Saturday, April 07, 2012

Ukiwa mwaminifu wa mapenzi, wewe ni "zoba"... Kifo cha Kanumba

Da Subi anatoa maoni yake juu ya kifo cha msanii maarufu wa Tanzania, Steven Kanumba, aka. Kanumba the Great aka. Denzel Washington wa Tanzania.
****************************************************************
 
Picture
Ikiwa ni kweli kuwa kifo cha Steven C. Kanumba, aliyekuwa mwigizaji maarufu wa filamu na sinema, kimesababishwa na ugomvi wa mapenzi uliotokana na kukosekana uaminifu, basi kauli niliyoitoa hapo juu ambayo nimeinukuu kwenye "zilipendwa", wimbo wa "Kadiri Kasimba" una ukweli na, waliotutangulia si wehu. Waliyaona! Wakatuasa. Tunajifunza?

Juzi hapa msanii "Diamond" kwenye mahojiano na CloudsFM kuhusu Wema Sepetu, aliyatamka maneno haya, "ku-cheat katika mapenzi ni kitu cha kawaida" bofya hapa kusikiliza kiwa huamini.

Si kwamba ninaamini takwimu finyu ya mtu mmoja na kuichukulia ya jamii nzima. Hapana.

Na si kwamba siamini maneno hayo au ni jambo geni sana kwangu, hapana.

Kilichonistusha ni kusema, "ni kitu cha kawaida"... kwamba ni kawaida tu kusalitiana kwenye mapenzi. Kwa vile aliyeyatamka ni msanii kioo katika jamii, sina uhakika kama ndivyo ilivyo kwenye ulimwengu wao wa wasanii au kwa vile anaishi katikati ya jamii na anawasiliana na wanajamii wengi, basi ameyaona hayo kila pahala, kwa hivyo imezoeleka na hakuna haja ya kustuka wala kushangaa usaliti unapotokea kwenye mapenzi.
  1. Tamaa - kushindwa kuzizuia tamaa zako za hali (mwili, muonekano, wasifu n.k.) au tamaa za mali
  2. Vishawishi - kushindwa kuzuia vishawishi vinavyoletwa kwako na wengine kwa njia ya tamaa (tizama namba 1) zao kwako.
Mengine yote yanayoufauta baada ya hapo kwa kweli ni sababu au visingizio vya kabla au baada

No comments: