Tuesday, September 02, 2008

Don LaFontaine afariki dunia!



Wengi hamtajua jina lake. Lakini mnajua sauti yake. Don LaFontaine ambaye alikuwa ni sauti ile unayosikia kwenye trela za sinema hapa Marekani, amefariki dunia. Habari zinasema kuwa alifariki wikiendi hii kutokana na ugonjwa wa pneumonia. Alikuwa na miaka 68. Alikuwa mwenye ile sauti nzito sana. Alifanya kuwa sauti kwenye trela, sinema na matangazo 5,000! Sijui nani atamrithi hapo.

Mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni. AMEN.