Tuesday, September 02, 2008

Bwana Arusi achinjwa Dar

Jamani, mbona mauaji yanazidi Dar? Wivu kitu kibaya sana. Mola ailaze roho yake mahala pema peponi. Amin.

***************************************************

Kutoka ippmedia.com
Bwana harusi Dar achinjwa!

2008-09-02
Na Mwandishi Wetu, Jijini

Mwanaume mmoja anayedaiwa kuwa mbioni kufunga ndoa wiki hii ameuawa kinyama baada ya kuchomwa kisu na kisha mwili wake kukutwa kandoni mwa barabara.

Taarifa ambazo Alasiri imezipata toka kwa baadhi ya waliodai kuwa ni mashuhuda wa tukio hilo, zinadai kuwa tukio hilo limejiri mishale ya saa 4:00, usiku wa kuamkia jana na kwamba marehemu ametambuliwa kwa jina la Nassoro Shomari.

Taarifa hizo zinadai kuwa bwanaharusi ni dereva taksi aliyekuwa akifanya shughuli zake katika Kituo cha Sinza Madukani Jijini.

Wanadai mashuhuda hao kuwa mwili wa bwanaharusi huyo mtarajiwa ulikutwa katika eneo la Tandale, kandoni mwa njia ya kuelekea Kijitonyama.

Aidha, taarifa hizo zinadai kuwa mmoja wa wale wanaotuhumiwa kufanya mauaji ya dereva taksi huyo ni mwanamke mmoja aitwaye Aisha, anayedaiwa kuwa ni mpenzi wa zamani wa marehemu.

Wakieleza zaidi, wanadai wasimuliaji kuwa chanzo cha kuuawa kinyama kwa dereva taksi huyo ni kisa cha kimapenzi, hasa kutokana na ukweli kuwa wiki hii alikuwa afunge pingu za maisha na mwanamke mwingine na kuwatosa wengine aliowahi kuwa nao hapo kabla.

Wanadai wasimuliaji kuwa kabla ya uamuzi wake wa kutangaza ndoa, marehemu aliwahi kuwa na uhusiano na mwanamke mmoja pale Tandale, jirani na njia ya kuelekea Kijitonyama.

Wanadai kutokana na utamu wa penzi lao, marehemu akafikia mahala pa kujifunga mbele ya mwanamke huyo, kwa ahadi kwamba atamuoa.

``Na tena ndiye aliyempangia chumba hapo Tandale... na alikuwa akimhudumia kwa kila kitu kiasi kwamba mwanamke wa wenyewe alijua kuwa yeye ndiye yeye tu... hakuna mwingine zaidi yake,`` akadai mmoja wa wasimuliaji.

Inadaiwa kuwa licha ya kuwa na ahadi ya kumuoa mwanamke huyo, marehemu alikuja kughairi na badala yake akatangaza kufanya mipango ya ndoa na mwanamke mwingine.

Hata hivyo, inadaiwa kuwa zikiwa zimebaki siku chache kabla ya harusi yake wiki hii, ndipo marehemu alipochepuka kidogo na kwenda nyumbani kwa mpenziwe wa zamani.

``Akiwa huko, haieleweki ni kitu gani hasa kilimkuta... lakini mwili wake ukakutwa kandoni mwa njia ukiwa umechomwa visu,`` akadai mmoja wa watu waliodai kuwa ni mashuhuda.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni hakupatikana ili kuzungumzia tukio hilo la kusikitisha.

Baadhi ya maaskari polisi wameiambia Alasiri kuwa ni kweli kuna tukio la mwanaume kuuawa kwa kuchomwa visu, na ambalo limejiri mishale ya saa 4:00, usiku wa kuamkia jana.

Hata hivyo, wamesema mwanaume huyo ni dereva wa daladala aina ya DCM linalofanya safari kati ya Mbagala na Sinza, likiwa na namba za usajili T 223 AUS.

Wanadai askari hao kuwa juhudi za kumsaka mtuhumiwa Aisha zinaendelea, kwani anadaiwa kutimka baada ya kujiri kwa tukio hilo.

SOURCE: Alasiri

9 comments:

Anonymous said...

Hao ndo WATANGANYIKA...! Mi naona ingependeza sana kama wangeungana na Burundi, Rwanda au Congo ndo mnafanana tabia (kuuwana)! Kuungana na Zanzibar nchi ya wastaarabu ni kutuzalilisha na kutupaka matope! Mimi mpaka ntakufa sijiiti MTANZANIA...! Endeleeni kuchunana ngozi, kuuwa mazeruzeru, mwengine kamuuwa mama yake kwa kugombea ugali! Ha ha ha huyu nae kauliwa bila sababu! Duh hata wanyama porini hawaishi hivyo, haitokei simba kumuuwa simba mwenziwe sembuse mama yake!

Anonymous said...

Khaa! mzanzibar 100% una matatizo. Nyie wazenji ndo vichaa si mliua wanawake wan watoto wasio na hatia kwenye mapinduzi! Watanganyika wastaarabu!

Anonymous said...

HUYU JAMAA NAE NI MNAFIKI KAMA ALISHAAMUA KUTANGAZA KWENGINE ILIKUWAJE AKARUDI KWA HUYO WA ZAMANI? AU ALIKTAKA APATE KIMWISHO-MWISHO? HAYO NDIO MATATIZO YA UZINZI NA UFUSKA. SASA YAMEMFIKA YA KUMFIKA KAUWAWA. NADHANI KWA SISI TULIO HAI TUNA MENGI YA KUJIFUNZA HAPA.

WEWE MZNZ 100% NILISHAWAHI KUKUONYA KUHUSU JINSI YA KUFIKISHA UJUMBE LAKINI BADO HUJANIELEWA. HIZI BLOG ZA WATU WENYE HESHIMA SIO ZA VILAZA KAMA WEWE KAMA HUNA LA KUONGEA NYAMAZA KIMYA. UHALIFU NA MAKOSA HAYANA KABILA DINI AU RANGI KILA PAHALA YAPO.

HALAFU WEWE KWA NINI UNAPENDA UBAGUZI NA KITU KIDOGO NI UZNZ? WAZNZ SISI TUNAWAJUA HAWANA HIYO TABIA YAKO YA AJABU. KAMA UNATAKA KUWAPAKA MATOPE WAONEKANE NI WABAAYA KAMA WEWE NADHANI UMECHELEWA.

CHEMI NAPENDEKEZA HUYU JAMAA AKILETA TENA COMMENT ZA AINA HII ZIWEKE KAPUNI

Anonymous said...

mzanzibar 100% hakuna kitu kama mzanzibar 100%. Watu zenji ni sawa na wamarekani wamechanganywa damu. Lazima una ubara au uarabu.
Na ile aibu waliofanya mababu zako wakati wa mapinduzi kuchinja na kubaka na kuiba yalikuwa ya kikatili. Mshukuru babu zenu Karume na Nyerere kwa kunyamazisha hiyo habari.

Anonymous said...

Mzanzibar 100% sidhani kama unaelimu hakuna nchi inaitwa Zanzibar ila kuna tanzania bara na visiwani ubaguzi atupendi mimi kama mbara uwa naona raha sana nikikutana na ndugu zangu wazanzibar nakuwatambulisha jamani hawa nindugu zangu watanzania wao wametokea zanzibar mimi bara uoni kama inapendeza hapo halafu tunaelewa sana kwasababu wana utu na ubinadamu sasa kama mwenzetu alivyosema hapo juu sijui wewe ni mzanzibar wa wapi.siku zote wananiheshimu mimi kama dada yao hakuna anaesema upuuzi kwangu so get life achana na mambo ya ukabila wewe mtuu

Anonymous said...

wewe unayejiita mnzanzibar100%unachemsha,unapotoa comment zako wewe unakua na chuki yako,au umesahau waliomuua mzee karume ni wanzenj?mimi naona wewe unakunywa supu ya muorobaini,ndio maana akili yako finyu.lakini ukae ukijua zenj hakuna mzenj pure!kuna wamakonde,wanyasa,wamatumbi,wazaramo.waluguru,wasukuma,wanyamwezi,n.k...na washirazi,waarabu koko kama wewe.watumbatu..na hiyo story ya kusema simba hajatokea kuumua simba mwenzie umeitoa wapi?au wewe huangalii national geographic programs?ukaona ji,nsi simba wanavyouuana,yaani wewe unatulinganisha na burundi,ruanda,na congo?kwani hujui ya jirani zetu ni vita,ndio maana wameuwana,kwa muono wangu mimi nakuona wewe huna akili timamu,alafu mimi narudia kwako tena na tena zanzibar itabaki wenye muungano ,hutaki au unataka..hivyo ni kivyako..fala wewe mnzenj koko.

Anonymous said...

wewe unayejiita mnzanzibar100% naona kama una utata katika kujielezea hoja zako,pia wewe unachuki yako ya binafsi,unawajumuisha wazenj wengine wasio na hatia au chuki dhidi ya watanzania wenizawao..usidhani chuki zako zitalipa katika bloggs zote unazotembelea..kama wewe ni mkristo naomba nenda kanisani ukajisafishe.na kama ni muislam nadhani mwezi huu wa ramadhani.wewe huna pesa ya futari..ndio maana unabwabwaja ovyo ovyo tu....naona kilichobaki wewe ingia kwenye blogg ya the utamu utangaze chuki zako na biashara yako kwa ujumla. nimekustukia mtoto wa kiume.unalo lako.
mkongwe

Anonymous said...

sinema za ki nigeria hizo..........nollywood....

Anonymous said...

huyo mnzanzibar 100% mnamuendekeza, just ignore the dude. Ukibishana na mpumbavu watu hawatajua tofauti........Fanya kama hayupo vile kama Zanzibar tulivyoifanya.