...

Hiyo ndio Tz ya hivi sasa, mambo kama hayo imekuwa kitu cha kawaida hapa kwetu bongo, hakuna kabisa usalama hao majambazi wameua na kutokomea mchana kweupe na hakuna mtu wala serikali kufuatilia uhaini huo. Hilo tukio limetokea mchana mbele ya kadamnasi ya watu lakini kila mtu alietazama adhana hio kakaa kimya kwani majambazi wale wana silaha zaidi ya askari wa vita wa kitanzania , na utawala wa ndugu yetu ndio hivyo tena hauna makali hata kidogo YAANI WANAJIFANYIA LOLOTE WAKIAMUA KWANI HAKUNA SEREKALI YA KUSEMA CHOCHOTE hio ndio bongo TAMBARALE YETU

wee acha tu hayo matukio ni ya kila siku mpaka imeasha zoeleka. KWA KWELI TANZANIA INATAKIWA SEREKALI NYINGINE