Wednesday, June 27, 2007

Mheshimwa Amina Chifupa atazikwa Njombe


Ama kweli kifo cha Mheshimiwa Amina Chifupa kimegusa wengi. Jana nimeshinda kwenye simu na neti kwenye e-mails naongea na watu kuhusu kifo chake. Kifo chake kimegusa wengi.

*********************************************************************

From ippmedia.com:

Wabunge kibao waangua vilio

2007-06-27

Na Emmanuel Lengwa, Mikocheni


Kama kuna siku ambayo Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limegubikwa na simanzi, basi ni leo asubuhi wakati Spika, Samweli Sitta alipowatangazia wabunge kwamba mwenzao, mheshimiwa Amina Chifupa, amefariki dunia.

Baada ya taarifa hiyo, wabunge wengi walishindwa kujizuia na kuanza kuangua kilio waziwazi. Mbunge Jenista Mhagama, Aziza Sleyum, Martha Mlaka na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Margareth Sitta ni miongoni mwa wengi waliokuwa wakibubujikwa machozi waziwazi na kuwalazimu wabunge wengine kujipa ushujaa wa kuwafariji muda wote. Vilio hivyo na simanzi vilishika kasi zaidi wakati wabunge wote walipotulia vitini ili kumsikiliza Spika wa Bunge, Mhe. Sitta wakati akiendelea kueleza utaratibu unaofuata.

Kadhalika hapa Jijini Dar, nyumbani kwao marehemu Amina, vilio vilitawala huku ndugu na jamaa wakiwa hawaamini kama kweli mpendwa wao amewatoka. Alasiri ilipotinga nyumbani kwa baba wa marehemu, Brigedia mstaafu Chifupa, Mikocheni Jijini leo asubuhi imemkuta aliyekuwa mume wa marehemu pamoja na na familia yake, wakiwa katika majonzi makubwa.

Akizungumza na Alasiri, Bw. Mohamed Mpakanjia, amesema mazishi ya aliyekuwa mkewe yanatarajiwa kufanyika kesho huko wilayani Njombe. ``Tutaondoka kesho kwenda Njombe kwa mazishi? leo tunatoa fursa kwa ndugu, jamaa na marafiki na wananchi wa waliopo Jijini Dar ili kuweza kumuaga kabla ya kumsafirisha,`` akasema Bw. Mpakanjia.

Bw. Mpakanjia amesema ikiwa ratiba itakwenda kama ilivyopangwa, baada ya wabunge kutoa heshima za mwisho, mwili wa marehemu utaondoka kwa ndege kuelekea Njombe ambako utazikwa kesho,? akasema. Kabla ya kifo chake, Mheshimiwa Chifupa anakumbukwa jinsi alivyokuwa akitoa hoja kadhaa nzito nzito bungeni.

Marehemu alikuwa akiwashangaza wengi kutokana na ujasiri wake wa kuibua mambo mazito kama yale ya kujitolea kuongoza mapambano dhidi ya biashara ya dawa za kulevya waziwazi, jambo ambalo wazoefu wengi wamekuwa hawaonekani kulifanya.

Pia alikuwa mstari wa mbele katika kutetea maslahi ya vijana, kukemea rushwa na kupigania haki za wanawake.

Historia ya mbunge huyo aliyekuwa miongoni mwa waheshimiwa wenye umri mdogo zaidi katika bunge la sasa inaonyesha kuwa amepata elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Ushindi ya Jijini, kisha akajiunga na shule ya sekondari ya Kisutu. Alipomaliza kidato cha nne, Amina Chifupa alijiunga kidato cha tano katika Shule ya Sekondari Makongo kabla ya kuhitimu na kwenda kujiunga katika Chuo cha Uandishi wa Habari cha Royal College cha Jijini Dar es Salaam. Inaonyesha historia yake kuwa tangu akiwa shuleni, marehemu Amina alishaanza kazi ya utangazaji wa redio. Mwaka 2005, Amina Chifupa alitwaa ubunge baada ya kufanya vyema katika uchaguzi mkuu kupitia tiketi ya viti maalum (Vijana-CCM).
Hadi anafariki dunia jana usiku, marehemu Amina Chifupa alikuwa na umri wa miaka 27.

Tuesday, June 26, 2007

Mheshimiwa Amina Chifupa Amefariki Dunia!




Nimepata habari muda huo kuwa Mheshimiwa Amina Chifupa amefariki dunia katika Hospitali ya Lugalo, Dar es Salaam. Nilipiga simu nyumbani kwa wazazi wangu Dar na kuambiwa kuwa walitangaza kwenye television na walikatisha kipindi cha Rebecca kusudi wa tangaze.

Mungu amlaze marehemu Amina mahili pema peponi. Amin.

Amina, ulikuwa shujaa kwa wanawake wengi, tutakukosa, Mola amekuchukua mapema mno. Ninalia pamoja na ndugu zako.
*******************************************************************

Comments za Baba mzazi wa marehemu kwenye Michuzi blog:
MH. AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIA HATUKO NAYE TENA. KWA MUJIBU WA BABA YAKE MZAZI MZEE CHIFUPA (PICHANI) AMBAYE NIMEONGEA NAE DAKIKA TANO ZILOPITA, HAYATI AMINA AMEFARIKI SAA TATU KASOROBO USIKU HUU HOSPITALI YA JESHI YA LUGALO ALIKOKUWA AMELAZWA. MAKELELE YA VILIO YALITAWALA MAZUNGUMZO YETU KUTHIBITISHA HABARI HII YA KUSTUA.

Safari ya Boti



Nimeona hii picha ippmedia.com leo. Caption ilisema kuwa ni wakazi wa Dar es Salaam wakienda kustarehe Bongoyo Island, kwenye boti iiliyotoka pale Slipway Dar.

Picha ni nzuri lakini iliniaacha na maswali. Mbona wazungu tu wamevaa lifejackets? (vifaa vya kuokoa maisha). Bila shaka hizo lifejackets ni zao binafsi. Na mawimbi hayo, duh! Ama kweli watu wameweka maisha ya mikononi mwa malaika. Lifejackets ni muhimu kama unasafiri kwenye boti na kwa bahati mbaya inapinduka au inazama. Maana unaweza kuelea kwenye maji kwa muda hata kama hujui kuogelea. Mara nyingi watu wanazama shauri ya uchovu kama hawajivaa.
Nakumbuka miaka ya nyuma Tanzania, maboti kadhaa yalipinduka na watu walikufa maji shauri ya kutokujua kuogelea na kuzama. Hata boti zilizama Lake Victoria na Lake Nyasa na watu kadha walipoteza maisha yao. Watu wangepona kama wangekuwa wamevaa lifejackets.
Na hata ukipanda kwenye ndege kitu cha kwanza wanakuambia hizo lifejackets ziko wapi kama kwa bahati mbaya ndege inaanguka kwenye maji.

Sidhani kama kuna sheria inayolazimisha hao wenye boti wawe na lifejackets za kutosha kwa ajili ya abiria yao. Na huenda ingekuwa ghali sana kwa hao wenye boti. WaBongo tuna maarifa lakini na hata dumu tupu inaweza kusaidia kuokoa maisha maana inalea kwenye maji.l
Lakini Mungu yupo na atatulinda. Ni kuomba kabla hujaingiwa kwenye boti.

Mjue Msanii Thecla Mjatta

Thecla Mjatta in Arusi ya Mariamu
Thecla Mjatta at a screening of the film, Tumaini
Thecla Mjatta (in baibui) with other cast of the film, Mlima Kolero
(photo from Jiachie blog)


Mama Thecla Mjatta ni mwigizaji mkongwe wa Tanzania. Huenda mnakumbuka zile michezo za kuigiza kwenye redio. Tulikuwa tunazingojea kwa hamu kila wiki, hasa kwa vile wakati huo hakuna TV miaka ya 70 na 80. Pia aliigiza katika michezo ya kuigiza kadhaa.

TV ilivyoanza alianza kuigiza kwenye michezo ya television. Mama Thecla pia ameigiza katika sinema kadhaa na kucheza kama watu ambao hamwezi kusahau.

Katika sinema ya Arusi ya Mariamu, anaigiza kama shangazi yake Mariamu, na hamtasahau anvyopagawa.

Katika sinema ya Maangamizi the Ancient One aliigiza kama mama wa mhusika mkuu, Samehe. Samehe, alishuhudia kifo cha cha kuunguzwa na moto na baba yake mzazi amabaye alikuwa ni mchungaji mwenye imani kali ya dini. Sinema ya Maangamizi iliteuliwa kama sinema ya kwanza kutoka Tanzania, katika mshindano ya Oscars mwaka 2001 (Foreign Language category).

Pia ameigiza katika sinema za Simu ya Kifo, Tumaini, Mzee Mkude, na mlima Kolero. Hivi karibuni ataigiza katika sinema ya Bongoland II, akicheza kama mama yake mhusika mkuu, Juma.

Kwa habari zaidi za sinema ya Bongoland II nenda : http://www.kibirafilms.com/bongoland/home.html

Monday, June 25, 2007

UGALI



Mwandishi Sandra A. Mushi ametoa hadithi mpya. Hadithi hiyo inaitwa ' The Plate of Ugali' (sahani ya ugali). Hadithi hiyo hasa inahusu mambo ya kunyanyaswa kwa mwanamke na mume wake (domestic violence). Imeandikwa kwa kimombo (English).
Hivi karibuni niliandika blogu kuhusu Sandra na bidii yake ya kutunga hadithi na mashairi. Mnaweza kusoma hapa: http://swahilitime.blogspot.com/2007/06/mjue-sandra-mushi.html
Pia tembelea Authors Den:
- http://authorsden.com/sandraamushi

*************************************************************************************


The Plate of Ugali




Read more stories by this author

It was one reason after another – as long as I was his punching bag – and almost always it was a plate of ugali that started it. Yep, his source of strength. Like the hair on Samson in the bible. Maybe ugali makes one mad. Maybe it had a drug.


My mama used to say a real African man doesn’t eat chips or pasta. That’s food for a mzungu man who gets his nails manicured, his face scrubbed and his lips conditioned with lip balm. A real African man eats ugali, my mama used to say. With their calloused fingers with rough nails he would mould the stiff porridge into little balls, dunk each ball into a stew then dunk the stew covered ball into mouth with chapped lips.

I would sit at the corner of the room watching his Adam’s apple bopping up and down as he swallowed a ball of ugali and meat stew. His jaw always moving in super-human speed as he chewed, making the vein on his forehead pop out angrily.

Ugali would make your man strong, my mama used to say. Strong enough to take care of you and our family, she would add. What she didn’t add was that ugali would make him strong enough to beat me black and blue. But maybe she was always right, because it was a plate of ugali that gave me strength today.

It had started with his plate of ugali not being warm enough. Then the following time he beat me black and blue it was because the bowl of stew did not have enough meat. The other times before that it was the disciplinary slap, as the elders called it. Married women needed the slap every now and then, they would say, to keep them in check.

Then he beat me again black and blue when I failed to pound his kisamvu the way he liked it. I had been vomiting the whole day; infact even getting up was a problem.

“My mother dug a whole farm the day she was giving birth and you say you can’t cook for your husband?” He had bellowed. “What kind of a woman are you?”

“But mume wangu, the doctor said …” lamenting, I had tried to explain before I was interrupted by a slap. The room started spinning around me.
“Has the doctor married you?” He gave me another slap which sent me reeling to the floor vomiting blood, “is the doctor your husband now? Or are you having an affair?”

My baby did not make it. I almost did not make it too. I broke a few bones and I almost became blinded on my left eye.

After that I became numb to the pain. It was one reason after another – as long as I was his punching bag – and almost always it was a plate of ugali that started it. Yep, his source of strength. Like the hair on Samson in the bible. Maybe ugali makes one mad. Maybe it has a drug.

Today he broke my two front teeth – after breaking four others last week. I laugh madly as I looked at four year old with his milk teeth missing. He grins at me nervously showing his gums.

Today he beat me because I refused to serve his mistress a plate of ugali. Like my body numbing to pain, my heart had numbed to reason. Maybe it was my fault when the plate of ugali wasn’t warm enough because I had run out of cool to warm the food; maybe it was my fault when I didn’t negotiate with the butcher to give me more meat than the money could buy; maybe it was my fault that I was too lazy too pound cassava when I was due; maybe it was my fault when I had used to the last of the flour to cook my baby porridge for lunch instead of cooking him his ugali; maybe it had all been my fault. But how could this be my fault? My mama told me my husband came first, then my children.

I had put some food aside for my husband, the fed the remaining to my children. How was that my fault? I never said anything when he brought her and moved me out of our marital bed. I said nothing.

He kicked his plate of ugali when there wasn’t enough for his mistress and made me eat from the floor after beating me black and blue - wounding the scars that had no even healed. On all fours I bent down and ate like a dog. As I lay clutching my stomach I see the mouse that I have been trying to catch for a while, rushing to the last crumbs of ugali on the floor. No amount of rat poison seemed to kill it. Rodent. Maybe I had been giving it the poison with the wrong food. Rodent. Rodent. I should have mixed the poison in ugali. Rodent. Or is it rodent and man. Rodent man. Kick. Rodent man. Kick. Rodent man, I think.

I feel humiliated when I hear her cheering him on. It was okay before, as I probably needed disciplining. But it’s not okay now. She is not supposed to be here, cheering on. But the ugali gave me strength.

“Stupid woman! Go make another plate,” he had kicked me on the shins as his mistress laughed again, louder this time. “And make it enough to give us strength for the work ahead of us tonight!”

Ugali has given me strength too. I look down as I limp to the back yard. I don’t want them to see my face. The smile on my face. Yes, ugali has given me strength.

Quickly I grab a khanga to hide my new scars, covering myself I dash to my neighbour to borrow me some money from her. Just as quickly I send my oldest to the market. Flour, kisamvu, coconut, curry powder, peanuts, nyanya chungu and some powder that will kill that rodent. Today I will make the best plate of ugali ever. The kisamvu will have peanut sauce and the dagaa will have coconut milk and nyanya chungu. Today I will catch that rodent with a plate of ugali for sure.

Sunday, June 24, 2007

Jamani mbona mmetukana!

Nimepokea hii story kwenye e-mail. Sijui kama ilitokea kweli, lakini naweza kuamini ilitokea. Watu wakianza kutamka lugha ambazo si zao wanatukana bila kujua.

Nilisimuliwa visa hivi viwili:

- Mchungaji wa kutoka kanisa fulani Ulaya, alifika kwenye hoteli fulani Mwanza. Naye alikuwa amejifunza kiswahili kabla ya kutua Bongo. Alipofika Reception akawasalimia wahudumu pale vizuri halafu kasema:

Father Mzungu - Naomba Mchumba

Receptionist - (Kashutuka kweli) Heh! Unasema nini?

Father Mzungu - Nimesema nataka Mchumba

Receptionist - (wakati huo na wafanyakazi na wageni wengine wanamtazama kwa mshangao wakidhani anataka changudoa) Dada mwenyewe kashindwa aseme nini.

Father Mzungu - Ndiyo nina mchumba. Mchumba yupo leo?

Ndo hapo kaingilia mgeni na kumwuliza kwa lugha yake alitaka nini. Kumbe mzungu alitaka chumba cha wanaume.

**********************************************************************

Wajapani wawili walifika pale Embassy Hoteli Dar na kujiandikisha Reception.

Wale wapokezi wakashindwa kutamka majina yao.

Yalikuwa - Mr. Kumamoto na Mr. Takeuchi!

Kumamoto pia ni mji huko Japani. Na wana majina yanayofanana ya Bongo, kama Maeda

*************************************************************************
Na hii nilishuhudia mwenyewe nikiwa mwandhis wa habari Daily News.

WaJapani walitoa msaada sehemu fulani miaka ya tisini. Sasa siku ya kuzindua mradi akaja mtu mzito kutoka wizara iliyohusika na mradi. Alishindwa kutamka jina la mgeni kutoka Japani, naye alikuwa anaitwa Mr. Kumamoto. Yule mzito wa wizarani alimwintroduce kama 'Rafiki yetu kutoka Japani' .

^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^

E-mail enyewe ndo hii:

Ifuatayo ni sehemu ya hotuba ya Mfadhili (Mzungu) wa mradi wa maji safi huko katika kijiji cha Mkomazi, Mkoani Tanga.

Mfadhili huyu kutoka ubalozi wa nchi moja - Majuu amewahi kujifunza kiswahili kwa muda wa miezi mitatu hivyo kutohitaji kufuatana na mkalimani wa ubalozi.

Alikuwa na hayamachache:

>Mzungu: Jambo wanakijiji wa Mkuma Wazi?

(akimaanisha Mkomazi)

> Watu walibaki kumtumbulia macho na kujikausha wengine

Wakicheka kichini chini. Mzungu akadhani amepatia sana lugha ya kiswahili, akazidi kujitutumua:

Leo mimi na uke yangu (mkewe!)tumekuja hapa Mkuma wazi kukagua

mitombo ya mboo zenu inayoendeshwa kwa nguvu ya pepo

( Mitambo ya mbao inayoendeshwa kwa nguvu ya upepo!)

na Visimi yenu inatoa maji(Visima jamani!).

Mitombo hii ni pesa kidogo na wake yenu haitakuwa na maumivu zaidi kubeba maji.

Watu wakaduwaa kabisa!

Mzungu akaropoka tena:

Mbona watu mko pumbu wazi? (Alikuwa ana maanisha bumbuwazi

lililowapata wanakijiji! Wanakiji wakaanza kuzoza chini chini

hatimaye sauti zikawa za juu wakimuuliza Mzungu kwa nini

amewatusi kiasi hicho.)Mzungu wa watu akazidi kubomoka kiswahili:

Mzungu:

Pepo kubwa inafanya mitombo kufanya kazi bila kulala na visimi yenu

kutoa maji salama na mama wamepata uja zito na watoto yenu wanakuwa salama!


Wanakijiji wazidi kuzoza.


Mzungu:Nasema sikiliza watu wote, Kima, Nyama zenu!!!

Hapa alikuwa akitaka kusema watu wote kaeni kimya, nyamazeni!

Mzungu wa watu baada ya kufanikiwa kuwanyamazisha wananchi

akaendelea kuwaambia kwamba ameridhishwa na hali ya usafi wa visima

ikilinganishwa na siku za nyuma.


Mzungu wetu akaendelea kusema:

Mzungu:

Mimi na uke yangu tumechota maji kutoka visimi yenu na kuyaweka kwenye chupi yetu!

Akimaanisha wamechota maji toka kwenye visima na kuyaweka kwenye chupa.

Akazidi kubonga:

>

Mzungu:

Sasa mimi na uke yangu tutatoa chupi yetu na tutakunya mbele yenu!

lahaula lakwata wanakijiji waanza kuondoka:

Alikuwa anamaanisha kwamba watayamimina maji na kuyanywa mbele yao

ili kuwathibitishia kwamba ni safi na Salama.

Lugha ya watu bwana...

Friday, June 22, 2007

Zanaki Girls Secondary School (ZASESCO)


Baada ya Disco 1979 shule ya wasichana ya sekondari Zanaki. Kati ni Mwalimu wetu wa Physics Mr. Tamba, wakati huo alikuwa anasoma Education University of Dar es Salaam ,Fourth year, na kaja kufanya Practicals.

Tuliomzunguka, mbele kabisa mimi, kulia kwangu ni Natujwa Mbagga ambaye siku hizi ni Mama Shilla. Patricia Kassamia, mwenye bun (nimesahau jina), Kulthum, na huyo dada mwingine alikuwa anasoma darasa la Commerce.

Hapa ni baada ya Study Group tukiwa Form Four 1980. Watoto wa Aga Khan nursery walikuwa wamekwenda nyumbani ndo tukavamia playground yao kwa ajili ya kupiga picha.

Mbele kuanzia kushoto - Mimi, Lilian Maganga, Emily Mbagule, Theresia
Nyuma kuanzia kushoto - Dorothy Kihampa, Neema Kingswaga, na (Jina nimesahau)

Hapa ni Darasa la Form Four Science One! Sayansi Wani! (Enzi hiyo top floor kwenye corner) na tulikuwa wanafunzi 25 tu kwenye hiyo darasa. Tulikuwa wasomi kweli, maana mwalimu alikuwa antoa tuition bure, lakini wachache walibakia kuifaidi. Karibu wote walioenda Form Five kutoka Zanaki mwaka huo walitoka darasa letu la Science One.

Mbele, kuanzia kushoto -Demetria Joseph, Lucy Masamba, Rosemary
Nyuma, kuanzia kushoto -Dorothy Kihampa, Batuli, na mimi

Historia fupi - Kabla ya kuwa Zanaki Girls, ilikuwa Aga Khan Girls School. Shule ilitaifishwa baada ya Azimio ya Arusha. Katika hiyo compound kulikuwa na shule ya vidudu (private) na shule ya msingi na Hostel. Nasikia Hostel imerudishwa kwa Aga Khan.

Sketi za bluu. Tulianza kuvaa sketi za bluu nikiwa Form Two. Kabla ya hapo walikuwa wanavaa sketi za kijani. Nakumbuka walifanya kama fashion show asubuhi wakati wa mazoezi na gwaride na hiyo design ya bluu ilichaguliwa.

Thursday, June 21, 2007

Mimi na Marehemu Ernest Millinga (1993)



Hapa niko na Mzee Ernest Millinga ambaye alikuwa mpiga picha mkuu wa gazeti ya serikali ya Kiingereza, Daily News.

Hapa tulikuwa kwenye 'assignment'. Tulikuwa kwenye meli fulani pale Ferry Dar. Nadhani ilikuwa kuhusu mambo ya kujenga daraja pale Ferry.

Picha ilipigwa 1993 na mpiga picha maarufu, Muhidini Issa Michuzi.

Article kuhusu Bongoland II


Mtengeneza sinema Josiah Kibira, na timu yake watatua Dar hivi karibuni kutengeneza sinema, Bongoland II (Nyumbani ni Nyumbani).


Darhotwire wameandika kuhusu sinema ya Bongoland II.




Monday, June 18, 2007

Waandishi wa Habari wa Daily News


(Kushoto, Dr. Mwamoyo Hamza, Kati, Lady Diana Kibodya, kulia, Chemi Che-Mponda)

Wikiendi hii tulisherekea 50th Birthday, ya Mama Diane Kibodya (Lady Diana), huko Springfield, Massachusetts. Ndugu na marafiki walitoka sehemu mbalimbali kusherekea.

Kwa bahati sisi watatu tuliowahi fanya kazi Daily News (TSN) na kusoma Tanzania School of Journalism (TSJ) (miaka mbalimbali) tulikutana na kupiga picha ya kumbukumbu. Mimi nilikuwa chipukizi kwa Dr. Mwamoyo na Lady Diana lakini walinifundisha mengi. Nawashukuru.

*******************************************************************

Kibodya Family watoa Shukurani

From an e-mail message 6/18/07

Dear Friends:

On behalf of Lady D, we the Kibodyas give many thanks to you and your family for coming to join us in Lady D 50Th Birthday Party. We could not do it alone, definitely your help has made this event "unique" in many ways. Thank you for your help, thanks for your time and resources. May The Almighty God reward you well.. Amen!

For some of you who could not attend because of other obligations, we know deeply in our hearts that you had good intentions and may The Almighty Lord reward you well.

All of you have a permanent place in our hearts for your kindly words, gifts, helping in cooking, taking pictures and video camera as well as for those tireless, the most talented DJ's who came all out to showcase their skills! (Paul Massudi, Samora and Rich Maka) Without forgetting our flamboyant outstanding MC "Mzee wa Ngwasuma!" Emmanuel Bandawe! What a talent!

I am sure you saw the dance! If you missed asked somebody! Our daughter Hawa and her 3 friends gave us an African "high energy" dance and we give special thanks our sisters and brothers from South Africa who did acapella songs and showed us how the banqanga dance is performed.

Thanks to all of you who travel from far and for those who live near and special thanks to "Father Chui" for your hospitality my family and I know we can count on you! This Email cannot be enough to thanks each and every individual but we chose to use as a mean of quicker communication and I have started to call each one of you to thank you personally!

Shukran!

Isaac A. Kibodya, Esq.,

Lady Diana Kibodya Asherekea 50th Birthday!

Lady Diana witnessed the murder of Hector Pieterson by racist police.
Lady Diana Kibodya receives well wishes from a guest. A South African Guest leads a South African Dance


Lady Diana joins in a South African Song

Springfield Tanzanian Dance Group


Lady Diana Kibodya, alisherekea miaka 50 toka azaliwe katika Party kabambe iliyofanyika Springfield, Massachusetts siku ya jumamosi, juni 16. Ndugu na marafiki walitoka sehemu mbalimbali kusherekea naye.

Party ilifunguliwa kwa wageni kuimba wimbo wa taifa wa Afrika Kusini, (nkosi sikelel iAfrika) na wimbo wa taifa wa Tanzania. Asili yake Lady Diana ni Afrika Kusini. Pia walitoa shukrani kwa nchi ya Tanzania kusaidia sana katika ukombozi wa Afrika Kusini na hasa kutoa hifadhi kwa wakimbizi. (Mnakumbuka makambi ya Dakawa na Mazimbu?) Kwa kifupi wanafunzi waliandamana kupinga kufndishwa kwa lugha ya makaburu ya Afrikaans. Waliandamana kwa amani lakini polisi mbaguzi alianza kufyatua risasi ndipo vijana 20 walipoteza maisha yao.

Lakini watu wengi hasa vijana waliohudhuria sherehe hiyo walipatwa na butwa kusikia habari zake. Karibu kila mtu alijua kuwa asili yake ni Afrika Kusini. Lakini hawakujua kuwa alishuhudia kijana, Hector Pieterson mwenye miaka 12, alivyopigwa risasi na askari wa kibaguzi wa Afrika Kusini. Picha ya tukio hiyo ilisambazwa kwa wageni (picha ya kwanza kabisa).
Mume wake, Lady Diana, Bwana Isaac Kibodya, alisoma risala ambayo ilisimulia historia ya mke wake, na watu wengi walishikwa na machozi. Baada ya Hector kuuwawa, askari wa BOSS (polisi wa kikatili) walianza kusaka wanafunzi hao. Ilibidi wakimbie nchi yao kwa kutembea hadi Swaziland kwa mguu. Alisema kuwa wanafunzi wengine hawakufanikiwa kutoroka, lakini yeye alifanikiwa kufika Swaziland, halafu alipelekwa Uganda, na hatimaye Tanzania.

Tanzania alisoma Chuo cha Waandishi wa Habari, na Chuo cha Ustawi wa Jamii. Alikutana na mume wake, Isaac Kibodya, mwaka 79. Bwana Kibodya alifurahisha watu alivyosema, " Diana alikuja kwenye birthday party yangu ya kusherekea miaka 23, toka skiu hiyo alikuwa wangu!"

Lady Diane alikuja Marekani kusoma mwaka 1985, New Hampshire. Hivi sasa anakaa Springfield, Massachusetts na familia yake. Lady Diana na mume wake wana watoto wanne na mjukuu moja wa kiume.

Mungu ambariki Lady Diana na aweze kusherekee 'birthdays' nyingi zaidi.

Kwa habari zaidi ya SOWETO UPRISING someni:




Friday, June 15, 2007

Halahala mnaosema mtoto si wako!




Miaka mingi nimeudhika sana na tabia ya wanaume kukataa watoto wao. Wanatembea na mwanamke, anapata mimba, na wanasema si wakwao. Mwanamke anabisha, na wanasema oh huyo mwanamke malaya katembea na wengine, huyo mtoto si wa kwangu. Nasema Shenzi Taipu mkome tabia yenu mbaya!

Halafu ndugu wanasema oh, sijui tungojeee tuone mtoto anafanana na nani. Loh, je kama mtoto anafanana na mwanamke na ndugu zake ndo mmepata kisingizio. Eh he! Si nilikuambia huyo mtoto si wakwangu. Pumbavu kabisa nyie wanaume, cheki dental formula ya mtoto mbona ina fanana na yako. Au mtoto kazaliwa na vidole sita kwenye mguu kama wewe, japo sura kafanana na mama yake. Wanaume kwa kupenda kukwepa majukumu yao!

Miaka mingi wazungu wamekuwa na njia za kugundua baba mtoto hasa ni nani. Walikuwa wanapima damu. Lakini siku hizi kuna 'fail proof' njia ya kuhakisha nayo ni DNA Testing. Na kama ulikuwa hutaki kupima utapimwa tu, maana kajinywele kinatosha kupima. Kama uliacha shahawa kwenye shuka inatosha kupimwa hata kama imekauka. Kama ulikuwa unapiga busu na mama mtu na kuacha denda kwenye blausi yake, inatosha kabisa kupata hiyo DNA. Hata kama umegusa mahala unaweza kuacha chembe chembe za ngozi na kupimwa DNA!

Kesi maarufu za DNA ni:

Mtoto wa marehemu Anna Nicole Smith. Wanaume wanne waligombania mtoto wake wa kike, DannieLynn na kudai ni wakwao kwa vile alitembea nao. Huyo mtoto ni bilionea maana anarithi mapesa ya mama yake. Basi, Anna kaolewa na mwanasheria wake, Howard Stern, huko wanaume wengine wanadai oh, mtoto wa kwao. Wote walipimwa DNA. Kumbe baba mtoto ni wa mpiga picha, Larry Birkhead. Duh! Baada ya testi huyo stern alimkabidhi mtoto kwa Birkhead bila ubishi wowote.

Na kwa sasa mcheza sinema Eddie Murphy anapimwa kwa ajaili ya mtoto aliyezaa Spice Girl Melanie Brown. Murphy anaseme mtoto wa Scary Spice si wa kwake, lakini mmh sijui kwa kumtazama tu naweza kusema hakuna haja hata ya kupima mtoto ni wa Murphy. Anywy, hiyo DNA test ndo itamaliza maswali yote.

Prince Harry, mtoto wa marehemu Princess Diana na Prince Charles (?) wa Uingereza. Watu wanadai ni mtoto wa mpambe wa Diana, James Hewitt, maana katembea naye akiwa ameolewa na Prince Charles. Harry mwenyewe anataka DNA test kujua nani baba yake amalize maswali ambayo yamemsumbua miaka mingi.

Ngoma ya Tap Dance



Wapendwa wasomaji, bado ninanendelea kujifunza ngoma ya waMarekani, Tap Dance. Jumapili iliyopita tulifanya maonyesho kwenye Dance Complex, Central Square, Cambridge. Hapa niko kwenye studio nafanya mazoezi.

Mwakani nikibahatika nitaenda New York, kuchukua kozi fupi ya Tap na Mwalimu maarufu kama Savion Glover.

Kwa habari zaidi kuhusu Tap Dance nenda:

http://www.tapdance.org/

http://www.atdf.org/

Niliwahi kublog kuhusu Tap Dance mnaweza kusoma hapa:

http://swahilitime.blogspot.com/search/label/Tap%20Dance

Tuesday, June 12, 2007

Rais Bush aiibiwa Saa yake Albania!


Kuna habari kuwa Rais Bush ameibiwa saa yake ya mkononi akiwa kwenye ziara Albania. Wanasema kuwa Bush alifurahi sana jinsi wananchi wa walivyokuwa wanamshabikia kiasi kuwa aliamua kwenda kuwasalimia. Hiyo kusalimiana na wananchi haikupangwa. Ndo hapo wajanja wakawai saa yake.
Wengine wanasema hata pete yake ya ndoa ilibiwa pia.

Wanasema saa ilikuwa ya bei mbaya kweli. Lakini bila shaka ilikuwa na inusrance kali kama Lloyds of London.
Serikali ya Marekani inakataa kuwa saa yake iliibiwa. Lakini mbona video haidanganyi? Mara unaona saa mara haipo. Cha kuchekesha msemaji wake, Tony Snow, kasema "Baada ya kutazama video tulithibitisha kuwa saa yake haikuibiwa." Jamani! Kama haikuibiwa kwa nini mlitazama video kuona kama imebiwa?
Kwa habari zaidi someni:

Marudio - OmbaOmba


Leo nimeona nirudie topiki ya ombaomba hapa Boston. Nikitokea South Station kwenye subway leo asubuhi kuna ombaimba fulani anaitwa Gus, alikasirika na kutupa hela kwenye sidewalk. (Kisa alipewa pennies (senti moja moja). Huyo Gus amekaa pale miaka na miaka zaidi ya miaka 15. Kila siku hakosi, wakati wa Lunch makao yake ni Federal Street. Wikiendi anazunuguka kwenye subway siku nzima, kula kwake ni pale Food Court ya South Station. Hizo pennies alizopewa na huyo mzungu mwanamke zilikuwa anyingi kidogo, basi kazitupa chini kwa hasira. Kazoea noti.

Nashangaa sana. Hao si wanasema wanataka spare change? Lakini ukiwapa na hazitoshi wanatupa chini kama kukutukana. Hao ombaomba wana viwango vyao na kama huna usiwape chochote. Mara nyingi wanakuwa na hela kuliko wewe mfukoni.

****************************************************************
From: December 31, 2005

Hapa Boston kuna ombaomba kibao! Tena wengi ni wazungu. Hao ombaomba wengi wao ni walevi na watumia madawa y kulevya na wenye ugonjwa wa akili. Miaka nenda, miaka rudi, ombaomba ni hao hao!Unapita njiani, unasikia “Spare Change”! Utaona mtu kasimama na kikombe chake anakitikisa. Kuna wengine usipowapa kitu wanakutukana matusi ya nguoni.

Halafu kuna wale wakali wanakufuata mpaka ndani ya ATM. Basi watu kwa uoga wanatoa walichonacho na kuwapa kwa kuhofiwa kupigwa au kuibiwa. Haya, lakini ni lazima niongelee kitu ambacho nimeona, na labda wengine hapa USA mmeona. Kuna ubaguzi katika kile watu wanachotoa kwa ombaomba. Tuseme mtoaji ni mzungu, na ombaomba ni mweusi, basi kama atampa kitu anampa vichenji. Huyo huyo mzungu atatoa noti kwa ombaomba mzungu. Nimeshuhudia mara nyingi tu.

Nimeona ombaomba wa kizungu wakipewa noti za $1, $5, $10 na hata $20! Lakini mweusi atapewa vichenji, kwa nini? Je, ni kwa vile mzungu anajisikia vibaya kuona mzungu mwenzake katika hali hiyo, hivyo ni jitihada ya kumwinua? Je, ni kwa vile anaona kuwa mweusi ni hali ya kawaida kuwa maskini? Sijui kama tutaelewa sababu. Halafu utaona weusi wako tayari kutoa kwa yeyote. Atampa mzungu, atampa mweusi lakini mara nyingi nimeona weusi wakisaidia weusi wenzao kuliko mzungu. Kisa, anajua kuwa yule mzungu anaweza kuishi maisha mazuri akitaka maana Marekani maana bado kuna ubaguzi Marekani.

Lakini nisiseme kuwa wazungu wote ni wabaguzi, maana mwaka juzi kuna ombaomba Cambridge, anaitwa Ramsey, alikuwa amesimama pale Memorial Drive. Basi Mzungu jike tajiri kapita ndani ya gari yake ya fahari na kampa noti ya $100. Ndiyo kampa dola mia moja! Halafu mzungu kamwambia Merry Christmas, maana ilikuwa Christmas Eve. Lakini jambo kama hiyo kutokea ni bahati nasibu.Utaona wazungu wana jaribu kusaidia wazungu wenzao kupata public housing na huduma zingine. Lakini mweusi anaweza kupitwa. Kuna magari ya kuwasaidia zinapita mitaani, lakini hebu cheki, hao ‘volunteers’ wataenda kwa wazungu kwanza halafu mweusi ataambulia kilichobaki.

Ajabu na si kitu cha kushangaza sana ni kuwa hao ombaomba wa kizungu wakienda kuoga, ku-shave, kuchana nywele na kuvaa vizuri, anaweza kupata kazi kabla ya wewe mweusi na digrii zako!Na kama hamniamini ukipita barbarani tazama mwenyewe. Ngoja niishie kwa leo, na kwa maksudi sijaongelea habari ya welfare, na shelters maana hii blogu ingekuwa ndefu mno!

Nairobi Red Eye umeingia Tanzania Tena!




Nasikia ule ugonjwa wa 'Nairobi Red Eyes' (Conjuncivitis) umeingia tena Tanzania. Huo ugonjwa mbaya kweli maana unasambaa kirahisi sana. Wagonjwa walalamika kuwa ni kama vile kuwa kwenye michanga kwenye macho. Pia macho yanatoa machozi na tongotongo kwa wingi. Waznungu wanaiita 'pink eye'.
Jinsi pekee ya kuepukana nayo ni kunawa mikono kila mara, na usifikiche jicho/macho. Ukishake hands na mtu vijidiudu vinasambaa ukigusa alipogusa mwenye nacho pia unaweza kuambukizwa. Pia usi-share dawa ya macho ya mgonjwa.

Huo ugonjwa ulianza kuitwa Nairobi Red Eyes baada ya kuwa epidemic miaka ya 80. Haikukawia na ugonjwa huo ukaingia Dar es Salaam na kuwa epidemic. Ndo watu wakaanza kuita Nairobi Red Eyes kwa sababu waliona ilianzia Nairobi. Wakati ule maji shida, basi ilikuwa vigumu watu wanawe mikono kila mara, ndo ulikuta kila kona mtu mgonjwa, unamkwepa.
Kaeni Macho!

Monday, June 11, 2007

Kwa Heri Sopranos!



Sijui kama mlikuwa mashabiki wa Sopranos. Jana ilikuwa mwisho wa hiyo show. Na watengenezaji waliacha watazamaji kwenye mataa iliishia vipi. Walitumia Njia ya 'Fade to Black' kumaliza show. Kwa hiyo sisi watazamaji tubakie kujadili Sopranos iliisha vipi.

Mimi nimekuwa mshabiki wa Sopranos kama mwaka moja hivi. Nilikuwa nasikia watu wakiongea kuhusu Sopranos lakini wala sikutazama miaka yote hii. Ila nilianza kutazama kwenye reruns. Comcast wana On Demand, na uliweza kuonza Seasons zote. Kwa muda mfupi nilijua habari za Big Pussy, Christopher, akina Aprile na wengine.

Basi nikaanza kuzitama na kugundua kumbe Sopranos ni nzuri. Huyo Tony Soprano, japo ni mobster ana maisha na familia, na marafiki na watu wanaomwabuud na wanaomwogopa, na pia alikuwa amejaa ashki ya uzeeni. Episodes nyingi walimownyesha Tony akifanya mapenzi na wanawake wasio mke wake. Wengine waliweza kuwa hata umri wa binti yake, wazungu wanaiita 'mid life crisis'.

Lakini ilikuwa kila ukimzoea character, huyo anauliwa! Kifo nilichofurahia ni cha mshenzi Ralph, aliyeua fariai wa Tony Soprano. Ralph alikuwa kichaa anaua watu kwa kufurahia kweli. Kifo nilichosikitika kuona ni cha Bobby Bacala, wiki iliyopita. Huyo baba, alikuwa mpole na alikuwa anajali watu, lakini Tony alimlazimisha kwenda Canada kuua mtu. Bobbby aliuliwa kwenye Toy store.

Yule Baba mdogo wa Tony, Uncle Jr. jana walimwonyesha hana akili kabisa, zimefyatuka shauri ya ugonjwa wa Alzheimers. Na Silivio aliyekuwa concilieri (mshauri) wa Tony alipigwa risasi wiki iliyopita na sasa yuko kwenye coma.

Mtoto wa Tony A.J. maskini ya mungu, show ingendelea nadhani anefanikiwa kujiua. Tokea yule binti mDominica amwache amekuwa kama mwehu hivi. Na hata siku moja atakuwa katili kama baba yake.

Binti yake Tony, Meadow, naona atafanikiwa kimaisha. Anasomea sheria. Na inaelekea ataolewa na rafiki aliyekuwa anatembea naye kisirisiri.
Dada yake Tony, Janice, kawa binadamu alikuwa anajadili ataishaje na watoto wa marehemu mume wake, Bobby Bacala. Hao watoto wa Bobby ni yatima, maana mama yao alikufa kwenye ajali ya gari, ndo Bobby kamwoa Janice.
Paulie, yule mzee rafiki yake Tony mwenye nywele kama vampire, haachi kuchekesha. Jana kasema eti paka ni nyoka mwenye manyoya (fur). Kisa Tony katokea kumpenda paka wa mitaani. Ajabu huyo paka alipena kukaa na kulia mbele ya picha ya Christopher, aliyeuliwa na Tony. Je, roho ya Christopher imo ndani ya huyo paka?
Kuna mengi ya kusema kuhusu Sopranos, nadhani kwa vile imekuwa na washabiki wengi huenda wakatengeneza sinema za Sopranos. Na wakitengeneza mtasikia kuna Sopranos Movies hata 20!

Asante HBO kwa hadithi tamu ya The Sopranos.

Saturday, June 09, 2007

African Americans Remember their Slave Ancestors



Siku ya jumamozi, 6/9/07) waMarekani weusi walikumbuka mabibi na mababu zao walioibwa kutoka Afrika na kulazimishwa kuingia utumwani. Japo ni wachache waatakaohudhuria ni vizuri kuona wapo wenye moyo wa kukumbuka wahenga.

Watumwa waliteswa na kusihi maisha duni sana huko wakijenga taifa la Marekani. Shukurani yao ilikuwa ubaguzi ambao mapak leo weusi wanaiona Marekani.

Mungu awape nguvu na umoja.

****************************************************
June 9, 2007 CHARLESTON, S.C. (AP) -- Eighteen years ago, Tony Akeem organized a ceremony in New York City to honor the millions of Africans who died crossing the Atlantic during the slave trade. Similar observances have since spread around the world.

Today , offerings of water, honey and rum were to be poured along the shores of South Carolina and elsewhere for Middle Passage Remembrance Day. The remembrance is held the second Saturday in June.

"We must, we must, honor our ancestors," said Tony Akeem, who has been organizing an observance at Coney Island, N.Y., ever since a 1989 conference on the slave's brutal trip was held at Medgar Evers College in Brooklyn, N.Y., where he works as a photographer.

The observances have spread from Philadelphia to San Francisco and from Brazil to Ghana. Most were started by people who have attended the New York event, Akeem said.

Saturday marked the 10th year South Carolina was participating in the remembrance. As many as 100 people were expected at a Fort Moultrie dock on Sullivans Island near Charleston.
The first slaves arrived in Charleston in 1670, the same year the Carolina colony was created. Historians estimate nearly 40 percent of the millions of slaves brought to what became the United States passed through Charleston. Many others died at sea.

"The stories run pretty strong that there were people who realized they were enslaved and would rather drown than be enslaved and when allowed up on the decks, would just jump into the water," said Fran Norton of the Fort Sumter National Monument, which includes Fort Moultrie. "It commemorates those people who gave up their lives for freedom."

Just how many perished in the slave trade will never be known.

"We know that many died of disease because they were packed in the ships like sardines," said Osei Terry Chandler, a project director at a Charleston education facility who is helping organize the South Carolina memorial.

Participants at the ceremonies in New York and South Carolina planned to drizzle water, rum and honey into the waves Saturday. Some were to toss flowers into the coastal waters. Some were to beat drums.

"Pouring libations is simply to venerate your ancestors," said Bill Jones, who helps organize the Coney Island ceremony. "It gives the ancestors a cool drink of water, or a little bit of gin or a little bit of rum, whatever you pour the libation with.

"In African spirituality we believe we are in constant contact with our ancestors. They are not someplace in heaven, they are right here with us."

Mkenya yuko jela New Hampshire baada ya kutarisha maisha ya Mtoto!


MKenya Esther Ngari (20)anshsikiliwa na polisi, wa Nashua New Hampshire, kwa dhamana ya $50,000 baada ya kuhatarisha maisha ya mtoto aliyekuwa anamwangalia.
Esther alikuwa ana babysit watoto wadogo wawili, moja alikuwa na miezi 18 and mwenzake alikuwa na miezi sita tu. Hakujuana nao mpaka jana hiyo hiyo.
Sasa huyo mwenye miezi kumi na nane alienda chumbani kwake na kula vidoge vya Esther vya ugonjwa wa kifafa. Wakati huo Esther kalala. Angetoa taarifa mapema kuhusu tukio isingekuwa shida sana. Tatizo ni kuwa Esther alijua kuwa mtoto alimeza vidonge lakini hakusema kitu.
Baba wa watoto alikuja kuchukua wanae. Aliona kuwa mtoto anapata shida kukaa macho na pia alikuwa anashindwa kunyayua kichwa. Walivyofika nyumbani mtoto alianza kutapika ndo kapiga simu 9-11. Mtoto alikuwa hoi kiasi kuwa ilibidi apate MedFlight (ndege) hadi Children's Hospital Boston.

Madakatari wana wasiwasi kuwa huenda, ubongo, ini ,na moyo wa mtoto zimehairibiwa. Anasema kama Esther angesema mapema mtoto asingeugua kiasi hicho.
Polisi wanasema kisheria ilikuwa jukumu la esther kuhakisha kuwa mtoto hawezi kupata hizo dawa.
Kesi itakuwa mahakamani wiki ijayo, lakini kwa sasa vyombo vya habari vimerukia habari hizo. Esther amekuwa nchini Marekani kwa miezi mitano tu. Alikuja kama mwanafunzi. Aliwaambia polisi kuwa aliaacha mfuniko wa chupa ya dawa wazi kwa vile ilikuwa shida kuifungua. Hapa wanatengeneza vifuniko vya dawa, 'childproof' kusudi watoto washindwe kufungua.

Kwa habari zaidi someni:

Friday, June 08, 2007

Paris Hilton alie tu!








Binti tajiri na aliyeharibiwa kwa unasa, Paris Hilton, (26)amerudishwa jela huko Los Angeles, California.

Binti huyo anyejiona mrembo kuliko binadamu yeyote duniani na aliyezaliwa katika utajiri wa ukoo wa Hilton (Hilton Hotels), alitoka jela ghalfa siku ya Alhamisi, baada ya kukaa siku mbili tu alisababisha mzozo mkubwa kwenye vyombo vya habari Marekani.

Mchungaji Al Sharpton alisema, "Paris angekuwa ni mtu maskini, au mwanamke mweusi angekuwa bado yuko jela!" Ajabu watu wengi wanaopingana na mawazo ya Sharpton walikubaliana naye. Mweusi au maskini asingeweza kutoka jela Marekani kwa kusingizia atapata kichaa. Lazima pesa zilitembea.

Leo, Paris huko mahakamani kamlilia mama yake kama mtoto mdogo. Kama vile kusema "mama hebu walipe hao wapuuzi waniachie".

Alivyotoka jela Alhamisi ilikuwa amalizie kifungo chake nyumbani kwake. Nyumba enyewe ni ya kifahari kweli kweli. Na ilikuwa avae bangili kwenye mguu kusudi polisi wajue yuko wapi wakati wote. Ilikuwa akae siku 23, lakini hata tau hakufisha, huyooo, nyumbani!

Kisa cha Paris kuonja jela ni hivi, Septemba mwaka jana alikamtwa akiendesha gari amelewa. Alipewa probation ya miezi 36 and fine ya $1,500. Baada ya hapo alikamatwa mara mbili akiendesha gari bila leseni. Alisema eti hakujua kuwa leseni yake imesimamishwa kwa muda.

Jumatatu alivyoenda jela baada ya kwenda kwenye party ya matajiri, wanasema alikataa kula chakula cha jela na alikataa kulala. Haya yeye kazoea kula kweli mahoteli na restaurants za bei mbaya, chakula cha jela hakiwezi kwa sasa. Lakini nasema akishikwa na njaa atakula tu.

Jaji amemrudisha jela leo na atakaa sentensi yake ya awali ya siku 45. Alikuwa amepunguziwa hadi siku 23, lakini baada ya upuuzi huo kutoea jana Jaji kasema apate fundisho. Awe mfano kwa matajiri wengine Marekani, maana inaelekea matajiri wana sheria yao na maskini wana sheria yao!

Thursday, June 07, 2007

Mheshimiwa Sumaye Atoa Shukrani kwa WaTanzania New England



Mheshimiwa Sumaye na mke wake Esther wakifungua densi.

Leo aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania kwa miaka kumi, mheshimwa Frederick Sumaye, amemaliza masomo yake na kuhutimu shahada ya juu ya Masters of Public Administration kutoka Chuo Kikuu cha Harvard, John F. Kennedy School of Government mjini Cambridge, Massachusetts, USA.

Mheshimiwa Sumaye alitoa shukurani kwa WaTanzania waliomsaidia akiwa masomoni. Alisema kuwa maisha yake chuoni Marekani yamekuwa tofauti na maisha aliyozoea Tanzania ya kuwa na wahudumu, walinzi, wapishi nk. Alisema alikuwa mwanafunzi wa kawaida tu na alikuwa anajipikia, kujifulia, kufanya usafi na kubeba backpack ya vitabu kwenda darasani. Pia alikuwa na homework kibao na mwanzo aliona ni kazi kweli lakini alizoea.

Alicheskesha watu alivyosema kuwa Tanzania alizoea kuitwa 'Mheshimiwa' lakini hapa USA hata mtoto mdogo anamwita, Fred.

Alitoa shukurani kwa waKenya pia waliomsaidia.

Sherehe kabambe iliandaliwa na waTanzania chuoni Harvard ya kumpongeza mhesimiwa Sumaye kwa kuhitimu masomo yake. Sherehe ilihudhuriwa na waKenya, waGanda, waGhana, na waNigeria, na wazungu kadhaa pia.

Mhesmiwa Sumaye anatarajia kurejea Tanzania hivi karibuni.

Wednesday, June 06, 2007

Mjue Mtunzi Sandra A. Mushi



Sandra A. Mushi, ni mwandishi na mtunzi wa kiTanzania. Anajitahidi sana kuandika mashairi, na hadithi za kusisimua. Pia ameandika novels.


Hii ni moja ya mashairi yake:

THE MOMENTS
Remember all the moments for two ...
Attraction
Relaxation
Communication
Stimulation
You used to be my masseuse
You used to be my boo
And much more
But after the diamond ring
You stopped lighting candles and using oils too
Can’t remember the last time we had a hot thing
You used to be my fashion model
You used to be my beauty queen
And much more
But after the white veil on the aisle
You just wear a bath robe and drinking Gin
Can’t remember when you last used a nail file
You used to be my madam
You used to be my whore
And much more
But after the baby
You locked away the toys
and I’ve become a bore
Can’t remember when we last touched, now an ice cold lady
You used to be my dance partner
You used to be my date
And much more
But after the buying the house
You now only get me a beer, TV dinner and a cold plate
Can't remember the last time we went out, a subject I can't rouse
You had that feminine thing going,
Smelt like wild flowers from the Serengeti,

It would turn me on just to see you
Walk into a room
Across the room
Out of the room
Soft, round and proud

You had that serene thing going

Tasted like nectar from the Zanzibar,

It would put a smile on my face just to hear your voice
Speaking
Laughing
Smiling
Fiery, sweet and exotic

The girl next door, with me she has been flirting
My secretary, to me sexy jokes she has been emailing
Your best friend, to me she has been listening
Your sister, with me she has been smiling
The girls next door, wears black like you used to
My secretary, has ginger dreadlocks like you used to
Your best friend, wears the perfume you used to
Your sister, wears the ethnic jewel that you don’t wear
no more
Remember the moments for more than two ...
Hesitation
Attention
Temptation
Situations


Copyright © Sandra A. Mushi All Rights Reserved



http://www.authorsden.com/sandraamushi


http://authorsden.com/visit/viewpoetry_all.asp?Authorid=28003

Tuesday, June 05, 2007

Tangazo


Naomba wasomaji wa blog hii waelewe kuwa blogu yangu siyo journalism, Hakuna editor (Mhariri), na wala si hoji interview na kuandika habari hapa, sina ratiba maalum ya kuandika na wala silipwi. Hii Blogu ni maoni yangu na naandika na kuposti kwa wakati wangu. Na wala habari zinazoandikwa hapa haziwezi ku-qualify kupata award ya journalism, bali zinaweza kupata award ya blogging. Mtu yeyote anaweza kuanzisha blogu yake mwenyewe… hakuna qualifications zaidi ya kujua kuandikia, kusoma na kutumia internet. Asanteni.

Ukiumwa malaria Marekani!


Umewahi kuugua malaria Marekani? Usiombe maana ugonjwa ambao unatibika Bongo, inaweza kukuua hapa. Bora uje na dawa kutoka Bongo kabisa.

Hapa USA hawaelewi kabisa malaria ni ugonjwa wa aina gani. Nawambia huwezi kuipata kupitia kwenye hewa. Nikawaambia kuwa Afrika, m ugonjwa wa malaria ni common vile ugonjwa wa mafua hapa. Watu wengi tu wanapata. Nawaambia inaambukizwa na mbu, tena anopheles mosquito. Hapa Marekani hamna. Kuna siku niliwaambia watu weusi na wazungu wa hapa kuwa niliuugua malaria sana nikiwa Tanzania, wakanitazama kwa mshangao na woga. Utadhani walikuwa wanamtazama Frankenstein yule monster wa kwenye masinema!

Nafahamu wazungu kama wanne ambao wamekufa nao hapa. Kisa madaktari hawakujua wanaumwa nini. Wali safiri nchi zenye malaria na kuugua baada ya kurudi. Pia mara nyingi madatari wa Marekani hawa uzoefu na huo ugonjwa ambao Tanzania ni kama kuugua mafua hapa.

Kuna MBongo kanisimulia kuhusu alivyokuja tu kutoka Bongo miaka ya 80, New York. Anasema alianza kujisikia vibaya na akaenda clinic. Kamwambia daktari kuwa anadhani ana malaria, maana katoka Tanzania hivi karibuni. Heh! Kosa kubwa. Kajaza fomu kwenda CDC (Center for Disease Control). Anasema manesi walikuwa wanamwogopa. Wakawa wanauliza kama wanaweza kuambukizwa. Anasema daktari hakuwahi kutibu malaria na ilibidi angalie kwenye kitabu na kumwandikia prescription ya quinine! Damu ilipimwa na ilichukua siku tatu kupata majibu. Haikuisha hapo, anasema alivyofika nyumbani katembelewa na health officer wa serikali. Wakamwuliza maswali mia kidogo mpaka kaogopa kuwa atarudiishwa Tanzania.

Bahati nzuri haikuwa na malaria wakaacha kumsumbua.

Lakini hivi karibuni kuna jamaa alienda Tanzania, karudi na malaria. Akashindwa kwenda kazini , alichukua siku mbili off na kupiga simu kuwa amerudi kutoka safari lakini anaumwa. Alivyoenda kazini, bosi kamwuliza alikuwa anaumwa nini, jamaa kamwambia, alikuwa na malaria. Heh! Utadhani jamaa alimwambia anaumwa Ebola virus. Jamaa alifukuzwa kazi. Nikamwambia bora ungemwambia unflu au UKIMWI, kulikoni umwambie kuwa una malaria.

Na kuna dada fulani naye aliuugua, tena alipata attack ya kusikia baridi na kutetemeka akiwa kazini. Kazi aliyokuwa anafanya ni ya kuangalia wazee. Huyo alikuwa na bahati walimpa paid leave ya wiki tatu! Lakini aliniambia kuwa alijuta kwa nini aliwaambia maana watu walikuwa kama wanamwogopa.

Naona siku hizi mambo kidogo afadhali, maana kuna tropical disease experts wengi. Wengine walifanya practicals kwenye mahospitali za Afrika na hata Tanzania. Lakini ukimkosa mtaalamu wa kukutibu, Mungu akulinde.

Karibuni mtoe maoni yenu au story zenu za malaria Marekani.

Saturday, June 02, 2007

Marudio - Ulafi wa bia Haipendezi Marekani


Orignally Posted: Tuesday, March 28, 2006


*************************************************************************

Ulafi wa Bia Haipendezi Marekani!Hivi majuzi nilienda kwenye ‘Party’ ya waBongo hapa Boston. Party ilifanyika kwenye basement ya nyumba. Na kama kawaida waBongo walijaa. Na kama kawaida chakula kilikuwa kingi na vinywaji tele. Kwa ‘Party’ waBongo ndo wenyewe maana wanachanga bia na chakula bia shida. Huyo anakuja na kesi ya bia, yule anakuja na kesi, yule anakuja na tray ya mapochopocho, mambo swafi kabisa!

Basi kuna MBongo kashuka kwenye ndege juzi juzi, alikuwa kalala kwenye Lawn Chair ndefu anastarehe huko akipunga upepo wa USA. Jamaa kalala kwenye hiyo lawn chair tena bila wasiwasi wowote, huko anaongea na watu. Nikamcheki, jamaa kalegea kabisa na kikofia kichwani anakula maisha ya USA. Basi chini ya hiyo Lawn Chair alikusanya kama chupa kumi za Heineken.

Nikasogea kwa huyo jamaa kumcheki, kama ni mzima au taira au nini, au labda mtu hajiwezi, ndo maana kalala hivyo. Kuongea na jamaa nikakukuta ni mzima kabisa. Basi nikamwuliza sababu ya kulundika mabia chini ya kiti wakati ziko tele jikoni. Na nikamwuliza kama hapendi bia baridi maana kuziweka chini ya kiti zinapata joto. Nikamwambia jamaa kuwa ni mshamba na anajiaibisha.

Jamaa kabisha kasema yeye ana bia tele chini ya kiti atakuwaje mshamba na hawezi kujiaibisha. Hakuwa na habari kabisa kuwa wageni waliokuwepo walikuwa wanamsema chini chini. Lakini jamaa hakujali maana kajiona kafika! Tena kafika USA.

Nadhani watu wangemwona kafika kama hizo bia kununua yeye, na hiyo nyumba ilikuwa yake.

Kwa kweli tabia zingine za Bongo tunaweza kuziacha Bongo. Maana nakumbuka kwenda kwenye shughuli mbalimbali Bongo, na kuona watu wanakusanya bia chini ya kiti. Hiyo kukusanya bia chini ya kiti watu walikuwa wanafanya wakidhania bia zitaisha. At least walikuwa na akiba na rafiki akija wana kitu cha kumpa. Halafu ilikuwa ni sifa kuonyesha kuwa una hela ya kununua bia zote hizo.
Hapa USA karibu kila mahala kuna liquor store na kuna bia tele. Hela yako tu. Na kwenye party za waBongo hata siku moja sijawahi kusikia bia zimeisha, au zikiisha basi watu wanaenda kununua zingine.Jamani eh, tabisa zingine zinafaa ziachwe huko Bongo. Mnasemaje?

Designer Mustafa Hassanali ajibu hoja za Michuzi blog


Wapendwa wasomaji, kule kwa Michuzi, watu walikuwa wanaongelea sana juu ya nguo alizovaa Flaviana Matata, kwenye mashindao ya Miss Universe. Hasa designer Mustafa Hassanali alitajwa sana.


Sasa kampuni yake imefanya Public Relations na kujibu hoja waliozotoa wasomaji kule. Kweli blogu ya Michuzi imekuwa nzito kuliko site yoyote ya waTanzania.

Photo (Designer Mustafa Hassanali poses with model and Former Miss Tanzania, Nancy Sumary pic from Michuzi Blog)
***********************************************************************************

PRESS RELEASE Dated 1 June 2007
FLAVIANA'S WARDROBE SAGA


First and foremost, we at Mustafa Hassanali Couture would like to congratulate Ms Flaviana Matata for performing well at the Miss Universe Pageant which is attributed to the young girl’s zeal, zest and support from her organisers, sponsors and the people who voted for her. Flaviana prior to being a Miss Universe Tanzania 2007 had an opportunity to be cast to showcase our “Namaste” Collection in January 2007.

Pictures of that Show were published in Issa Michuzi Blog amongst many others. Since May 28 2007, the finals of the Miss Universe pageant, The Issa Michuzi Blog has been flooded with comments, remarks, feedbacks and allegation in regards to the Her Wardrobe, this has been intensified more so, since her arrival back from Mexico.

Mustafa Hassanali would like to clarify, refute and abstain from the following remarks:“bora wangempa deal hassanali ila waliogopa bei si unajua these stingy idiots hu just think of themselves....”
we Appreciate that, the Anonymous, thought of us…. But we would want to make clear, we design, create, construct and embellish as per the clients budget. All good and quality product does come with a price tag. “The biggest hindrance to creativity is budgets” Mustafa Hassanali“

Hivi kaka Michu,gauni lile"jeupe"ambalo hasa ndilo lilitukosesha sisi watz ushindi kwa"mwanamke wetu Flaviana"lilitengenezwa na"designer"wa kitz Hassanali au?? Kama Hassanali ndiye alilitengeneza gauni lile"baya"adhabu yake ni kupigwa bakora hadharani,manake halikutoa kabisa dada yetulets me know kaka Michu,nani hasa alitupokonya ubingwa huu kwa kutumia hila ya kumpa auni baya"jeupe "dada yetu?”

We hereby attest that Ms Flaviana Matata On stage evening gown, Official National Costume, Bikini, Pre-final rehearsal segment gown and her welcome home gown were NOT A MUSTAFA HASSANALI CREATION. Each designer has its own creative IQ which makes that their selling point. We respect it.

As they say “one mans meat is another mans poison” Kwa Kiswahili “Mkia was Nguruwe………….”“michuzi hakuna uzalendo wa kijinga tena la sivyo tutaacha kufagilia, wabunifu wa kibongo hawajafikia viwango kwa hiyo hakuna kuvaa nguo zao kwenye mashindano ya kimataifa la sivyo itakuwa aibu tu, vaeni nguo zao hukohuko bongo mkishatoka mnavaa nguo zenye mvuto zilizo kwenye international standardkwa lile gauni hata kumi bora wamempa sababu alikuwa unique and creative on her own beauty”

we @ Mustafa Hassanali would like to inform the person who wrote this comment, That fashion designers just like other professionals have their Identity. I would like to enlighten the said person that its passion for our work, just like the rest of you, drives us for our daily livelihood. As they Say Charity Begins at Home, Ailinda Sawe of Afrika Sana is a Professional Designer and one of the first in Tanzania with a Degree.

Ally Rhemtullah is another qualified designer from USA whilst Elly Mlaki studied in UK. The Late Kiiza Kahama studied in Paris. We Have So many professional DESIGNERS in Tanzania some who are trained and others are Qualified by Experience.

“Hivi ni nani aliye-design Night Gown yake?? Lile Gown lilikuwa baya kusema ukweli. Jamani Tanzania Designers wengi wabovu sana yaani hata tungemnunulia nguo kutoka Walmart angependeza sana kuliko lile gown baya. Angekuwa na Gown bomba angeweza kushinda. Lakini hata hivyo hongera sana Flaviana Matata.”

As stated Earlier that it was NOT A MUSTAFA HASSANALI.What Ms Flaviana Matata Wore during the pageant, had nothing to do with the Qualification status of designers in “Bongo” but its entire her own judgement, she is above 18yrs old, and that of her Organisation Miss Tanzania Universe.Mustafa Hassanali did design two over the Top Evening Gowns for Miss Flaviana Matata as her personal wardrobe which was commissioned and paid for by Flaviana personally.

ABOUT MUSTAFA HASSANALI COUTURE

Mustafa Hassanali Couture is renowned for its elegance, style, flamboyancy, glamour and glitz that has made it one of the most sought after fashion house in TanzaniaHaving been showcased throughout South, Central, Eastern Africa and Italy, this has influenced his cosmopolitan approach to the world of Fashion in Tanzania. It is his exquisite handwork, detailed beadwork and creative ensemble embellishments that make its designs alive. Whether it’s the corporate wear, Traditional costumes or a Wedding Ensemble… Mustafa Hassanali handles each piece with great care and gives the utmost attention to whole outfit right from first client contact to delivery, a personal touch all through.

True to its policy, each design and Outfit is a masterpiece of work…. A duplicate is NEVER created.That is what makes it unique, a Truly Mustafa Hassanali Affair.
Issued By:press@mustafahassanali.netTel: +255-71-5303880
P.O.BOX 10684 DAR ES SALAAMTANZANIATel: +255-78-4303880+255-22-2668555E-mail: press@mustafahassanali.netURL: http://www.mustafahassanali.net

Thursday, May 31, 2007

Jeff Koinange afukuzwa kazi CNN


Photo from CNN.com

Leo nimesikia habari za kusikitisha kweli. Jeff Koinange, amefukuzwa kazi CNN. Wanasema kuwa mwanamke aliyemtaka kamfanyia mbaya. Haya. Kweli wamepoteza mwandishi aliyejua Africa, na aliyetoa habari za kuaminika. Ni vizuri kuona mwafrika mweusi anaongelea habari za Africa na siyo mzungu. Kweli wamepata hasara na kama kafukuzwa shauri ya mwanamke ni hasara kwa CNN.
Huyo mwanamke anakataa kuwa yeye ndiye alisababisha afukuzwe. Soma habari zake na e-mail walizokuwa wanatumana hapa: