Tuesday, September 16, 2008

Muhimbili Vipi Tena???

Wadau, bila shaka mmefuatilia kwenye blogu mbalimbali habari za ajali ya gari iliyotokea hivi karibuni ambayo wapiga picha na waandishi wa habari waliiumia. Ukagundulika kuwa mashine ya CT Scan hazifanyi kazi katika hospitali za Muhimbili na Aga Khan.

Nauliza hivi, serikali ina hela ya kununua magari ya fahari, ndege na radar, lakini haina pesa za kununua mashine muhimu kama CT Scan? Na nakubaliana na Dr. Faustine, ni aibu kuwa miaka 47 baada ya Uhuru tuko katika hali hii!

****************************************************************

Kutoka Lukwangule Entertainment Blog:

Kuna tatizo gani Muhimbili?

Haya maneno hapa chini nimeyachukua katika blogu ya drfaustine (http://drfaustine.blogspot.com/). Natambua daktari anajua nini anachoandika na yuko serious katika ishu nyingi hasa zinazogusa maisha ya watu na haya ndiyo aliyoandika katika blogu yake. Something shoud be done, lakini sijui nani anatakiwa kufanya hili.Wakati mwingine unabaki ukishangaa. Hebu isomeni . Lukwangule

*******************************************************

Katika pita pita yangu katika Blogu ya Bw Beda Msimbe nimekutana na stori ya kusikitisha na kufedhehesha inayohusu kukosekana kwa huduma ya muhimu ya CT scan.Kwa taarifa zilizopo ni kuwa mashine ya Muhimbili na ile ya Aga Khan zote hazifanyi kazi.Kwa muda mrefu CT Scan ya Muhimbili imekuwa Spana mkononi.

Huduma hii inazalisha fedha nyingi sana. Kipimo si chini ya Tsh 100,000. Fedha hizi zinazotokana na mashine hii zinakwenda wapi?

Kwa taarifa nilizonazo ni kuwa hakuna fungu maalum lililopo kwa ajili ya matengenezo ya mashine hii. Pia mashine hii haina service warranty. Hivyo mashine ikiharibika inaweza kuchukua kipindi kirefu kabla ya kutengenezwa.

Haijulikani ni idadi gani ya wanaopoteza maisha kutokana na kukosekana kwa huduma nyeti kama hii na ile ya kusafisha figo (renal dialysis).

Siku za nyuma nimepiga kelele sana kuhusu suala la renal dialysis. Wataalam tunao, wafadhili wako tayari kutoa vifaa hivi muhimu, Muhimbili wanajivuta kutoa chumba cha kufunga vifaa hivi!

Swali la kujiuliza ni wagonjwa wangapi wenye ndugu wenye uwezo wa kupeleka wagonjwa wao Nairobi na Johannesburg? Hivi hatuoni fedheha miaka 47 ya uhuru bado tunakosa huduma muhimu kama hizi katika hospitali zetu za rufaa?

CT scan sio kipimo cha anasa, ni kipimo cha msingi katika hospitali za rufaa. Mgonjwa kama Bw Athuman Hamisi anakosa kupata matibabu ya msingi kutokana na madaktari kutojua majeraha katika uti wa mgongo yako wapi, kipimo hiki kingesaidia kujua tatizo liko wapi na kuweza kupata tiba stahili.

Watanzania tunaishi kwa kudra za Mwenyezi Mungu.
NB: Nampa pole mdau Athumani Hamisi. Mungu amjalie apone haraka.

1 comment:

Anonymous said...

Watu wa Tanzania wana tabia mbaya sana gari ikipinduka tu wanakimbilia kwaibia waliopata ajali, ni njia zote za Tanzania, sababu ni nini? umasikini? na huu ni wakati wa mfungo wa ramadhani na wengi wa njia hiyo ni waislamu safi! hii tabia ikomeshwe jamani. mimi nilipata ajali kama hiyo baada ya Kilwa vijiji vitatu kuelekea Dar, nilikuwa katika Suzuki Grand Vitara V6 mimi na my wife wangu na abitia mmoja ni ajali mbaya kama hiyo, nilipata pancha tairi la mbele kulia mwanzo wa daraja nikagonga daraja baada ya gari kunivuta upande mmoja na kushindwa kuirudisha barabarani kwa vile tukio lilikuwa la ghafla baada ya hapo AIR BAGS ZIKAVUMUKA ZIKATUSAIDIA MIMI NA MKE WANGU KUTOGONGA MELE KWENYE KIOO AU MIMI KUJIBAMIZA KWENYA USHUKANI, tukaserereka kuelekea mbugani kwa mwendo wa kasi na kujigonga katika tuta na kupinduka cali pia tulikuwa tumefunga mikanda wote watatu, mungu mkubwa hakuna hata mmoja wetu aliyetoka hata chembe ya damu tulitoka wazima lakini gari ilikuwa nyang,anyang,a na written-off, cha ajabu wwenyeji walikuja kwa fujo wakijuwa tumesha kufa ili wapore kila kitu, mimi nikawahi kutoka ndani ya gari, nikawafunguliwa wenzangu wakatoka na nikawambia ni marufuku mtu kusogelea gari kila mtu awe mbali asiguse gari, nilikuwa na bastola ambayo naimiliki kihalali nikaitowa na kushika mkononi nikasema mtu aguse gari na akione cha moto, wakanywea wakaanza kuwa marafiki wakatusaidia kupata ulinzi wa kulinda gari anagawa si bure tuliwalipa, wakaenda kumwita taariki ambaye aliongozana na katibu wa taarafa, ambao nao walitaka rushwa ya laki 500, 000.00 ili waniandikie ripoti nikakata, wakaninyanganya leseni na insurance yangu, mimi nikaondoka nakaenda kumshitaki kwa mkuu wa mkoa wa polisi, wakanirudishia lesini yangu ila hawakuniandikia ripoti yoyote, hiyo ndo hali halisi ya Tanzania ni rushwa na watu kutojaliana tena utu haupo tena. nakumbuka nilipokuwa mdogo gar zilikuwa zinalazwa nje na asubuhi unaikuta salama, siku hizi jaribu utakuta haipo, mtu akikwana na gari watu walikuwa wanamsaidia kusuku bure, siku hizi ni hatari tupu, mtu hata maji ya kunywa unaweza kunyimwa ukiomba, kwa kweli huu si utamaduni wetu wa kiafrika.