Wednesday, July 17, 2013

Picha za Kijana wa KiChina Aliyeponyeshwa na Askofu Kakobe

Haya wadau, picha hizi hapa za kijana wa kijana aliyekuwa hawezi kutembea anatumia wheelchair,  aliyeponyeshwa na Askofu Kakobe mwezi uliyopita kwenye Mkutano Toronto, Canada.











21 comments:

Anonymous said...

Iko kazi.

Zone 6 said...

mdau wa kwanza juu kabisa; na tena kazi yenyewe siyo ndogo.

Anonymous said...

Wangetuonyesha, medically, kwanza kwamba kweli hatembei!

Anonymous said...

Askofu Kakobe kweli ni mtumishi wa Mungu!

thomas said...

hawa jamaa wanatumia watu kutoa ushahidi wa uongo, kuna kesi nyingi sana huku afrika kuhusiana na uongo wa hao wanaojiita manabii, wanawalipa pesa watu ili wajifanye vilema...tumechoka kufanywa wajinga!!!!

thomas said...

wizi mtupu!!!

Anonymous said...

Aliyemponyesha ni BWANA YESU sio askofu kakobe

Anonymous said...

Believe this and you'll believe anything.

Anonymous said...

huyo kakobe baba yangu aliabudu kwake miaka mingi, baba alikuwa mzee lakini aliweza kufunga siku saba mpaka kumi bila kula wala kunywa maji, wakikaa kanisani na kakobe, wakimaliza wanapewa supu eti imetayarishwa na mahoteli maarufu, kakobe akimwona mzee wangu mtu muhimu kanisani, kila wakifunga tulikuwa tunasali maana siku ya kumi hata kutembea mzee alikuwa hawezi na kakobe hajali unakaa mbali shauri yako,sielewi kilichotokea ila mzee wangu aliumwa karibu mwaka mzima kakobe hakujali hata kutuma watu kuja kumwona na kumwombea mzee hadi alipofariki na hakuja hata kwenye mazishi, waliokuja kulala msibani walipewa adhabu, huwa watu wanapewa adhabu pale mwenge ila ni amini huwezi sema adhabu unazopewa na kinachoendelea, akisafiri kanda tu huwekwa hakuna mtu wa kuchukua jukumu la kuhubiri madhabahuni hadi arudi,inauma sana mzee wangu kutumikishwa na kakobe na asimjali wakati anaumwa hadi kufa sielewi kulitokea nini Mungu ndio anajua na sasa mzee wangu anapumzilko la milele baada ya utumishi wa uaminifu, samahani nimeenda nje ya topic

Anonymous said...

Wachina wengi ni njaa kali na sishangai kuwa wameshiriki katika tukio hili la kuwahadaa watu.

Anonymous said...

Bwana Yesu asfiwe sana. Kazi anayofanya askofu Kakobe si ndogo.

Anonymous said...

Tatizo ni kwamba wajinga wameamini uongo huu kwa miaka mingi sana. Sasa kukubali kwamba wamedanganywa kwa miaka mingi inawauma sana, na wanatamani wanachoamini kiwe kweli. Sasa imefika mahali wanakuwa "pathological compulsive liars" kwamba wanaamini uongo wao wenyewe. Kuna kakobe mmoja wa kenya alikuwa anawanya wagumba wanazaa. Waingereza wakatuma undercover believer wakagundua anawaiba watoto wa wazazi wengine nairobi hospital na anawapa waumini wake. wazazi wanaambiwa watoto wao wamefariki.

Anonymous said...

Halleluyah! Asante Askofu Kakobe!

Anonymous said...

I just don't believe any of this healing miracle stuff. Whatever happened to BabuKikombe? Fake fake fake!

Anonymous said...

Ni kweli wewe umeenda nje ya topic. Ila kwani Baba yako alikwenda kumtumiakia kakobe au Mungu?,Baba yako alifunga kwa manuafaa ya kakobe au kuutafuta uso wa Mungu?
Baba yako na wewe walikuwa na mtazamo mbaya ndio maana akaumwa na kufa maana alimfanya kakobe kuwa ndiye Mungu, hilo ni kosa ambalo watu wengu hulifanya kwa kuwaona watumishi kama miungu watu.
Halafu hii tabia ya kulala msibani mbona imepitwa na wakati?

Anonymous said...

sawa anony wa 23rd 7.15 baba yangu ni kati ya wazee waliokuwa kwenye serikali ya Nyerere walipostaafu ni watu waliopigika wengi walistaafu wakiwa maskini wa kutupwa hawakuona umuhimu wa kuiibia serikali yao wengi ndio wakakimbilia makanisani humo mpaka hilo la kakobe, inawezekana alikuwa anamwabudu na kufunga kwa ajili ya kakobe kama ulivosema mpaka akafa mi sielewi ila hajawahi kutueleza kuwa alifanya hivo. mi sijawahi kuabudu kwa kakobe,kulala msibani si ajabu kwa binadamu vijijini hadi mijini kwa ajili ya watu kufarijiana, wewe unasema imepitwa na wakati kuna mawili hujakutwa na shida kama hiyo au u MCHAWI au we ndio kakobe mwenyewe,maelezo yenye kaushetani fulani haiwezekani ukae na maiti peke yako ndani na kuzika unazika mwenyewe?mi namwabudu YESU Mungu alie hai upo hapo?

Anonymous said...

Sio ajabu watu kupinga miujiza inayofanywa kwa Jina la Yesu kupitia Mtumishi wake Zachary Kakobe.

Kama watu walimpinga Yesu mwenyewe na kuipinga miujiza aliyokuwa akiifanya na kusema kuwa ni ya uongo hata wengine wakadiriki kusema kuwa Yesu ni pepo (shetani) na anatoa pepo kupitia Beelzebuli mkuu wa pepo (Yohana 8:48-49, Mathayo 12:22-24). Sasa kama Yesu aliambiwa hayo hakuna cha ajabu kwa Kakobe kuambiwa maneno kama hayo.

Mungu atahukumu kila neno tunalolinena wanadamu.

Anonymous said...

Ni zahiri kuwa YESU ni jembe ki ukwelii

Anonymous said...

BWANA YESU ASIFIWE KWA KWELI MACHOZI YAMENITOKA! KWENYE BIBLIA KUNA SEHEMU INASEMA WATU WATAKUWA NA MACHO NA HAWATAONA! KWELI KUNA MANABII WA UONGO NA MANABII WA UKWELI DUNIANI HATA KWENYE BIBLIA INASEMA!MIE NILISHUHUDIA NDUGU YANGU KABISA TUMETOKA NAYE NYUMBANI TUNAMUUGUZA ALIKUWA HAWEZI KUTEMBEA ILA KWENYE ILE MIKUTANO YA JANGWANI AKAPONA KWA JINA YA YESU KWAHIYO TANGU SIKU HIYO NAAMINI YESU ANAPONYA FYI.KALAGHABAO

Anonymous said...

Hao wanaomkosoa Kakobe, hawajui walisemalo ni miongoni mwa watu wapumbavu ambao hata ukiwaelimisha hawawezi kuelimishika.

Anonymous said...

Lakini kiukweli mimi binti yangu aliugua kama kichaa au kuchanganyikiwa hivi. Nilikwenda makanisa yote ya uponyaji hawakuweza. Nilikwenda kwa kakobe aliifanya kazi hiyo vizuri na binti yangu hadi leo ni mzima. Sikutoa hata shilingi moja. Mimi ni mwandishi wa habari wa siku nyingi, anayebisha aje Global Publishers kuniulizia nimuambia. Mimi siyo muumini wa kanisa hilo, lakini mwanangu aliponywa pale. NAMSHUKURU SANA kwa sababu nilihangaika sana hata Hospitali ya Kariuki na MAMA NGOMA nilifika, hakupona. Ni hayo tu kwa leo.