Thursday, July 04, 2013

President Obama Over Kenyan Airspace - Utani


6 comments:

Anonymous said...

No Comments

Anonymous said...

Aiseiiii!

Anonymous said...

WEE ACHA TU SASA HAWA KINA OMERA SI WATATUANZIA MABALAA YAO? NA HUYO OBAMA WAKO, WABONGO KAENI MKAO WA KULA

Anonymous said...

duh wadanganyika kweli mburulaz tu. aliekwambia kwamba Obama kajaa tz kimapenzi nani?katumwa na ma boss wake makaburui aje kusaka gesi bongo kaona huu Jintao keshatia timu bongo kwa sana. kajaa nae kuomba mabaki ya mikataba jamaa anatembea ki maslahi tu hamna cha mapenzi walaaa nini ela kwanza. mshakaji mzungu kune ngozi nyeusi kaisaidia nini afica tangu alivoingia madarakani hamna.wamarekani na wa Europa watakula jeuri lao kutuibia watuibie afu dharau tena no way. biashara tunahamishia china wao hata kama wachukue hawana dharau. MDAU MPENDA AFRICA KWA SANAA TU; NAOMBA USBANIE COMENTI HII DA CHEMI FREEDOM OF SPEECH

Anonymous said...

Kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii, watu wamekuwa wakiwakashifu sana waandishi wa habari wa Tanzania eti "Kwa kushindwa kuuliza maswali mazuri" kwenye mkutano wa marais Obama na Kikwete. Ukweli ni kwamba, waandishi wa Tanzania hawakupewa fursa ya kuuliza. Mchagua waulizaji (pengine ndiye aliyepanga maswali pia !) hakutoa fursa kwa waandishi ambao pengine wangeuliza maswali magumu. Kulikuwa na nafasi ya maswali mawili na waulizaji waliteuliwa na Msemaji wa Ikulu ya Tanzania..... Mlitaraji nini kutoka kwa Wana Habari wa Tanzania kwenye mazingira hayo? Halafu kuna suala la Kiingereza, kwamba waandishi wa Tanzania hawajui lugha hiyo na hivyo hawafai. Tunapimana sana uzuri au ubaya wetu kwa kuangalia ni nani anazungumza Kiingereza kizuri. Tatizo ni kwamba hatujawahi kuchekana kwa kuzungumza BROKEN CHINESE wakati sote tunajua kuwa miaka 20 ijayo, CHINESE inaweza kuwa lugha muhimu ya mawasiliano kuliko hata hiki Kiingereza tunachojisifia kwa sasa. Labda kwa sababu mimi sijui Kiingereza lakini kuna sababu gani ya kuchekana au kudharauliana kwa sababu ya kuongea kiingereza kibovu? Nafananisha tabia hii na ile ya wakati wa utumwa ambapo mtumwa aliyepangiwa kazi ndani ya nyumba (domestic slave) alijiona bora kuliko yule wa nje. Kama ujumbe umefika, ya nini kuchekana?

Anonymous said...

Kuna UFAHARI gani kwa taifa huru kutembelewa na kiongozi wa Taifa jingine, kwamba watokee wa kujiona DHAIFU kwa sababu tu Obama hakufika Kenya? Inaingia akilini ama ni KULOGWA kunakotokana na imani ya kufanyika kuwa WANA WA WATUMWA wanaouishi UTUMWA?

Waafrika inafikia hatua hiyo? Hivi tunajua jinsi Marais tuliowachagua kwa mfumo wa kidemokrasia kama wanavyochaguliwa wa mataifa makubwa ikiwamo Marekani, wanavyopokewa wanapokwenda kwa 'mataifa makubwa'??? Tunazijua ishara za udhalilishaji, kejeli na fedheha wanazokutana nazo! Tunajua jinsi wanavyoumia mioyoni mwao kila wanapozifikiria heshima 'wanazomwagiwa' wawapo katika nchi zao za Kiafrika, ikilinganishwa na wanapokuwa kwenye 'mataifa makubwa'

Uchaguzi wa Kenya, moja ya nchi za Afrika Mashariki (EAC) ulitoa sauti ya Waafrika wa Kenya, ikiakisi hitaji la Waafrika wa Kenya walioichagua serikali ya Waafrika wa Kenya. Mlitaka Wakenya wakidhi matakwa ya 'mabwana wakubwa'? Haipaswi kuwa hivyo.

Msimamo wangu upo katika kuwapongeza Wakenya, kwa Rais Uhuru Kenyatta na Makamu wake, William Ruto, hata walipotangazwa kwenye orodha ya 'Ocampo Six', waliendelea kuielezea azma yao kuwania Urais. Waliizunguka Kenya, wakajieleza kwa Wakenya na kueleweka kwa Wakenya. Kwani wakenya walikuwa wajinga, wasiwaone kuwa ni 'wauajia na wabakaji' hata wakawachagua kuwa viongozi wao?????

Iweje sasa hoja kwamba kutokwenda kwa Obama huko Kenya iwe majuto kwa Wakenya?

Watavimba, watapasuka, Kenya itabaki kuwa ya Wakenya na viongozi wa Kenya watatokana na kuchaguliwa na Wakenya. Aende ama asiende Obama, Kenya itaendelea kuwapo.