Friday, February 22, 2008

Uzinduzi Rasmi - Bongoland II





Moja kwa moja kutoka mjini Dar-Es-Salaam, tunafurahi kutangaza siku ya uzinduzi maalumu wa sinema ya Bongoland II. Tarehe ya uzinduzi ni mwezi April 5, 2008 hapa mjini Minnepolis, Minnesota katika ukumbi wa sinema wa Oakstreet Cinema.

Sinema hii ilitengenezwa mwaka jana July pale mjini Dar. Vitongoji maarufu vya mji huo kama Manzese na Magomeni vilitumika katika utengenezaji wa sinema hii. Kusema kweli, hii itakuwa ni hadhi kubwa ya wasanii wa ki-Tanzania maana sinema hii itaonyeshwa katika tamasha mbali mbali za sinema za kimataifa.
Sinema hii ni inamhusu Juma Pondamali ambaye baada ya maisha na malengo yake kutofanikiwa nchini Marekani, aliamua kurudi nyumbani. Lakini visakato alivyovikuta nyumbani vilimshangaza sana na hakuna kitu chochote hapa ulimwenguni ambacho kingemtayarisha kupambana na visakato hivyo.ANGALIA TRELA MPYA

Jitayarishe kuwaona wacheza sinema wakongwe wa Tanzania kama Mzee Kipara, Bi Chuma Selemani Mzee na Bi Thecla Mjatta. Vile vile pia kuwaona wachezaji chipukizi kutoka mjini Dar-es-salaam.
Msanii mhusika mkuu ni Peter Omari ambaye anacheza kama Juma. Peter, ambaye kwa sasa anishi Mwanza, aliwahi kucheza katika sinema yetu iliyopita iliyoitwa TUSAMEHE.

2 comments:

Anonymous said...

Tunangojea kwa hamu! Safari hii Kibira kajitahidi kweli!

Anonymous said...

Looks Good! Big Up Kibira and Crew!